JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, Susan Ngongi akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya WPFD 2025 amesema Akili Mnemba (AI) si tena dhana ya nadharia ya mijadala, ni uhalisia unaobadilisha kwa kina namna tunavyotengeneza, kusambaza na kupokea taarifa, hivyo maamuzi ya leo ndiyo yatakayoamua kama AI itakuwa chachu ya Maendeleo au chanzo cha hatari mpya na ukosefu wa Usawa

Amesema Dira ya Maendeleo ya 2050 ya Tanzania inatambua Teknolojia na Ubunifu kama nguzo za Maendeleo jumuishi na endelevu, hivyo na AI inapaswa kuwa sehemu ya msingi ya azma hiyo

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema “Uandishi usiofuata Maadili unaweza kuwa chanzo cha kuporomoka kwa Tamaduni, Mila na Desturi zetu, na hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa Vyombo vya Usimamizi wa Taaluma hii.”

Ameongeza “Kwa mantiki hiyo, pamoja na kwamba leo tunaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, lazima tutambue hakuna Uhuru usio na Mipaka, wala hakuna Uhuru bila Wajibu. Hivyo, tunaposherehekea Siku hii, tusheherekee pia uzalendo wa Nchi yetu na kuhimizana juu ya kutumia Akili Mnemba (AI) kwa umakini.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Mwesigwa Felician amesema Mtandao wa Telegram hauna shida na unafanya kazi kama kawaida

Amesema hayo baada ya kuulizwa swali na Mdau katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, kuhusu changamoto ya Mtandao huo akidai haufanyi kazi hadi anayetumia alazimike kutumia VPN

Kuhusu malalamiko kwa Wadau kuhusu Kamati ya Maudhui kutotenda Haki kwa Wanahabari haswa Mtandaoni, amesema Kamati hiyo ipo Kisheria kwa lengo la kusimamia Maudhui na inaongozwa na Kanuni ambazo zipo kwenye miongozo ya Mamlaka katika kusimamia Sekta ya Habari

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Balozi wa Uswisi-Tanzania, Nicole Providoli amesema Mijadala iliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025 imeonesha faida na changamoto zinazoweza kusababishwa na Akili Manemba (AI), pia imegusia suala la uhakiki wa Taarifa ambalo nalo ni la muhimu

Ameeleza kuwa AI inaweza kuwa msaada mkubwa katika stori za uchunguzi na kumsaidia Mwanahabari kupata taarifa nyingi lakini tukumbuke kuwa #AI inafanya kazi kutokana na taarifa zilizopo na sio ambazo zipo nje ya Mtandao

Tutambue kuwa AI sio adui wala Mwokoaji, bali inaakisi kile kilichopo kwenye Ulimwengu wa Mtandao, ndio maana Uswisi inashirikiana na Wadau mbalimbali Tanzania wakiwemo; Serikali ya Tanzania, UTPC, SJMC na JamiiAfrica

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Kuna changamoto ya baadhi ya Taasisi za Serikali kushindwa kuwa ‘Active’ katika kujibu kwa wakati kuhusu taarifa mbalimbali zinazokuwa zinasambaa Mtandaoni

Hayo yamesemwa na Nuzulack Dausen kutoka Nukta Africa ambaye ameongeza kuwa “Wanapofanya hivyo kuna Watu wanaweza kuwa wanaumizwa na Taarifa au Matukio yanayosambazwa kama hayana ukweli au hajayafafanuliwa.”

Amesema “Nadhani hiyo ni changamoto ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi kwa maana ya kwamba wahusika wawe wanajibu au wanatoa ushirikiano haraka wakati wa mchakato wa kuhakiki taarifa.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo anasema “Katika kufanikisha elimu ya kukabiliana na taarifa potofu, tumewajengea uwezo Wadau wa Habari kukabiliana na changamoto ya taarifa potofu, tumekuwa tukifanya hivyo kwa Wadau mbalimbali.”

Ameongeza "Tuliamua kufanya uwezeshaji kwa Wadau wa Habari kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa zaidi ya Wanahabari 1,000.”

Ameongeza “JamiiAfrica iliingia makubaliano na redio mbalimbali za Kijamii kutoka katika Mikoa tofauti kwaajili ya kuwapa elimu ya masuala ya uhakiki wa Habari na ni mchakato ambao bado unaendelea.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Akizungumzia suala la uhakiki wa Taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema kupitia JamiiCheck.com wanashirikiana na Wanachi kuwaonesha kile kinachofanyika kwa kuwa ni sehemu ya Elimu ya kuelewa mchakato wa uhakiki wa Taarifa potofu

Ameongeza “Tunafanya kwa kushirikiana na Jamii kwa kuwaeleza na pia hata kwa Wanahabari na Wananchi wengine wana nafasi ya kushiriki ndani ya JamiiCheck kuhakiki taarifa kwa kuwa ni Jukwaa ambalo linawashirikisha Watumiaji.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2025, amesema Uwepo wa Sheria sio Mwarobaini wa taarifa za uzushi, kwani tukifanya hivyo Watu wengi watakamatwa na watawajibishwa

Ameongeza “Jambo muhimu ni kutoa Elimu kwanza kwa Jamii, kuna mambo mengi yanafanyika kutokana na Watu kutokuwa na Taarifa sahihi. Hivyo, Serikali na Wadau kwa pamoja wanatakiwa kushirikisha Wananchi

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Alphonce Shiundu, Mhariri Africa Check ya Kenya anasema wakati wa Uchaguzi mara nyingi Vyama na Wadau wa Siasa hutumia Fedha nyingi kusambaza uzushi, wanaweza kutumia njia mbalimbali ili kukamilisha jambo lao la kusambaza taarifa za propaganda

Ameongeza kuwa wakati mnapokuwa mnatengeneza Maudhui ni vizuri kuwa na mpango mkakati wa kudhibiti Taarifa hizo kwa kuwa taarifa nyingi za uzushi huwa zinavutia

Shiundu anasema ni vizuri kufikiria kuhusu njia sahihi na nzuri za kukabiliana na Taarifa potofu hasa wakati wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mwanahabari ambaye unajihusisha na uhakiki wa Habari hautakiwi kuegemea katika kitu kimoja au njia ile ile wakati unapofanya uhakiki wa Taarifa, unatakiwa kujiongezea Uwezo ili uweze kwenda mbele zaidi ya Akili Mnemba (AI)

Reagan Kiyimba kutoka Media Initiative (Uganda) amesema hayo na kuongeza kuwa Waandishi wa Habari wanapaswa kuboresha ujuzi wao ili wawe hatua moja mbele ya yanayopangwa wakati wa Uchaguzi, ikiwemo matumizi mabaya ya AI na Teknolojia nyingine mpya zinazoibuka

Amesema “Kabla ya kufuatilia Taarifa uwe unajua mambo ya muhimu kwa kuwa vitu vinabadilika. Pia, unaweza kushirikiana na Taasisi mbalimbali ndani na nje ya Nchi yako ili kupata Elimu zaidi, Mwanahabari wa Kuhakiki Taarifa ujuzi wako unatakiwa uwe unaboreshwa kila mara.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa anasema “Fact Checking ni msingi mzuri sana kwa Mwanahabari. Kuna namna mbili za kuifanyia kazi, kwanza ni mbinu za kiuandishi wa Habari na pili njia za Kidigitali ili kupata ukweli.”

Amesema “Tunalazimika kutoa mafunzo ya uhakiki kwa Wanahabari kutokana na kwamba Mitaala haina mafunzo ya nyenzo za Kidijitali za kufanya uhakiki.”

Anaongeza “Tulichelewa hapo kati kuingiza suala la Uhakiki wa Habari katika masomo yetu ya Habari, lakini kuongezeka kwa Habari potoshi hasa za Kijamii ndio kumezidi kuleta uhitaji kwenye tasnia ya Habari.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Kuna wakati Utani unaweza kwenda tofauti na vile ambavyo Watu walitarajia, kuna vitu vinaweza kufanyiwa utani na Watu wakaamini kuwa kilichoandikwa au kuchapishwa ni cha kweli

Hayo yamesemwa na Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa ambaye amesema “Kuna maelekezo kuwa unapotengeneza Maudhui unatakiwa kuweka angalizo la kuwa unachokifanya ni Utani lakini sidhani kama Watu wote wanazingatia hilo, matokeo yake kile kinachochapishwa kinasambaa na kuaminika.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema “JamiiAfrica ipo tayari kuwapokea Watu kutoka Vyuoni kuwajengea Uwezo wa masuala ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wanahabari, tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ni wakati muhimu ambao tunaweza kutoa Elimu hiyo.”

Ameongeza “Tuna Mkataba wa ushirikiano na Vyuo kadhaa ikiwemo UDSM, SAUT na UDOM. Tunapoelekea hatuwezi kufanya kila kitu peke yetu, ndio maana tuna Mikataba na Redio za Kijamii 15 kwaajili ya kutoa Elimu hiyo, hatuwezi kufanikiwa kupitia ushirikiano wa UTPC peke yake"

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
👍1
ARUSHA: Akizungumzia kuhusu kuwawezesha Wanawake kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 katika masuala ya Uhakiki wa Taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo amesema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wadau wa Habari Wanawake na programu hizo zimekuwa zikiendelea

Amesema “Tulikuwa na Mradi maalumu pamoja na WiLDAF kuhusu kuwajengea uwezo Wanawake, pia kama kuna mapendekezo mengine yoyote kutoka kwa Wadau tupo tayari kuyapokea na ikiwezekana kushirikiana nao.”

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
BUNGENI: Mbunge wa Viti Maalum, Christina Mnzava amehoji mpango wa Serikali wa kuja na sera ya kuwapatia posho Wazee wote wa Tanzania Bara, kama ilivyo Visiwani Zanzibar

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema wamelipokea na wataendelea kulifanyia kazi kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara husika ili kuona hali ya Kiuchumi kama itaruhusu basi litatekelezwa

Zaidi https://jamii.app/PoshoWazee

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #ServiceDelivery #Governance
ARUSHA: Akisoma maazimio ya Wadau wa Habari katika kuadhimisha Miaka 32 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema Wadau wa Sekta ya Habari Nchini wanaungana kuendeleza na kulinda misingi ya Uhuru, Uwazi na Kujisimamia kwa Vyombo vya Habari

Amesema Kaulimbiu ya Mwaka 2025 ya “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari,” inaakisi mabadiliko makubwa ya Kidigitali yanayoendelea kuibadilisha Tasnia ya Habari Duniani kote

Ameeleza kuwa Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inabadilisha kwa kasi namna taarifa zinavyokusanywa, kuchakatwa na kusambazwa.

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Maazimio ya Wadau wa Habari katika kuadhimisha Miaka 32 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025 yanaeleza kuwa Teknolojia inaleta fursa kubwa katika kuongeza ufanisi wa Uandishi wa Habari, Upatikanaji wa taarifa na kutatua changamoto ya utofauti katika Lugha

Akisoma maazimio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo ameeleza Teknolojia inaibua changamoto mpya kama vile upendeleo wa kimfumo, (Algorithmic bias), taarifa potofu, Migogoro ya Maadili na hatari kwa Uadilifu wa habari

Kwa muktadha huo, kuna haja ya kuweka uwiano sahihi kati ya ubunifu wa Kiteknolojia na Uwajibikaji ili kuhakikisha Uhuru wa Vyombo vya Habari unadumishwa katika zama hizi za Kidijitali.

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
ARUSHA: Nuzulack Dausen, Mkurugenzi wa Nukta Africa anasema kuna Watu wanaanzisha taarifa potoshi wakiwa na lengo la kujiingizia kipato kutokana na kuamini wanapofanya hivyo wakitumia njia za kuvutia inaweza kuwavutia Watu kubonyeza au kufuatilia taarifa zao

Ameeleza kuwa wengine wanafanya taarifa hizo makusudi kwasababu zao za Kisiasa. Wanaweza kufanya hivyo kwa lengo la kuhamisha fikra za Watu ili waache kujadili kitu fulani na wajadili suala analotaka yeye

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayTwo

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #FactChecking
Filamu ya Makala ya #BloodParliament inaonesha ushahidi wa video na picha zaidi ya 5,000, ikiwemo Matukio ya Polisi wakifyatua risasi kwa #Waandamanaji karibu na majengo ya Bunge Juni 25, 2024. Pia, inawataja Maafisa wa Usalama wanaodaiwa kutoa amri za kuua, pamoja na wale waliotekeleza mauaji hayo

Katika Maandamano hayo ya #RejectFinanceBill2024 ya Juni na Julai 2024, zaidi ya Watu 60 waliuawa huku Polisi wakitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya Waandamanaji, wengi wao wakiwa #GenZ

Wananchi wametoa wito kwa Mamlaka kuwawajibisha Maafisa wote waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha Haki inatendeka kwa waathiriwa na Familia zao

Zaidi https://jamii.app/BloodParliament

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #SocialJustice