JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema madai ya Waandishi wa Habari kudaiwa kupigwa na Jeshi la Polisi wanatakiwa kwenda Mahakamani ili kupata Haki. Pia, ametoa wito kuwa raia hawatakiwi kujifanya ‘Wadwanzi’ bila kuangalia hatari zinazoweza kutokea mbele, hawatakiwi kulaumu Jeshi la Polisi

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
1
MBEYA: Jeshi la Polisi Mkoani humo limekanusha taarifa zinazolituhumu Jeshi hilo kuhusika katika tukio la kuvamia Nyumba ya Kada wa CHADEMA, Mdude Nyagali, kumpiga, kumjeruhi na kisha kuondoka naye kusikojulikana na kusema kuwa wanaendelea na ufuatiliaji

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo Mpaluka Said (Mdude) azitoe ili kufanikisha kumpata pamoja na taarifa za Watu waliohusika katika tukio hili ili waweze kukamatwa

Taarifa ya Jeshi hilo imeeleza Mei 02, 2025 majira ya asubuhi, walipokea taarifa kutoka kwa Sije Mbugi Emmanuel (Mke wa Mdude) kuwa majira ya saa 08:00 usiku wakiwa wamelala, Watu wasiofahamika waliwavamia baada ya kuvunja mlango na kuingia ndani na kisha kumjeruhi Mdude sehemu mbalimbali za Mwili wake na kutoweka naye

Soma https://jamii.app/PolisiMbeyaMei2

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Timu ya #Simba imepata ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni siku chache tangu Simba ilipoingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF)

Mashujaa FC ilitangulia kufunga kupitia kwa Jaffar Kibaya dakika ya 5, Simba ikasawazisha kupitia kwa Leonel Ateba dakika ya 65 kwa njia ya penati ambaye pia aliongeza la pili dakika ya 90+15 kwa penati pia

Simba imeendelea kubaki nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi ikifikisha pointi 60 katika michezo 23, nyuma ya Yanga yenye alama 70 yenye michezo 26, huku Mashujaa FC ikiwa nafasi ya 10 kwa kuwa na alama 30 katika michezo 27

Soma https://jamii.app/SimbaMashujaaFC

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
👍31
DAR: Balozi mbalimbali Nchini ikiwemo Marekani, Sweden na Umoja wa Ulaya wamelaani tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025

Balozi hizo zimesisitiza kutafutwa kwa Haki kupitia uchunguzi wa haraka na wa wazi

Upande wa Ubalozi wa Marekani umeeleza “Tunalaani vikali vitendo vyote vya ukatili, hasa vile vinavyolenga kunyamazisha wito wa Haki, Maridhiano na Haki za Binadamu.”

Soma https://jamii.app/USEmbassyOnKitima

#JamiiForums #Democracy #Accountability #Kuelekea2025
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na Wanahabari, leo Mei 2, 2025, Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, amesema taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, ni ya awali na hivyo haitakiwi kulishwa maneno ikiwemo kusema alivamiwa na Walevi

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amewataka Wananchi kuendelea kuwa na imani na Jeshi la Polisi wakati uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima ukiendelea

Soma https://jamii.app/ChalamilaOnKitima

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
👎1
Tunakutakia Mapumziko mema ya mwisho wa Wiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend
👍2
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba wa kufanya uchunguzi juu ya tukio la Kada wa #CHADEMA, Mdude Nyagali ambaye imeelezwa alivamiwa, akapigwa na kuchukuliwa na Watu ambao utambulisho wao haujajulikana

LHRC imesema tukio hilo lililotokea katika Makazi ya Mdude, Mkoani Songwe na mengine ya namna hii yanayoendelea kuvunja Haki za Binadamu Nchini yanatakiwa kuchukuliwa natua na Mamlaka hiyo

Pia, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Fulgence Massawe, amesema wamelitaka Jeshi la Polisi Songwe kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa shambulio hilo la kikatili

Soma https://jamii.app/LHRCKuhusuMdude

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Padri Monsinyori Samwel Muchunguzi ameeleza kuwa suala la Viongozi wa Dini kutozungumzia Siasa ni gumu kwa kuwa sehemu ya Waumini wao ni Wanasiasa, hivyo wao nao ni sehemu ya Waumini wanaostahili kupata darasa wanalolitoa kwa Waumini

Amesema hayo wakati wa Maadhimisho Takatifu ya kuwatengeneza Wanafunzi wa Seminari ndogo ya Mtakatifu Maria Rubya na kuiombea Miito, Jimbo Katoliki Bukoba

Soma https://jamii.app/PadriMuchunguzi

#JamiiForums #Governance #Demokrasia #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Democracy
👎21👍1
UGANDA: Mkuu wa Majeshi Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais #YoweriMuseveni kupitia machapisho yake katika Mitandao ya Kijamii amekiri kumteka Mlinzi wa Mwanasiasa Bobi Wine (Edward Mutwe) ambaye aliripotiwa kutekwa na Watu wasiojulikana Aprili 27, 2025 na hajulikani alipo hadi sasa

Muhoozi pia amejisifu kuteka na kuwatesa Wapinzani wake huku akitishia kuua hadharani yeyote anayekosoa Serikali iliyopo Madarakani

Edward Mutwe ni Mlinzi Mkuu wa Bobi Wine ambaye ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha upinzani Nchini Uganda cha The National Unity Platform (NUP)

Soma https://jamii.app/MuhooziMay2025

#JamiiForums #UgandaPolitics #Governance #HumanRights
👍1
KENYA: Watu Wanne waliohusika kuandaa Makala ya 'Blood Parliament' iliyoonesha Mauaji yaliyotokea wakati wa Maandamano ya Gen Z kisha kurushwa katika Kituo cha BBC wamekamatwa na kushikiliwa kwa Siku moja na Jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa

Taarifa ya Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Filamu na Televisheni Kenya (KFPTA), Ezekiel ‘Ezy’ Onyango, amesema Vifaa vyao ikiwemo Kompyuta na Vifaa vya kuhifadhi nyaraka (hard drive) vilikamatwa wakati wa operesheni hiyo

Amesema “Tumejulishwa wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kuchapisha taarifa za uongo na #Cyberbullying. Watuhumiwa hao walikamatwa jana Mei 2, 2025 wameachiwa asubuhi ya leo Mei 3, 2025

Soma https://jamii.app/BloodParliamentUpdates

#JamiiForums #KenyanPolitics #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumhoji Mtu aliyeandika kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa "Siku za Kitima zinahesabika"

Mtu huyo anayetambulika kwa jina la Dr. Frey Edward Cosseny akitumia Akaunti yake ya Mtandao wa X, Aprili 28, aliandika “Mwambieni Kitima iko Siku ataingia kwenye 18 hatokaa asahau Tanzania, Muacheni ajifanye Mwanasiasa. Mfikishieni meseji Siku si nyingi atapata anachokitafuta Dawa yake iko jikoni atakuja kuozea jela.”

Aprili 30, 2025, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima akashambuliwa na kujeruhiwa na Watu wasiojulikana akiwa Makao Mkuu ya TEC, Mei 1, 2025 Jeshi la Polisi likatangaza kumshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio hilo

Soma https://jamii.app/BashungwaMaelekezo

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance #Uwajibikaji
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Peter Kibatala akizungumza na Wanahabari, leo Mei 3, 2025, amesema mteja wao ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, ambaye anashikiliwa Gerezani anatarajiwa kuanza kufanya mgomo wa kula Chakula hadi Haki ipatikane

Amesema hiyo ni sehemu ya kusisitiza Haki ipatikane bila kufafanua Haki ipi anayoizungumzia

Soma https://jamii.app/MawakiliMei3

#JamiiForums #Democracy
👍2