JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mei 21 kila mwaka Maadhimisho ya Siku ya Chai Duniani.

Mdau unazifahamu aina ngapi za chai?

Mjadala zaidi https://jamii.app/AinaNgapiChai

#JamiiForums #InternationalTeaDay #JFChitChats
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yake, jana Mei 20, 2025 amewataka Watanzania kuendelea kuliamini Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kulipa uhuru na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa

Soma https://jamii.app/WaziriTaxNukuu

#Governance #JamiiForums #Accountability #Transparency #JFNukuu #JFQuote
Vipi Mdau, ulizingatia nini kwenye kumpa Mtoto wako Jina?

Jina ulilopewa na Wazazi/Walezi wako limewahi kukuletea usumbufu wowote Maishani mwako?

Mjadala zaidi https://jamii.app/JinaMtotoKitaa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories #Malezi #Parenting
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya Kusini kimetangaza kuvunja rasmi kambi iliyokuwa imewekwa kushinikiza kupatikana kwa Kada wao, Mpaluka Said Nyagali (Mdude) aliyetoweka tangu Mei 02, 2025

Ikumbukwe Mdude anadaiwa kuvamiwa na kupigwa nyumbani kwake, Mtaa wa Iwambi Jijini hapo, hajapatikana huku CHADEMA ikitumia njia tofauti kumtafuta Mwanaharakati huyo bila mafanikio

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi, Mei 21, 2025, Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Masaga Kaloli amesema baada ya kupata vitisho ikiwamo kumwagiwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni sumu, wameona harakati za kumpigania Mdude zihamie nyumbani ili kuokoa maisha ya wengine.

Soma https://jamii.app/KambiMdudeKuvunjwa

#JamiiForums #HumanRights #Governance #KuelekeaUchagua2025
👍2
Mwandishi wa Andiko hili la Stories of Change 2022 anasema Watu wanaoingia Madarakani wanapaswa kutunza Amani ya Nchi, Kuhamasisha Uzalendo, kuleta Mabadiliko bora, Fursa kwa Haki na Usawa, Haki za Binadamu kuzingatiwa na Utawala bora kutekelezwa kwa misingi thabiti

Soma zaidi https://jamii.app/KigodaUzalendo

#JamiiForums #JamiiAfrica #SOC2022 #Democracy #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amewataka Watanzania kuitumia siku ya leo Mei 22, 2025 ambayo ni ya mwisho kujiandikisha katika Vituo vya Wapiga Kura ili waweze kupata haki zao za kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025

Amesema hayo alipotembelea Vituo katika Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba kukagua zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili

Soma https://jamii.app/KujiandikishaMwisho

#JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy
Mdau wa JamiiForums.com anasema Mfundishe Mwanao awe anasalimia Watu wadogo kwa wakubwa pamoja na Kuwaheshimu Wageni au Jamaa mnaokaa nao hapo Nyumbani. Asiwadharau kwa namna yoyote hasa watakapomkanya jambo kwa namna ya kumfunza

Jifunze mengi zaidi ya kumfundisha Mwanao hapa https://jamii.app/MfundisheMwanaoYafaida

#JamiiForums #JamiiAfrica #Malezi #Maisha #JFStories #JFChitChats
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#JFKUMBUKIZI: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara (Bwege) kupitia #CUF akizungumzia thamani ya Maisha ya Mtu

Mjadala https://jamii.app/BwegeKuuaWatu

#JamiiForums #HumanRights #HakiZaBinadamu
👍3🥰1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#KENYA: Jeshi la Polisi limefika katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Jijini #Nairobi, leo Mei 22, 2025 ikiwa ni hatua ya tahadhari kufuatia taarifa za Maandamano yaliyopangwa na Wanaharakati wanaoshinikiza kuachiwa huru kwa Mwanaharakati maarufu #BonifaceMwangi

Wanaharakati hao wanaandamana kwa Amani wakitaka Serikali ya #Tanzania kutoa maelezo kuhusu sababu ya kushikiliwa kwa Mwangi ambaye walikuja Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, Mei 19, 2025.

Soma https://jamii.app/PolisiUbaloziTZKE

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy
👍1👏1
KENYA: Kituo cha Runinga cha NTV kimeeleza kuwa Mwanaharakati Boniface Mwangi amerejeshwa Kenya baada ya Siku kadhaa za kushikiliwa Jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda fuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu

NTV imeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora, Musalia Mudavadi amesema Mwangi aliachiliwa Asubuhi ya leo Mei 22, 2025 bila kutoa taarifa zaidi

Aidha, NTV imesema Familia ya Mwangi imethibitisha Ndugu yao alisafirishwa kwa Gari na kutelekezwa kwenye Mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Ukunda ambapo kwasasa wamempeleka Hospitali kwaajili ya kuangalia Afya yake.

Soma https://jamii.app/MwangiFreedUkunda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy #HumanRights
😁1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia kero ya mtaro uliopo ya Mtaa wa Karatu (Mbezi Beach) kwa umesababisha changamoto kwa Watumiaji wa barabara hiyo

Soma https://jamii.app/KeroMtaaKaratu

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #JFMdau2025
👍1
Handaki la Lærdal nchini #Norway ndilo handaki refu zaidi la barabarani Duniani ambalo inauunganisha Miji ya Lærdal na Aurland

Ujenzi wake ulianza Mwaka 1995 na kuanza kutumika rasmi Mwaka 2000.

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #Tourism #LærdalTunnel
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com anasema alipomaliza Darasa la saba alipewa kazi ya kupanda miti kwenye shamba la Ekari moja alilonunua Baba yake mpaka muda wa kwenda Kidato cha 1 ulipofika

Pia, alipomaliza Kidato cha 4 alikabidhiwa Shamba la Vitunguu kuanzia kuandaa Shamba hadi kuvuna kipindi cha likizo ya kusubiri Kidato cha 5

Mafunzo yote hayo aliyopitishwa na Wazazi wake anasema yamemjengea Kujiamini na kuw na Ujuzi wa kufanya vizuri kwenye Ajira aliyojiajiri na kuweza kuwasimamia aliowaajiri.

Soma zaidi https://jamii.app/MtotoKufanikiwaMalezi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeLessons #Parenting
1