Kuanguka mara zote siyo kushindwa, wakati mwingine ni sehemu ya safari ya kujifunza, kukua na kujiandaa kwa ushindi mkubwa zaidi.
#JamiiForums #JamiiAfrica #GoodMorning #AmkaNaJF #Maisha

👍3
Mwandishi wa Andiko la Stories of Change 2021 anasema utakapopata Pesa na Utajiri usisahau kujali Afya yako sababu Ugonjwa wa Kisukari haubagui kati ya Masikini na Tajiri
Anasisitiza kuzingatia Uzito wa Mwili, fuata taratibu za Kitabibu katika Kula, Kunywa Maji ya kutosha, Kufanya mazoezi na kula kiasi kingi cha mbogamboga na Matunda
Soma Andiko hili zaidi https://jamii.app/MatajiriKisukariSOC21
#JamiiForums #JamiiAfrica

❤1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ambaye anafanya Kazi ya Bodaboda anasema haelewi kwanini wenye Magari wakishusha Abiria mbele ya jengo la Kituo cha Treni ya SGR (Zero Kilometer) hawakamatwi kama wanavyokamatwa Bodaboda?
Anadai kibaya zaidi baadhi ya Walinzi wa hapo wakiwakamata wanataka hongo ya Tsh. 10,000, na kama huna wanakupeleka Kituoni kukuandikia faini ya makosa matatu ambapo unatakiwa kulipa Tsh. 30,000. Anatoa wito Mamlaka za juu zifuatilie hali hiyo
Soma https://jamii.app/BodabodaMaegeshoSGR
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wanachama na wafuasi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) wakiwa kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo kunafanyika Mkutano Mkuu, leo Mei 21, 2025
Inadaiwa CHAUMMA inatarajiwa kuwapokea Wanachama wapya takriban 3,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini
Soma https://jamii.app/MkutanoChaumma
#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy

Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Malaka husika na Mtandao wa Waokota Taka Rejeshi Dar es Salaam (MTAWADA) kushughulikia changamoto zinazowakabili waokotaji wa Taka Rejeshi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vinavyowawezesha kujikinga wakati wa kuokota taka hizo pamoja na kudhulumiwa bei ya taka kutokana na mizani kuchezeshwa na Wanunuaji
Soma https://jamii.app/WaokotaTakaKudhulumiwa
#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025

Jukwaa la 14 la Afrika kuhusu Utawala wa Mtandao (AfIGF) linalotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 29 hadi 31 Mei 2025 Jijini Dar es Salaam litawakutanisha Wadau kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Serikali, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia, Watafiti na Vijana kwa lengo la kujadili kwa kina masuala ya maendeleo ya Kidijitali Barani Afrika
#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaKidijitaliAfrika #JamiiForums
#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaKidijitaliAfrika #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Serikali imetoa fedha Tsh. Bilioni 6 kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambayo itajengwa eneo la Magomeni
Pia, imetoa magari mawili mapya kwa Katibu Tawala Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala yenye thamani ya Tsh. Milioni 639 huku Mkuu wa Mkoa wa Dar, Albert Chalamila akisema bado wanahitaji magari mengine zaidi.
Soma https://jamii.app/OfisiMpyaDar
#JamiiForums #Governance #Transparency

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UCHUMI: Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Akaro amesema kwa mujibu wa kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025 bei na malipo ya bidhaa na huduma zote ndani ya nchi yanapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania
Ameongeza kwa kusema ni kosa la Kisheria kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni; kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni; au kukataa malipo yanayofanyika kwa Shilingi ya Tanzania
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika semina ya Waandishi wa Habari iliyofanyika Mei 20, 2025 katika Ofisi za Benki Kuu, Dar es Salaam
Soma https://jamii.app/MarufukuFedhaKigeniManunuzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFUchumi
Ameongeza kwa kusema ni kosa la Kisheria kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni; kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni; au kukataa malipo yanayofanyika kwa Shilingi ya Tanzania
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika semina ya Waandishi wa Habari iliyofanyika Mei 20, 2025 katika Ofisi za Benki Kuu, Dar es Salaam
Soma https://jamii.app/MarufukuFedhaKigeniManunuzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFUchumi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema kilichoingiliwa ni akaunti za Mitandao ya Taasisi na sio Mifumo ya Serikali, akilihakikishia Bunge kuwa Mifumo ya #TEHAMA ipo salama na akaunti tayari zimerejeshwa
Akizungumza #Bungeni, leo Mei 21, 2025, Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, ambapo amesema akaunti hizo ziliingiliwa kutokana na udhaifu wa taratibu za kiusalama katika usimamizi wa akaunti.
Soma https://jamii.app/KudukuliwaAkauntiJerry
#JamiiForums #JamiiAfrica #OnlineSafety #CyberSecurity #CyberAttacks

Ajali ya MV Bukoba ilitokea Mei 21, 1996 katika Ziwa Victoria ambapo taarifa za vyanzo mbalimbali zilionesha Meli hiyo ilitengenezwa na Kampuni ya Kibelgiji na ikazinduliwa Julai 27, 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano.
Ili kupunguza Majanga ya Ajali Nchini, tunajifunza kutokana na makosa au tunaendelea kuyapuuza?
Soma https://jamii.app/MVBukobaMei21
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHistoria #MVBukoba

👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Serikali kupitia Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa imeonya wanaopanga au wanaotarajia kuvuruga Amani wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025 na kwamba Vyombo vya Dola vimejipanga kuhakikisha Uchaguzi unafanyika katika mazingira ya Amani na Utulivu
Akijibu swali la Mbunge wa Malinyi, Antipas Mgungusi aliyeomba kuongezewa Gari la Polisi ili kuimarisha Ulinzi katika Jimbo lake, #Bungeni, leo Mei 20, 2025, Waziri Bashungwa amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kupanga au kuchochea vurugu wakati wa Uchaguzi.
Soma https://jamii.app/BashungwaPolisiUchaguzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #UchaguziMkuu2025 #Governance

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza Mwanaharakati kutoka Kenya Boniface Mwangi, pamoja na Mwanasheria kutoka Uganda, Agather Atuhaire bado hawajapata taarifa kamili wako wapi baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi
Mratibu wa #THRDC Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema Mawakili walipewa taarifa jana, Mei 20, 2025 na Jeshi la Polisi kwamba taratibu za kuwarudisha wawili hao kwenye Nchi zao zimekamilika lakini hawaelewi kwanini bado wameendelea kubaki nao mpaka sasa
Mwangi na Atuhaire walikuja Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, iliyosikilizwa Mei 19, 2025 katika Mahakama ya Kisutu.
Soma https://jamii.app/MwangiAtuhaireTHRDC
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Diplomacy