JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHINYANGA: Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama kimesema, Watia nia 9 wa nafasi za Ubunge na Udiwani Wilayani humo, wamebainika kujihusisha na vitendo vya kugawa Fedha kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM nyakati za usiku, kinyume na Maadili ya Chama

Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, amesema Wagombea hao wanatoka kwenye Majimbo yote matatu ya Wilaya hiyo: Kahama Mjini (5), Ushetu (2) na Msalala (2)

Ameeleza “Tumebaini baadhi ya watia nia wanazunguka usiku kwenye Kata mbalimbali kuwapa Wajumbe Fedha, wengine hadi Tsh. 10,000 ili wawapitishe kwenye mchakato wa ndani. Hii ni aibu, ni udhalilishaji na ni kinyume cha Maadili ya CCM. Chama hakiwezi kumvumilia Mgombea wa aina hiyo."

Soma https://jamii.app/RushwaWatianiaUdiwani

#UchaguziMkuu2025 #KemeaRushwa #JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Siasa
Mkurugenzi wa ldara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary (66) amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025

Inaelezwa kuwa Hillary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Amefanya kazi Redio Tanzania mwaka 1981 hadi 1994 alipojiunga na Radio One Stereo. Mwaka 2003 alijiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na BBC akiwa Idhaa ya Kiswahili. Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media. Desemba 30, 2021 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano – Ikulu Zanzibar

Zaidi, Soma https://jamii.app/CharlesHilaryAfariki

#RIPCharlesHilary #JamiiAfrica #JamiiForums
👍1😭1
Katika kusherekea Siku hii ya Mama Duniani, tunawatakia kina mama wote heri, afya njema na upendo usio na kifani

Asanteni kwa upendo, nguvu na kujitolea kwenu kila siku, ninyi ni nguzo ya familia na jamii

#JamiiAfrica #JamiiForums #MothersDay #Mother
👏3👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Tulia Ackson akifafanua hoja ya Bunge kutojadili kuhusu uwepo wa matukio ya Watu kudaiwa kutekwa na wengine kupotea Nchini, amesema suala hilo linahitaji ushahidi na isiwe suala la kusikia

Amezungumza hayo wakati akihojiwa na Wasafi FM, Mei 9, 2025, ambapo Mtangazaji Charles Williams alimuuliza “Kumekuwa na vitendo vinavyoitwa vya Utekaji, hata Ripoti ya LHRC imeeleza hilo, hapa Mbeya amepotea Mdude (Nyangali), CHADEMA na Serikali wametangaza dau kwa atakayefanikisha kupatikana kwake.”

Akaongeza “Je, vitendo vya Watu kupotea au kutekwa vinaonekana vimeshamiri au vimerejea kwa kasi, Watu wanadhani Bunge lina sababu ya kusimamisha shughuli zake na kulijadili kwa kina suala hilo, wewe unasemaje?"

Soma https://jamii.app/TuliaNaWasafi

#JamiiForums #Governance
🤬2👍1😭1
Marekebisho ya Mfumo wa Uchaguzi (Reforms) ni msingi wa Uchaguzi Huru na wa Haki, lakini Je, maboresho “yanayotajwa” kufanyika tayari yanatosha? Wananchi na Wapigakura wanayafahamu na kuyaunga mkono? Msimamo wa Vyama vya Siasa ni upi? Vimeridhika?

Usikose Mjadala wa “Reforms’ za Uchaguzi; Je, Tume, Vyama na Wananchi wanaongea lugha moja?” kupitia Xspaces ya JamiiForums, Mei 12, 2025 kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, tuchambue hali halisi ya ‘reforms’, changamoto na njia ya kuelekea Uchaguzi Mkuu Huru, wa Haki na wenye uwazi

Kujiunga bofya https://jamii.app/ReformsSpace

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
👍2👏1
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema kuna baadhi ya Watu na Viongozi wa #CHADEMA wanatoa matamko ikiwemo ya kutaja majina ya Askari wakiwatuhumu kuhusika na tukio la kupotea kwa Mwanachama wa Chama hicho, Mpaluka Said Nyagali (Mdude) bila kuwasilisha ushahidi wowote

Taarifa ya Polisi inaeleza “Jeshi linatoa onyo kali kwa Mtu au kikundi chochote cha Watu wenye nia ovu kujaribu wala kuthubutu kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwemo kudhuru Askari ama familia za Askari, pia wajionye sana na wasifikiri kufanya kitendo hicho ni rahisi kwao.”

Imeendelea “Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua za Kisheria na kumshughulikia Mtu au kikundi chochote cha Watu watakaojaribu kufanya uhalifu kutokana na matamko au kauli hizo zinazotolewa.”

Soma https://jamii.app/PolisiTamkoMbeya

#JFMatukio #JamiiForums #Governance
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Ndugu wa marehemu, Kurwa Igembe wamekataa kuuchukua mwili katika Hospitali ya Misheni Chimala wakitaka uchunguzi ufanyike kuhusu kifo cha Kurwa ambaye inadaiwa alipigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mei 7, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanal Maurid Surumbu ameiambia Azam TV kuwa Askari Wanne wa TANAPA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma hizo ikidaiwa kulitokea majibizano kati ya Askari hao waliowatuhumu Wafugaji kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Wilayani Mbarali

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Nursheed Mridi amekiri mwili huo kuwa na jeraha la risasi lakini bado uchunguzi haujafanyika

Soma https://jamii.app/AskariWaTANAPA

#JamiiForums #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amemtangaza Rashid Mijuza kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa huku aliyekuwa Meneja wa Uwanja huo, Malinde Mahona amepelekwa Makao Makuu ya Wizara hiyo kuwa Msimamizi wa viwanja vyote nchini

Kabudi amesema hayo Mei 10, 2025 alipokagua Uwanja huo na Viwanja vya Mazoezi ya CHAN 2024 ambapo pia amesema nyasi za uwanja huo zipo tayati kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba dhidi ya RS Berkane ya Morocco

Ikumbukwe, Aprili 7, 2025, baadhi ya waliojitambulisha kuwa ni Wazee wa Klabu ya Simba walimlalamikia Mahona kuwa amewazuia kuingia uwanjani wakati timu yao ikijiandaa kucheza dhidi ya Al Masry ya Misri, hivyo wakashinikiza Meneja huyo awapishe hali ambayo ilizua sintofahamu kwa muda

Soma https://jamii.app/MkapaStadiumUpdates

#JFSports #JamiiForums #JamiiAfrics
2
Ukimuuliza Mtanzania kuhusu Nchi za #Nordic, yaani Sweden, Norway, Denmark, Finland au Iceland, wengi watasema: “Aaah zile nchi za maisha bora! Kule hakuna rushwa! Elimu ni bure na watu wao wana furaha kweli kweli”

Lakini, ni hayo tu unayoyajua?

Je, unajua uhusiano wao na Afrika ukoje? Wanavyotumia teknolojia kusaidia jamii? Tamaduni zao za kipekee? Au ushirikiano wao wa kimataifa unaoleta maendeleo ya kijamii?

Ni muda wa kuonesha maarifa yako. Bofya link na uone ni kwa kiasi gani unaelewa kuhusu Nchi za Nordic:

https://jamii.app/NordicDodoso

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
👍1
DAR: Magoli yaliyofungwa na Steven Mukwala yameiwezesha Timu ya #Simba kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya #KMCFC ambayo imepata goli kupitia kwa Rashid Chambo katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa KMC

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 69 ikiwa nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi nyuma ya Yanga yenye pointi 70, timu zote hizo mbili zikiwa zimecheza michezo 26

Upande wa KMC imesalia katika nafasi ya 11 ikiwa na alama 30 katika michezo 27

Soma https://jamii.app/KMCSimbaDar

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
👍1
HISPANIA: Timu ya #Barcelona imeifunga Real Madrid Magoli 4-3, ushindi unaoifanya ifikishe pointi 82 ikiwa na maana inahitaji alama 2 katika michezo mitatu iliyosalia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (#LaLiga), Madrid ikibaki nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 75

Licha ya kupoteza #KylianMbappé ameifungia #RealMadrid magoli yote matatu (hat trick) na kushika nafasi ya kwanza ya Wafungaji wa LaLiga akifikisha magoli 27

Matokeo hayo yanaifanya Madrid kuwa imefungwa mara nne mfululizo msimu huu, michezo iliyopita; Barcelona 3-2 Real Madrid (Copa de Rey), Real Madrid 2-5 Barcelona (Super Cup) na Real Madrid 0-4 Barcelona (LaLiga)

Soma https://jamii.app/ElClasico25

#JFSports #JamiiForums #JFLaLiga25
👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anaeleza ili kupunguza changamoto ya foleni katika maeneo mbalimbali ya Jiji, Chama cha Mapinduzi (#CCM) kiliwahi kunukuliwa kuwa kwa kuwa chenyewe kimeshika dola, mpango uliopo kwenye Ilani yao ni kujenga/kukamilisha barabara za juu (flyovers) kwenye makutano kadhaa ya barabara

Anasema baadhi ya maeneo yaliyoanishwa ni makutano ya Changombe, Kamata, Uhasibu, Morocco, Mwenge, Magomeni, Tabata, Fire, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na United Nation, Makutano ya Ally Hassan Mwinyi na Kinondoni

Mdau anakumbushia kuwa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole pia alizungumzia mipango hiyo, hivyo anahoji michakato hiyo iliishia wapi?

Soma https://jamii.app/FlyOverDar

#JamiiForums #Accountability #JFHuduma
1👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendokasi (UDART), Waziri Kindamba amekiri kuwa usafiri wa Mwendokasi umekuwa changamoto na kero kwa Watumiani wengi, ndio maana hatua zimechukuliwa ikiwemo kuongeza mabasi mapya ya Kisasa 99

Ameeleza wameelemewa na mabasi chakavu na machache hali iliyosababisha kuagiza Mabaso 100 kutoka China na tayari moja limewasili likitumia gesi asilia, linabeba abiria 155 na linatarajiwa kuanza safari Jumatatu Mei 12, 2025 njia ya Morocco -Kivukoni

Mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wamelalamikia changamoto mbalimbali za huduma ya usafiri huo, baadhi walisema mradi unazidiwa na wingi wa Wateja kuliko uwezo wa mabasi

Soma https://jamii.app/KindambaMwendokasi

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFAccountability
👍4
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
👍1
MWANZA: Mdau anasema Mwanzoni mwa Machi, 2025, kuna Mdau alihoji kuhusu Meli ya New MV Victoria kutofanya kazi na Mamlaka kutotoa muongozo wowote, baadaye Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) ikaeleza kuwa Meli ipo katika ‘service’ ya kawaida na inatarajia kurejea kazini ndani ya wiki tatu hadi Siku 30

Mdau anadai kufikia Mei 11, 2025, miezi miwili imekatika meli haijarejea na hakuna tamko lingine kuhusu kinachoendelea

Anatoa wito kwa TASHICO kujitokeza na kueleza kinachoendelea kwa kuwa ukimya wao unawaumiza wengi

Soma https://jamii.app/MvVictoriaMay

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania – Moshi (TPS), SACP Ramadhani A. Mungi amesema “Kundi la Vijana ndilo la uzalishaji, maendeleo ya Taifa hili yanatokana na Vijana kwa kuwa wao ndio wachapakazi, wana nguvu kubwa za mwili na akili, shughuli zote Kiuchumi asilimia kubwa zinaendeshwa na Vijana.”

Amesema hayo alipokuwa TPS wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Medani za Kivita kwa Wanafunzi wa mafunzo ya Awali Kambi ya Kamba Pori, Mei 6, 2025.

Soma https://jamii.app/NukuuYaMungi

#JamiiForums #JFNukuu #JFQuote #Governance
👍4
UCHAMBUZI: Mei 10, 2025, Chama cha #ACTWazalendo kilichambua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG) Mwaka 2023/24 na kutoa mapendekezo kadhaa na hatua za kuchukuliwa na Serikali

Sehemu ya mapendekezo hayo ni kuwa “Tunasisitiza kwamba Serikali ihakikishe kwamba mfumo wake wa kielektroniki unafanya kazi wakati wote na maeneo yote na kuweka utaratibu wa kutokuruhusu miamala kufanyika nje ya mifumo hiyo.”

Mengine ni “Tunasisitiza Viongozi, Wawakilishi, Vyama vya Siasa, Wadau wa Maendeleo na Wananchi kuhakikisha wanakata mirija ya ubadhirifu ili kuhakikisha kunakuwepo na ustawi wa kweli wa Watu.”

Soma https://jamii.app/CAGUchambuziACT

#JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji #CAGReport2025 #RipotiCAG2025
👍1