JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHERIA: Wakili Bashir Yakub amechambua kuhusu kosa la Uhaini kupitia andiko lake ndani ya JamiiForums.com, akisema Kifungu cha 39 Kanuni za Adhabu, RE 2022 kinaelezea matendo ambayo yanahesabika kuwa ni makosa ya Uhaini

Soma https://jamii.app/KosaLaUhaini

#JFSheria #JamiiForums #CivilRights
Historia inaeleza baada ya Said Mwamwindi kumuua Dkt. Wilbert Kleruu, Mwamwindi alichukua kofia ya pama ya Kleruu akaivaa, akaubeba Mwili (akisaidiwa na Mtoto wake) na kuuweka kwenye buti la Gari alilokuja nalo Marehemu na kisha kuendesha kuelekea Kituo cha Polisi Iringa Mjini kujisalimisha

Mahakamani, Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamuua Kleruu alirukwa na Akili, ila Jaji aliukataa utetezi huo kwa kutilia maanani kwamba baada ya Mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua Bunduki ambayo aliitumia kuua

Kesi ya Mwamwindi ni miongoni mwa zile chache ambapo adhabu ya kifo ilitekelezwa nchini, kabla ya kusitishwa kwa vitendo kwa utekelezaji wa adhabu hiyo tangu miaka ya 1990

Bonyeza hapa kusoma Historia hii kwa urefu zaidi https://jamii.app/DktKleruuKifoMwamwindi

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKumbukizi #Historia
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema Bunge la Tanzania halijatimiza wajibu wake wa kuwasemea Wananchi katika kushughulikia masuala nyeti ya Kitaifa ndio maana Bunge la Ulaya limeamua kujukua majukumu hayo

Amesema β€œTunaona Bunge la Ulaya ndilo linayajadili mambo yanayopaswa kujadiliwa na Bunge la Tanzania, hii ni ishara kuwa Bunge letu limekosa uthubutu na linaogopa wajibu wake.”

Ameeleza hayo Mei 8, 2025 katika Mkutano wa TLS uliojadili hali ya Kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Soma https://jamii.app/MwabukusiMaoni

#JamiiForums #Democracy #JFMatukio
πŸ‘2
Serikali ya Tanzania imetoa tamko kujibu maazimio ya Bunge la Ulaya yaliyotolewa Mei 8, 2025 kuhusu mwenendo wa mashauri ya Kisheria kwa kueleza kuwa Tanzania inashikilia misingi ya Utawala wa Sheria, Demokrasia na Haki za Binadamu kwa mujibu wa Katiba yake

Tanzania inaendelea kuthamini ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya na iko tayari kwa mazungumzo ya wazi, yenye heshima na yanayozingatia ushahidi kuhusu masuala ya maslahi na umuhimu wa pamoja, ambayo lazima yajengwe juu ya uwazi, usawa, kuheshimiana na uelewa wa uhuru wa Taasisi za kila nchi, Katiba zake na muktadha wa Sheria na Utamaduni wa kila Taifa

Tamko limeeleza kuwa Serikali ya Tanzania inathibitisha dhamira yake ya kulinda amani, kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025 huru na wa haki, kulinda haki na uhuru wa msingi wa Wananchi wote kwa mujibu wa Katiba

Soma https://jamii.app/TamkoLaTanzania

#JamiiForums #JFDiplomacy #Diplomasia #Governance #CivilRights
#MAISHA: Mdau wa JamiiForums.com anasema licha ya kuwa ana Marafiki wengi ila anaye Rafiki mmoja ambaye walijuana tangu Shule ya Msingi, na huwa wanakwaruzana na kupotezeana kwa muda ila baadaye wanasameheana na Maisha yanaendelea

Vipi Mdau, nawe unaye Rafiki ambaye hata mkigombana bado Urafiki wenu huwa unaendelea?

Shiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/UrafikiUsiokwisha

#JamiiForums #JFChitChats #JFStories #JamiiAfrica #LongtimeFriendship
❀1πŸ‘1
Maisha yanaendeshwa na Imani na Matumaini, hata kama hauna hakika ya kesho. Ishi bila woga huku ukiamini kesho itakuja na utakuwa tayari kuikabili.

Tunakutakia Mapumziko mema ya mwisho wa Wiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #GoodMorning #AmkaNaJF #Maisha
πŸ™1
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, mjadala kuhusu Marekebisho ya Mfumo wa Uchaguzi (Reforms) haukwepeki. Kuna wanaosema reforms tayari zimefanyika, huku wengine vikisema bado kuna kasoro na wengine wakisema hawatashiriki Uchaguzi hadi kasoro hizo zishughulikiwe

Maswali muhimu ni je, β€˜Reforms’ zilizofanyika zinatosha? Kwanini sauti ya pamoja ya Vyama haijasikika? Vyama vingine vinaona umuhimu wa β€˜reforms’? Je, Wananchi wanafahamu mabadiliko yaliyofanywa na kuyaridhia?

Kufahamu haya na mengine, jiunge nasi katika Mjadala, kupitia Xspaces ya JamiiForums, Mei 12, 2025 kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku

Kujiunga bofya https://jamii.app/ReformsSpace

#ElectionReforms #Kuelekea2025 #ReformsSpace #Accountability #Democracy #FreeAndFairElections
πŸ‘3
Tanzania inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu 2025, lakini je, tuko tayari?

Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi yamejadiliwa, huku baadhi yakitajwa yamefanyika, lakini yamegusa kiini cha matatizo yanayolalamikiwa?

Kufahamu haya na mengine usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa β€œβ€˜Reforms’ za Uchaguzi; Je, Tume, Vyama na Wananchi wanaongea Lugha moja?” kupitia #XSpaces ya JamiiForums, Mei 12, 2025, Saa 12:00 jioni – 2:00 usiku

Kujiunga bofya https://jamii.app/ReformsSpace

#ElectionReforms #ReformsSpace #Kuelekea2025 #Uwajibikaji #Demokrasia #FreeAndFairElections
πŸ‘1
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Afya ya Uzazi na Jinsia (UNFPA) limetangaza kuwa Serikali ya Marekani imeamua kukata ufadhili wake wa baadaye kwa shirika hilo, hatua inayotajwa kusitisha msaada muhimu kwa Mamilioni ya Watu walio katika Mazingira ya Migogoro na kwa Wakunga wanaookoa Maisha ya akina Mama wakati wa kujifungua

Imeelezwa Marekani imefikia hatua hiyo ikidai UNFPA inahusishwa na utoaji wa Mimba wa kulazimishwa na upasuaji wa Uzazi wa hiari Nchini China, madai ambayo yamekanushwa mara kadhaa na tathmini huru, ikiwemo zile zilizofanywa na Serikali ya Marekani yenyewe

Uamuzi huu unakuja huku zaidi ya ruzuku 40 za kibinadamu zikiwa tayari zimesitishwa, zenye thamani ya takriban Dola Milioni 335. #UNFPA ilikuwa ikitegemea wastani wa Dola Milioni 180 kutoka Marekani kwa Mwaka

Soma https://jamii.app/USCutsUNFPA

#UNFPA #AfyaYaUzazi #HakiZaWanawake #JamiiAfrica #JamiiForums #HumanitarianAids
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, amesema Chama hicho kimetenga Tsh. Milioni 10, kwa yeyote atakayesaidia kutoa taarifa za mahali alipo Mdude Nyagali ambaye hajulikani alipo, tangu alipochukuliwa na Watu waliodaiwa kuwa Polisi usiku wa kuamkia Mei 02, 2025

Soma https://jamii.app/Mil10CDMMdude

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Democracy
πŸ‘1πŸ‘Ž1
DAR: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imemkamata Diwani wa Kata ya Buguruni, Busoro Pazi (CCM), kwa tuhuma za #Rushwa na wizi wa Mali za Umma

Tuhuma za wizi zinahusu vifaa vya majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, yaliyobomolewa na vifaa vyake kutoweka, ikidaiwa kuwa yeye na wafuasi wake walihusika

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, TAKUKURU ilimkamata Pazi Aprili 9, 2025 na baadaye akaachiwa kwa dhamana. Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Sosthenes Kibwengo, alithibitisha kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana Diwani Pazi, lakini akasisitiza kuwa suala hilo liko katika uchunguzi

Soma https://jamii.app/DiwaniBuguruniRushwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #KemeaRushwa #UchaguziMkuu2025