JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau, ni kitu gani kikiboreshwa katika mfumo wa Uchaguzi kitakufanya ujisikie huru na tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025

Kutoa maoni na mapendekezo yako, usikose kujiunga nasi katika Mjadala muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu kupitia #XSpace ya JamiiForums, Mei 12, 2025, Saa 12:00 jioni – 2:00 usiku

Bofya hapa kujiunga: https://jamii.app/ReformsSpace

Tafadhali 'share link' hii na yeyote ambaye hutamani apitwe na Mjadala huu

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
1👍1
UCHAMBUZI: Chama cha #ACTWazalendo kikichambua Ripoti ya CAG Mwaka 2023/24, kimesema Deni la Taifa limepanda kufikia Tsh. Trilioni 97.35 kutoka Tsh. Trilioni 82.25 Mwaka uliopita, hilo ni ongezeko la zaidi ya Tsh. Trilioni 15, hali hiyo inaweka hatari mustakabali wa Taifa kwa kuwa baadhi ya viashiria kama “uwiano wa kulipa deni kwa mapato” vinakaribia ukomo wa hatari uliowekwa na taasisi za kimataifa

ACT imesema kuwa ripoti ya #CAG imeonesha uwiano wa kulipa deni kwa mapato ya ndani umefikia 14.5%, ukikaribia kikomo cha tahadhari cha 18%, pia uwiano wa kulipa deni kwa mauzo ya nje ni 11.7%, ukielekea ukomo wa hatari wa 15%

ACT imeongeza "Maana yake, sehemu kubwa ya mapato ya Serikali inaishia kulipa madeni badala ya kuendeleza huduma kwa Wananchi. Mapato ya Serikali kwa Januari 2025, kwa Mfano ilikusanya Tsh. Trilioni 2.63 katika makusanyo hayo Serikali ilitumia Tsh. Trilioni 1.2 kulipia huduma ya deni"

Soma https://jamii.app/CAGUchambuziACT

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #CAGReport2025
👍2
KENYA: Rais Ruto alipokea rasmi ripoti ya Mchakato wa Upatikanaji wa Viongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Mei 6, 2025, kutoka kwa Mwenyekiti wa Jopo la Uteuzi, Dkt. Nelson Makanda baada ya kukamilika kwa mchakato wa usaili na uhakiki wa Wagombea

Hata hivyo Waangalizi wa Uchaguzi (ELOG) wamesisitiza kuwa #Uwazi wa mchakato huu ni muhimu kwa kuimarisha imani ya Umma katika Taasisi ya Uchaguzi, hasa kuelekea chaguzi zijazo

Usaili wa nafasi ya Mwenyekiti wa IEBC ulikamilika Machi 26, ambapo Wagombea 11 walihojiwa. Mei 8, Rais Ruto alimteua Erastus Edung Ethekon kuwa Mwenyekiti mpya wa IEBC, uteuzi unaosubiri kuidhinishwa na Bunge

Ethekon, ambaye aliwahi kuwa Wakili wa Kaunti ya Turkana, anatarajiwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati, aliyefariki Februari 2025

Zaidi https://jamii.app/RipotiKE

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #FreeAndFairElections #Demokrasia #Governance #Transparency
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA) imesema magari ya usafiri wa Umma yatakayokatisha au kubadili “ruti” kinyume na Leseni zao, yatachukuliwa hatua ikiwemo kufungwa kwa kifaa cha VTS kwa ajili ya kufuatilia Mwenendo wa vyombo hivyo

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara wa LATRA, DCP Johansen Kahatano ambaye ameongeza kuwa wanafanya hivyo ili kukabiliana na ukatishaji wa ruti ambao unafanywa hasa na Daladala

Mfumo wa VTS unawezesha kufuatilia mwenendo wa chombo ikiwemo suala la mwendokasi na kuonekana katika Mfumo wa LATRA

Soma https://jamii.app/KukatishaRuti

Video Credits: Torch Media

#JFHuduma #JamiiForums
👍1
DAR: Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeanzisha Majimbo mapya 8 (Nane) ya Uchaguzi huku Majimbo 12 yakibadilishwa jina, hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, leo Mei 12, 2025

Hivyo, idadi ya Majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 yatakuwa 272 kutokana na ongezeko la majimbo hayo yaliyotangazwa, ambapo 222 yakiwa Tanzania Bara, 50 yakiwa Tanzania Zanzibar

Soma https://jamii.app/TumeTangazoMei12

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍1
DODOMA: Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC), Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wanahabari, leo Mei 12, 2025 ametangaza majimbo 12 yalibadilishwa majina

Amesema mabadiliko haya ni sehemu ya maboresho ya mipaka ya kiutawala ili kuhakikisha uwiano wa idadi ya Watu kwenye majimbo ya Uchaguzi na ufanisi wa uwakilishi wa Wananchi Bungeni

Soma https://jamii.app/TumeTangazoMei12

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Karibu katika Mjadala unaosema "Reforms za Uchaguzi: Je, Tume, Vyama na Wananchi wanaongea lugha moja?" ili uweze kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi kuelekea maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025

Kushiriki Bofya: https://jamii.app/ReformsSpace

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
Akizungumza katika mjadala wa “‘Reforms’ za Uchaguzi; Je, Tume, Vyama na Wananchi wanaongea Lugha moja?” msemaji wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bara, Eugene Kabendera amesema “Tunahitaji mabadiliko ya kweli ya Mifumo ya Uchaguzi, tunaweza kusogeza mbele Uchaguzi wakati huo tunajipanga. Hatutakiwi kurudi nyuma tulipotoka kwa Watu kuumizana”

Akitolea mifano Nchi jirani kama Kenya na Malawi amesema Nchi hizo zimekuwa na Uchaguzi wa Haki kutokana na Chama kilichopo Madarakani kutolewa na kukubali matokeo

Amesisitiza kuwa iwapo tutahitaji Heshima ya Vizazi vijavyo siyo lazima kuingia katika machafuko na mapigano

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
1👍1
Akichangia mada katika mjadala wa "Reforms’ za Uchaguzi; Je, Tume, Vyama na Wananchi wanaongea lugha moja?” Yukapi (Mdau) amesema “Mchakato wa Uchaguzi, kwa sasa hivi Tume na Wananchi hatuzungumzi Lugha moja, huo ndio ukweli na Kuna Watu wanahisi wakiunga Mkono mabadiliko kuna Chama fulani kinaweza kuondolewa Madarakani”

Ameongeza kuwa Vijana wengi hawapigi kura au kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi kwa madai ya kauli ya “Kwanini niende kupiga kura wakati mshindi anajulikana?" Hiyo ni hatari sana kwa Demokrasia

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
👍1
Mdau Yukapi akichangia mjadala ameshauri Makamishna na Maafisa wa juu wengine wa Tume ya Uchaguzi wasichaguliwe na Rais, kuwepo na mchakato mwingine wa kuwapata ili kuondoa Mazingira ya upendeleo

Ameongeza kuwa “Jeshi la Polisi halitakiwi kuhusishwa katika hatua kadhaa za ndani ya Uchaguzi ili kuondoa Mazingira ya kupendelea upande fulani, lakini pia Vyombo vya Habari virushe taarifa kwa usawa, vinavyofanya kwa Chama tawala zifanye pia kwa Vyama vingine”

#ReformsSpace #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Uwajibikaji #FreeAndFairElections #Kuelekea2025
👍1