JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Kasalali Mageni, Mbunge wa Sumve (CCM) amesema Jimbo lake lina Barabara hewa za lami, akidai ni kutokana na kusainiwa kwa mikataba ya ujenzi ambayo haina utekelezaji kwa miaka mingi na kuwa hali hiyo inasababisha wabaki wakipigwa vumbi na Viongozi wa Kitaifa kutofika kutokana na ubovu wa barabara zilizopo

Amesema hayo Mei 6, 2025, Bungeni wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyeomba Bunge limpitishie Tsh. Trilioni 2.28 kwaajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine

Baadaye Waziri Ulega alisema "Mtani wangu usiwe na wasiwasi, nimekusikia na jambo lipo katika vitabu. Nataka nikuhakikishe nina safari ya Mwanza, nitakwenda hadi Sumve na ninajua sasa hivi watani mnapenda sana maendeleo na mimi nataka usikasirike na hutaharibikiwa kwa sababu ya barabara."

Soma https://jamii.app/JimboLaSumve

#JamiiForums #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Bunge la Ulaya (EU) limejadili kuhusu mashtaka yanayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu na kutoa azimio kuwa aachiwe huru bila masharti

Wakichangia hoja hiyo, jana Mei 7, 2025, Wabunge mbalimbali wametoa wito wakieleza haki itendeke katika shauri hilo na kulinda uhuru wa Kisiasa, usalama wa Waandishi wa Habari, Watetezi wa Haki za Binadamu ili kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Bunge hilo na Tanzania

Pia, wamegusia kuruhusiwa kwa Vyama vya Upinzani kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Uhuru na Haki

Soma https://jamii.app/BungeUlayaLissu

#JamiiForums #Governance #Democracy
πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KIGOMA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Aprili 29, 2025 kulitokea taharuki wakati Jeshi la Polisi lilipotumia mabomu ya machozi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, ufafanuzi umetolewa wa kilichotokea

Awali, Mdau alidai baadhi ya Wakimbizi wamekuwa wakiuza pombe haramu na hata walipoonywa na Viongozi hawakujali na walishiriki kuanzisha vurugu Askari walipofika kukagua

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Filemon Makungu amezungumza na JamiiForums na kusema wamewakamata na kuwafikisha Mahakamani Wakimbizi 25 kwa kufanya vurugu na kuzuia maafisa wa Idara ya Wakimbizi kukagua vijiwe vya kuuza bidhaa zilizopigwa marufuku kambini

Soma https://jamii.app/WakimbiziKigoma

#JamiiForums #Accountability
πŸ‘2
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com anadai Wakazi wa Kitongoji cha Miale, Kata ya Mkuranga wakipata dharura gari ndogo au Bajaji haviwezi kupita katika barabara ya Mtaani hapo kutokana na ubovu

Anadai mara kadhaa wamewasilisha malalamiko yao na maombi yao ya kuboreshewa Barabara kwa TARURA, lakini wamekuwa hawapati mwitikio wa kuridhisha, hata wale wanaochota mchanga nao hawashughuliki na maboresho, badala yake wanazidi kuharibu

Anaeleza kuwa eneo hilo linahitaji kifusi cha mawe ili likae sawa, tofauti na hapo Wakazi wa huko watakosa sehemu ya kupita

Soma https://jamii.app/MialeMkuranga

#JamiiForums #Accountability #Governance #ServiceDelivery
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2025/2026, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara hiyo imefikisha Huduma ya Maji Vijijini kwa zaidi ya Asilimia 83 ya malengo yake ya kufikisha Asilimia 85 kufikia Desemba 2025, amesema hayo Bungeni leo Mei 8, 2025

Soma https://jamii.app/AwesoMajiVijijini

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala kuhusu Matumizi ya Akili Mnemba (AI) kwa kuzingatia Maadili (Ethical use of AI) akilalamikia suala la baadhi ya Watu kuitumia AI kudhalilisha wengine, badala ya kujinufaisha kwa kuongeza Maarifa na kipato

Ametoa mfano wa kauli iliyotolewa na mmoja wa Watumiaji wa Mtandao wa X ya kukemea matumizi mabaya ya AI kufuatia matukio ya hivi karibuni

Wewe unaitumia #AI kufanyia nini?

Mjadala https://jamii.app/MatumiziAI

#JamiiForums #JamiiAfrica #AIBenefits #Technology #Cyberbullying
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Biharamulo, Eng. Ezra Chiwelesa amepinga baadhi ya maazimio yaliyotolewa na Bunge la Ulaya, lililojadili kuhusu mashauri ya Mwenyekiti wa #CHADEMA, Tundu Lissu ambapo ametoa wito kwa Serikali kukataa maelekezo ya Bunge hilo

Soma https://jamii.app/ChiwelesaBungeni

#JamiiForums #Governance #Diplomacy
❀1
DAR: Timu ya #Simba imeendeleza mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kasi, hiyo ni baada ya kuichapa #PambaJiji Magoli 5-1 kwenye Uwanja wa KMC Complex

Kiungo mshambuliaji Jean Ahoua amefunga magoli matatu (hat trick dakika ya 15, 36 na 48) huku mawili yakifungwa na Leonel Ateba (80 na 84), goli la Pamba Jiji limewekwa wavuni na Mathew Tegisi dakika ya 85

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 66 katika michezo 25 ikiwa nyuma ya #Yanga yenye pointi 70 katika michezo 26 wakati Pamba Jiji ipo nafasi ya 13 kwa kuwa na pointi 27 katika mechi 27

Soma https://jamii.app/SimbaPamba

#JamiiForums #JFLigiKuu25 #JFSports
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
VATICAN: Robert Francis Prevost (69), raia wa Marekani ametangazwa kuwa Papa Mpya wa 267 wa Kanisa Katoliki, leo Mei 8, 2025 akichukua nafasi hiyo baada ya kifo cha Papa Francis (88) aliyefariki Aprili 21, 2025

Mara baada ya Papa kutambulishwa imeelezwa atakuwa anatambulika kwa jina la Pope Leo XIV

Idadi ya Wapigakura ilikuwa ni Makardinali 133 walio chini ya umri wa Miaka 80 na Mshindi alihitajika kupata angalau Kura 89, sawa na theluthi mbili ya kura zote

Soma https://jamii.app/PapaMpya

#JamiiForums
❀1πŸ‘1
Andiko hili la Stories of Change 2022 limeshauri TANROADS kuwa na Utaratibu wa kukagua Barabara mara kwa mara sabau Watendaji wanapojifungia Ofisini kwa muda mrefu, ndipo hata kunapotokea tatizo Barabarani, inachukua muda mrefu kulishughulikia

Pia, anasema ulinzi wa Miundombinu hii ni wajibu kwa kila Mwananchi. Unapoona walakini mahali toa taarifa kwa wahusika ili wanaposhindwa kuchukua hatua kwa wakati wawajibishwe kwa Ushahidi wa kushindwa kwao

Soma Andiko hili zaidi https://jamii.app/UlinziMiundombinu

#JamiiForums #JamiiAfrica #SOC2022 #Accountability #Uwajibikaji
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, mjadala kuhusu Marekebisho ya Mfumo wa Uchaguzi (Reforms) haukwepeki. Kuna wanaosema reforms tayari zimefanyika, huku wengine vikisema bado kuna kasoro na wengine wakisema hawatashiriki Uchaguzi hadi kasoro hizo zishughulikiwe

Maswali muhimu ni je, β€˜Reforms’ zilizofanyika zinatosha? Kwanini sauti ya pamoja ya Vyama haijasikika? Vyama vingine vinaona umuhimu wa β€˜reforms’? Je, Wananchi wanafahamu mabadiliko yaliyofanywa na kuyaridhia?

Kufahamu haya na mengine, jiunge nasi katika Mjadala, kupitia Xspaces ya JamiiForums, Mei 12, 2025 kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku

Kujiunga bofya https://jamii.app/ReformsSpace

#ElectionReforms #Kuelekea2025 #ReformsSpace #Accountability #Democracy #FreeAndFairElections
πŸ‘2❀1
Warembo mpo? Mdau wa Jukwaa la Urembo, Mitindo na Utanashati (LifeStyle), ndani ya JamiiForums.com amehoji baada ya kusuka Rasta ama vinginevyo, ni kwa muda gani inafaa kuziosha au kusuka tena ili kuepusha usumbufu na Kero kwa wengine?

Wadada, mnafumua Nywele zikianza kutoa harufu au hadi gharama ya kusuka irudi?

Mjadala https://jamii.app/UsafiWaNywele

#JamiiAfrica #JamiiForums #LifeStyle #Maisha
Ripoti ya CAG kwa Mwaka 2023/24 imebaini Miundombinu ya alama za Barabarani katika makutano muhimu Dar es Salaam imepitwa na wakati, hali iliyosababisha hitaji la udhibiti wa foleni kwa Mikono kupitia Askari wa Usalama Barabarani

Aidha, ukosefu wa bajeti ya kutosha umekwamisha juhudi za matengenezo, ambapo Tsh. Bilioni 1.8 hutengwa kwa Mwaka ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Tsh. Bilioni 200

Pia, imebainika kuna upungufu wa alama za Barabarani, ambapo Barabara ya Bagamoyo ina upungufu wa Taa za Barabarani kwa 73%, huku mistari ya Barabarani iliyofifia na ukosefu wa alama za Barabara vikiongeza hatari za ajali.

Soma https://jamii.app/CAGBarabaraDar

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Accountability #Uwajibikaji
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anaeleza kuwa hali ya Mvua imesababisha changamoto ya foleni, katika maeneo mengi ikiwemo Barabara ya Morogoro hasa katika maeneo ya Ubungo, Kimara Mwisho, Stop Over na Mbezi Temboni

Anasema changamoto ya foleni imekuwepo kila siku asubuhi hata kama hakuna Mvua na Mvua ikinyesha hali ndio inakuwa mbaya zaidi. Anahoji, hakuna namna Mamlaka zinaweza kufanya kukabiliana na kero hiyo?

Soma https://jamii.app/UbungoMbezi

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
❀1πŸ‘1