JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Amani ni zawadi ya thamani isiyolipika. Hakuna mafanikio, uhusiano au nafasi yoyote inayostahili kuipoteza

Chagua yale yanayokuinua, yanayokutuliza na yanayokusaidia kuwa toleo bora la 'wewe'

#JamiiForums #JamiiAfrica #Goodmorning #AmkaNaJF #Maisha
πŸ‘2
Mdau wa JamiiForums.com ameshauri Watu kutofanya siri kwenye mambo yanayohusu Familia. Amesema fikiria umejenga, huna uliyemshirikisha; una pesa Benki, Biashara, hata Mtoto nje ya Ndoa ila hakuna Ndugu anayemjua. Likitokea la kutokea ghafla, kila kitu kinapoteza maana

Amesema tujifunze kushirikishana, tuache siri zisizo na tija

Mdau, ni jambo gani huwezi kumshirikisha Mtu au Watu wako wa karibu?

Mjadala https://jamii.app/TupunguzeSiri

#JamiiAfrica #JamiForums #Maisha
πŸ‘1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Desemba 2024, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, alitoa Miezi Mitatu kwa Mkandarasi wa Barabara ya Msongola - Mbande, kukamilisha Barabara hiyo kabla Mvua za masika kuanza, lakini hadi sasa ujenzi haujaisha na hali inazidi kuwa mbaya

Ametoa Wito kwa Wizara ya Ujenzi kufuatilia changamoto hiyo kwani Wananchi wengi wanategemea njia hiyo lakini kwa sasa wanaweza kutumia hadi Saa 3 kwenye kipande hicho

Zaidi https://jamii.app/BarabaraKisewe

#JamiForums #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #JFMdau2025 #Accountability #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#HUDUMAZAKIJAMII: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko jana, Aprili 29, 2025 akihitimisha kujibu hoja za Wabunge waliochangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, amesema hakuna jambo linakera Wananchi kama kukatikiwa na Umeme

Amesema "Hakuna jambo linakera Wananchi kama kukatika Umeme hasa kama hawajapewa taarifa na ndio maana tumeamua Kituo chetu cha Huduma kwa wateja tukiimarishe, Umeme unapokatika Watu wapewe taarifa. Tumeamua kila Wilaya na kila Mkoa kuwe na 'magroup' ya WhatsApp, Meneja awe 'admin' kwenye yale magroup kwaajili ya kuwapa taarifa Watu".

Vipi Mdau, upo kwenye 'group' la TANESCO la Wilaya au Mkoa unaoishi? Mara yako ya mwisho kupata taarifa ya kukatika kwa Umeme ni lini?

Mjadala https://jamii.app/KukatikiwaUmeme

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Mshiriki wa Stories of Change 2024 anapendekeza kufanyika kwa Kilimo cha Nyasi ambacho kitaongeza Uzalishaji wa Nyasi na kupunguza Migogoro inayojitokeza kati ya Wakulima na Wafugaji na kwenye Maeneo ya Hifadhi na Misitu

Kusoma zaidi Andiko lake tembelea https://jamii.app/KilimoNyasiSOC04

#JamiiForums #JamiiAfrica #SOC2024
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu Mkuu wake, John Mnyika kimetoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura kuwajibika kutokana na tukio la Wanachama na Viongozi wa Chama hicho kudaiwa kukamatwa, kupigwa na kuumizwa na Polisi

Mnyika amesema "Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), kama haya matendo hayana baraka zake ajitokeze yeye mwenyewe atoe taarifa kwa Umma, juu ya matukio ya kupigwa, kuteswa na kuumizwa kwa Wanachama na Viongozi wa CHADEMA, akitaja idadi halisi, akitaja sababu ya hali hizo na kuwajibika kutokana na hayo"

Zaidi https://jamii.app/MnyikaPressApr30

#JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights #Governance #Democracy
❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mnyika amewaonesha Waandishi wa Habari, video ya mtu aliyemtaja kwa jina la Noel akiwa amelala chini baada ya kudaiwa kupigwa rungu la kichwa, kung'atwa na mbwa na kuvunjwa Mguu na Polisi katika eneo la Mahakama ya Kisutu, Aprili 24

Zaidi https://jamii.app/UshahidiCHADEMA

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imekumbusha Taasisi zote za Umma na binafsi Nchini zinazohusika na kuchakata taarifa binafsi za Watu, kuhakikisha zinajisajili kwenye Mfumo wa Usajili wa #RCMIS kabla ya tarehe ya mwisho, 30 Aprili 2025

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 (Sura ya 44), Taasisi yoyote inayokusanya au kuchakata taarifa binafsi, ikiwemo Mashirika ya Umma, Kampuni, Sekta ya 'hospitality', NGOs, Vyombo vya Habari, Shule, Vyuo, pamoja na watoa Huduma za Afya, inatakiwa kuwa imesajiliwa rasmi na PDPC ili kuzingatia matakwa ya Sheria

Imeelezwa, kushindwa kujisajili ni ukiukwaji wa Sheria ambapo mhusika anaweza kutozwa faini ya kati ya Tsh. 100,000 hadi Tsh. 5,000,000 au kifungo cha hadi Miaka Mitano, au vyote kwa pamoja

Soma https://jamii.app/SikuYaMwishoYaUsajili

#JamiiForums #DigitalRights #Governance #HakiYaFaragha #UlinziWaTaarifaBinafsi
πŸ‘1
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Tawi lake la Bonyokwa kimemvua rasmi uanachama John Mrema aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama na kukaidi misingi na maadili ya Chama

Kwa mujibu wa barua rasmi ya Aprili 30, 2025 iliyosainiwa na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki ni kuwa Kamati Tendaji ya Tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kufikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa Tuhuma dhidi ya Mrema ni pamoja na kusambaza barua ya Wito ya Kamati ya Nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia rasmi. Hata hivyo, Mrema amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo

Zaidi https://jamii.app/JonMremaCDM

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Accountability
#MAISHA: Unampa Ushauri gani Mdau huyu wa JamiiForums.com ili aweze kuyashinda Mawazo ya kuona anaelekea kufeli Maisha

Mjadala zaidi https://jamii.app/KutoboaMshaharaSerikali

#JamiiForums #LifeLessons #JFStories #JFChitChats #JamiiAfrica
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Baada ya kusambaa kwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima na Watu wasiojulikana, usiku wa jana Aprili 30, 2025, Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Rauli Mahabi β€œHaraja”, Mkazi wa Kurasini kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio limetokea Saa Nne Usiku maeneo ya TEC - Kurasini, Temeke na kwamba alishambuliwa kichwani na kitu butu akiwa maliwatoni pembeni ya kantini

Muliro amesema Padre Kitima anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan

Soma https://jamii.app/KitimaUpdates

#JFMatukio #JamiiForums #Governance #HumanRights