KENYA: Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari katika mzunguko wa Hifadhi ya City kwenye Barabara ya Ngong Jijini Nairobi kutoka kwa Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki ambao bado hawajatambulika
Mbunge huyo wa Kasipul ambaye chama chake kinaongozwa na Raila Odinga amepigwa risasi Saa 1:30 Usiku, jana Aprili 30, 2025 ambapo mashuhuda wamesema mtu aliyempiga risasi alisogea karibu kabisa katika dirisha la gari na kufyatua risasi kisha kutokomea kusikojulikana
Alikimbizwa Hospitali lakini baadaye ikatangazwa amefariki, Jeshi la Polisi la Kenya bado halijatoa tamko kuhusu tukio hilo
Soma https://jamii.app/RIPCharlesWere
#JamiiForums #KenyanPolitics #HumanRights

๐1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumzia uamuzi wa baadhi ya kesi kufanyika kwa njia ya Mtandao, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametolea mfano Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) walitoa tamko linaloashiria uvunjifu wa Amani na Usalama, hali iliyosababisha baadhi ya Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao kwa njia ya Mtandao
Amesema "Watanzania waelewe kuwa Jeshi linapokuwa na taarifa za Kiusalama linashirikiana na Mahakama kutoa Haki ile ile lakini kwa kutumia Teknologia ya Mahakama Mtandao ili kuzuia fujo Mtaani, naomba Watanzania watuelewe.โ
Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29
#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights

โค1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameliagiza Jeshi la Magereza kusimamia Sheria na taratibu kwa wanaotaka kuwaona Wafungwa na Mahabusu, akieleza taratibu hizo lazima ziheshimiwe bila upendeleo na hakuna wanaotakiwa kupewa Huduma Maalum (V.I.P)
Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29
#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29
#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
JamiiAfrica inawatakia Wafanyakazi wote Maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Tukumbuke, nyuma ya kila Huduma bora, Bidhaa nzuri na Maendeleo ya Taifa kuna jasho, Maarifa na Bidii ya Mfanyakazi
Tuendelee kusimamia Haki, Mazingira salama ya Kazi na Maslahi bora kwa Wafanyakazi wote. Bila Mfanyakazi, hakuna Mafanikio
#JamiiAfrica #JamiiForums #MeiMosi2025 #WorkersDay

โค2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania litaendelea kuwawezesha Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao wakiwa Magerezani kupitia Mahakama Mtandao, hasa kunapokuwepo na viashiria vya matishio ya kiusalama
Ameyasema hayo Aprili 30, 2025 alipoambatana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kukagua Makasha ya kisasa ya Mahakama Mtandao yanayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya Kiteknolojia katika Gereza la Isanga -Dodoma
Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29
#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
Ameyasema hayo Aprili 30, 2025 alipoambatana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kukagua Makasha ya kisasa ya Mahakama Mtandao yanayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya Kiteknolojia katika Gereza la Isanga -Dodoma
Soma https://jamii.app/BashungwaAprili29
#JamiiForums #Accountability #Governance #HumanRights #CivilRights
๐1
DAR: Akizungumzia tukio la Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima kujeruhiwa, Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa amesema eneo alikoshambuliwa hulitumia kufanyia kazi zake baada ya shughuli za pamoja na hakuwa anapata kinywaji, wala si sehemu kunakopatikana kinywaji chochote
Askofu Pisa amesema Padri Kitima alikuwa na Mapadri wenzake katika kikao, walipomaliza wenziwe waliondoka, akabaki eneo la mgahawa anakofanyia shughuli zake siku zote na kuwa hakuna baa wala vinywaji na kama kuna anayehitaji kupata vinywaji kwa kawaida angeenda nje ya eneo hilo
Ameongeza โMaana ukisema Mtu alikuwa anakunywa kwa saa zote hizo maana yake alikuwa anakunywa pombe, si hivyo. Wakati anatoka kurejea ndani kuna uchochoro wenye giza, hapo ndipo akavamiwa na kujeruhiwa na kitu kizito kichwani na kidevuniโ
Soma https://jamii.app/TECPadriKitima
#JFMatukio #JamiiForums

๐3๐ฅ1
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, tukio lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025, katika eneo la Kurasini, Dar es Salaam
Padre Kitima alivamiwa na watu Wawili wasiojulikana na kushambuliwa kichwani na mwilini na kusababishiwa majeraha mbalimbali
CCM imesema inalaani vikali kitendo hicho cha kikatili na kisicho na utu dhidi ya kiongozi wa dini, ambaye kimesema amejitolea maisha yake kuhudumia jamii kwa upendo na uadilifu
CCM imetoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kali wahusika wa tukio hilo
Soma https://jamii.app/CCMKitima
#JamiiForums #Governance #Accountability #HumanRights

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limelaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa baraza hilo lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025 katika Makao Makuu ya TEC, Kurasini, Dar es Salaam
Kwa mujibu wa taarufa ya Baraza hilo, Padre Kitima kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan
Aidha, TEC imetoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Vilevile uchunguzi wa tukio hili ufanyike kwa haraka, kwa uwazi na bila upotoshaji ili kurejesha imani ya wananchi
Soma https://jamii.app/TamkoTECMei1
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice

Hatua ndogo ni hatua bado. Usijione mdogo kwa sababu hujafika kule unapotamani kufika
Acha kujilaumu kwa kile ambacho hujafanya jana, leo ni nafasi nyingine ya kujaribu tena, kujifunza tena na kusonga mbele
#Goodmorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF
Acha kujilaumu kwa kile ambacho hujafanya jana, leo ni nafasi nyingine ya kujaribu tena, kujifunza tena na kusonga mbele
#Goodmorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kada wa CHADEMA, Mdude Nyagali anadaiwa kukamatwa usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2025 akiwa katika makazi yake Mbeya na Watu wanaodaiwa kujitambulisha kuwa ni Polisi
Taarifa iliyochapishwa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi imeeleza kuwa inadaiwa Watu hao walibomoa mlango wa nyumbani kwa Mdude na kisha kuingia ndani wakiwa na silaha za moto, ambapo walimpiga na kuondoka naye
JamiiForums inaendelea na jitihada za kutafuta taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhusu taarifa hizo zilizotolewa na Mwabukusi
Zaidi soma https://jamii.app/MdudePolisi
#HakiZaBinadamu #Demokrasia #HumanRights #SocialJustice

DAR: Mwanasiasa James Mbatia amezungumzia tukio la kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Charles Kitima akidai waliofanya tukio hilo wanaonekana ni Watu wenye mafunzo ya juu na kwamba walilenga kumdhulumu uhai wa Kiongozi huyo wa Dini
Ikumbukwe tukio hilo lilitokea Aprili 30, 2025, baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, Jumanne Muliro akasema wanamshikilia Rauli Mahabi โHarajaโ na uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo
Soma https://jamii.app/MbatiaOnKitima
#JamiiForums #HumanRights #JFMatukio

๐2
Mdau kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala kuhusu maslahi ya Watumishi wa Sekta Binafsi, baada ya Serikali kuongeza Mishahara kwa asilimia 35.1 kwa Wafanyakazi wa Umma wanaolipwa kima cha chini, huku kukiwa bado na hali ya sintofahamu kwa upande wa Wafanyakazi wa Sekta Binafsi
Wafanyakazi wa Sekta binafsi wamekuwa wakilalamikia Mazingira duni ya Kazi, Mishahara midogo isiyoendana na gharama za Maisha, kutokuwepo kwa Mikataba ya Ajira iliyo wazi na ya Haki, nk
Kwa mtazamo wako, nini kinakwamisha upatikanaji wa maslahi bora kwa Wafanyakazi wa Sekta Binafsi?
Mjadala https://jamii.app/MishaharaSektaBinafsi
#JamiiForums #JamiiAfrica

DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amekosoa utaratibu uliotokea Mahakama ya Kisutu kuhusu uamuzi wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu kusikilizwa kwa njia ya Mtandao badala ya kufikishwa Mahakamani, akidai uamuzi huo ulikuwa wa Hakimu na siyo Mahakama
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi ametoa wito kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kutoa maelekezo na kama hatatimiza hilo awajibike kuhusu tukio la Raia kukamatwa, kuzungushwa kwenye Magari na baadaye baadhi yao kutupwa kwenye Msitu
Amesema hayo akikumbushia matukio kadhaa yaliyotokea Aprili 24, 2025 wakati wa mchakato wa kufuatilia shauri linalomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika Mahakama ya Kisutu
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
Amesema hayo akikumbushia matukio kadhaa yaliyotokea Aprili 24, 2025 wakati wa mchakato wa kufuatilia shauri linalomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika Mahakama ya Kisutu
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
โค2๐1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi akizungumza na Wanahabari, leo Mei 2, 2025 ametoa wito kuwa kuna umuhimu wa uwepo wa chombo kinachoweza kusimamia utendaji wa Mamlaka mbalimbali za Serikali ikimemo Jeshi la Polisi ili kuongeza Uwajibikaji
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
Soma https://jamii.app/MwabukusiMay2
#Accountability #CivilRights #JamiiForums #Kuelekea2025
๐1
KAGERA: Meneja wa Wakala wa Barabara (#TANROADS) Mkoa, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya amesema ujenzi wa Barabara njia Nne Bukoba kutoka Rwamishenye - Makutano ya Barabara ya Stendi ya Mabasi unaendelea baada ya kusuasua kwa muda, akieleza unatarajiwa kukamilika Novemba 2025
Kutokamilika kwa Barabara hiyo kumelazimisha Wananchi kutumia njia mbadala kwa kuzunguka kupitia Nyakanyasi, ambapo Mhandisi Ntuli amesema โWananchi wamekuwa na maswali, hatujalala, kazi inaendelea, tunaendelea na ukarabati wa Daraja la Kanoni.โ
Ikumbukwe Desemba 6, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alihoji kuhusu mchakato huo kwa kuandika โUjenzi wa Njia Nne Bukoba unasuasua, Mamlaka hazifahamu Barabara hiyo ndio mlango wa Uchumi wa Mji?โ
Soma https://jamii.app/BarabaraKagera
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability