JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amesema analaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, na ameliagia Jeshi la Polisi kuwasaka wote waliohusika na uhalifu huo ili hatua za Kisheria zichukuliwe

Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Viongozi wa dini Nchini katika kudumisha Amani, Mshikamano wa Kijamii, na Maadili ya Taifa

Ameeleza hayo, Mei 02, 2025 wakati wa hafla ya kuwaaga Watumishi wa Umma waliostaafu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo alikumbusha kuwa Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha Usalama wa Raia na Mali zao kupitia Vyombo vyake vya Usalama

Soma https://jamii.app/BashungwaMaelekezo

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance #Uwajibikaji
πŸ‘1
MOROGORO: Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob Mameo Ole Paulo, alisema ujumbe huo alipokuwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu, Aprili 18, 2025 ambapo pia alisisitiza kwa Serikali kuzingatia malalamiko yanayotolewa na Wananchi.

https://jamii.app/AskofuJacobNukuu

#Demokrasia #JamiiForums #HumanRights #JFNukuu #Quote #JamiiAfrica
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema Waandishi wa Habari wanao wajibu wa kusaidia umma kubaini Taarifa za ukweli na uongo, na wanaweza kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuongeza tija licha ya kuwa nayo inachangia kuzalishwa kwa Taarifa za uongo

Ameyasema hayo Mei 2, 2025 katika mafunzo ya Siku moja ya Wanahabari 150, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo inaadhimishwa Mei 3, ambapo Kaulimbiu ya Mwaka 2025 ni β€œUhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba/Unde kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari.”

Aidha, ametoa kongole kwa #JamiiAfrica ambayo imekuwa ikishughulikia kubaini Taarifa sahihi na zisizo sahihi kupitia Jukwaa la #JamiiCheck

Soma https://jamii.app/WPFD2025

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking #MisDis04
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta waliotengeneza na kusambaza waraka feki uliodaiwa kutolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), ambao ulilenga kuchochea mgongano kati ya Kanisa na Serikali

Soma https://jamii.app/BashungwaMaelekezo

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance
πŸ‘Ž1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Jebra Kambole ametoa wito kwa Uongozi wa Mahakama kusimamia suala la Haki ya Wananchi kupata taarifa ya kinachoendelea Mahakamani, akitoa mfano wa Maafisa wa Usalama kuwapiga na kuwazuia Wanahabari kutimiza majukumu yao ya kuwahabarisha Wananchi

Soma https://jamii.app/MawakiliMei3

#JamiiForums #Democracy #WPFD2025 #WorldPressFreedomDay #PressFreedom
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania kuwa Nchi iko salama na kwamba waendelee kutii Sheria bila Shuruti na kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya Wahalifu wanaotaka kuvuruga Amani ya Nchi

Soma https://jamii.app/BashungwaMaelekezo

#JamiiForums #Accountability #HumanRights #Governance
πŸ‘Ž1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SHINYANGA: Serikali imesema Vitambulisho vya Kidigitali kwa Waandishi wa Habari vinatarajiwa kuanza kutolea wiki moja kutoka leo Mei 3, 2025

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ambaye ameongeza kuwa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari haitasita kuwafutia usajili Wanahabari watakaokwenda kinyume cha Kanuni na Maadili ya kazi zao

Soma https://jamii.app/KitambulishoMwandishi

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #JamiiForums #JamiiAfrica
πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Jaji Warioba amesema Viongozi wa Dini wanaweza kusaidia kufanya mazungumzo ya kutafuta muafaka wa Kisiasa nchini, ambapo watakuwa wanazungumza na kushauri nini kifanyike

Akizungumza katika Kongamano la Uchaguzi Mkuu wa Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amesema wanaamini kama Viongozi wa Kisiasa wakikubali kukutana, wakawa na Watu wa kuwashauri inawezekana kufikia muafaka tukaenda kwenye Uchaguzi vyama vyote vikishiriki, Wananchi wakashiriki na tukatoka salama

Soma https://jamii.app/JajiWariobaMei3

#JamiiForums #Governance #Demokracy #Kuelekea2025
πŸ‘4
KENYA: Ripoti ya Wizara ya Afya kwa ushirikiano wa African Population and Health Research Centre (APHRC) na Taasisi ya Guttmacher imeeleza kuwa kati ya Aprili 2023 na Mei 2024, zaidi ya visa 792,000 vya utoaji mimba vimeripotiwa Nchini #Kenya

Ripoti imeeleza namba hiyo ni sawa na wastani wa visa 57.3 kati ya Wanawake 1,000 wenye umri wa miaka 15 – 49, na Asilimia 80 ya wanaofanya hivyo wapo kwenye ndoa

Mtafiti Mkuu wa Guttmacher, Margaret Giorgio amesema β€œWanaotoa wanafanya hivyo kwa kuwa hawajajiandaa kuwa wazazi, pia wengine ambao tayari wameshakuwa na Watoto wanachukua hatua hiyo kutokana na kuhofia gharama za maisha kuwa kubwa.”

Soma https://jamii.app/AbortionsKenya

#PublicHealth #JamiiForums #PublicHealth
πŸ‘1πŸ‘Ž1
Muda mfupi baada ya Rais Donald Trump kupost picha yake iliyotengenezwa kwa AI yenye Mwonekano wa Mavazi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani (Papa) na kukosolewa na wengi Mtandaoni, Uongozi wa Kanisa Katoliki New York umemwambia Trump asiwakejeli

Kupitia ukurasa wao wa X (zamani Twitter), Uongozi wa Kanisa Katoliki New York ulisema kuwa hakuna cha kufurahisha kuhusu alichokifanya Trump, hasa ikizingatiwa kuwa Kanisa bado linaomboleza kifo cha Papa Francis aliyezikwa Aprili 26, 2025 na lipo kwenye mchakato wa kumpata kiongozi mpya, hivyo kumtaka Trump kutochukulia jambo hilo kwa mzaha

Zaidi https://jamii.app/TrumpPapa

#JamiiForums #JamiiAfrica
😁3πŸ‘1
Mdau wa JamiiForums.com anasema Vijana msikubali kubanwa na Visingizio. Kama huwezi kuwa Mwanafunzi bora, basi kuwa Mfanyabiashara hodari. Kama huwezi kuwa Mfanyabiashara mkubwa, basi anza na vibanda. Kama huwezi kuwa na Duka, tafuta bidhaa na utembeze. Vyovyote iwavyo hakikisha unapiga hatua

Anasema kuwa na Mtaji mdogo sio shida, unachohitaji ni Wazo bora, Akili za Mtaani na Darasani huku akitaja Biashara unazoweza kuzifanya kwa Mtaji wa kuanzia Tsh. 20,000–100,000.

Fungua hapa kufahamu Mawazo ya Biashara aliyoyataja https://jamii.app/PambanaKiakili

#JamiiForums #JamiiAfrica #Biashara #Uchumi #Ujasiriamali
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Familia ya marehemu Edga Mwaniwe, Wakazi wa Manispaa ya Mpanda imegoma kuuchukua mwili wa ndugu yao huyo kwa ajili ya maziko uliohifadhiwa Hospitali ya Manispaa Mpanda, leo Mei 4, 2025 ikiwa ni siku ya saba

Msemaji wa familia hiyo, Charles Mwaniwe amesema kifo cha ndugu yao kina utata na kwamba mshukiwa namba moja hajachukuliwa hatua na Jeshi la Polisi

Taarifa ya Polisi kuhusu tukio hilo imesema inawashikilia Watu Saba kwa kusababisha kifo cha Edga kwa kumshambulia wakimtuhumu kuuza madini feki kwa Tsh. 570,000 kwa Robert Benedict ambaye ndiye familia inamtuhumu

Kuhusu Robert, Polisi imesema alifika eneo la tukio na kukuta Edga akishambuliwa, akamchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi baadaye hospitali ambapo alipoteza maisha

Soma https://jamii.app/KataviTukio

#JFMatukio #JamiiForums #Accountability #HumanRights
πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Makamu wa Rais Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Eusebius Nzigilwa amesema tukio la kushambuliwa kwa Katibu wa Baraza hilo, Padre Charles Kitima lilitaka kupora haki ya uhai, uhuru wa haki yake ya kusema na kutenda kadiri ya wito wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, huku akiongeza kuwa ni shambulio dhidi ya heshima ya taifa kwani linajulikana kuwa kisiwa cha amani.

Askofu Nzigilwa amesema hayo leo Mei 04, 2025 katika Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa`ichi OFMCap, katika ibada ya kusimikwa kwa askofu Stephano Musomba wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo

Soma https://jamii.app/Mei4TEC

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Accountability #SocialJustice
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi limesema linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na Mwananchi (ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa) kupitia Mitandao ya Kijamii, akiwatuhumu askari Wawili kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi huku wakitaka kufahamu alipo Mdude

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimefika Mbeya kwaajili ya uchunguzi zaidi wa suala hilo, huku likitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli wa suala hilo atoe ushirikiano

Soma https://jamii.app/UchunguziMei4

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice
πŸ‘1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefika Ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoani humo kwa lengo la kumpa ushahidi wa watu wanaodai ni askari ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la kumjeruhi kisha kumteka Mpalukwa Nyagali, maarufu kama Mdude

Aidha, Wanachama hao wamedai kuwa wataendelea kuandamana kwenda Ofisini kwa RPC kila siku, mpaka watakapopata Majibu ya mwisho ya Mdude yupo wapi

Soma https://jamii.app/UshahidiMdude

#JamiiForums #HumanRights #SocialJustice #JamiiAfrica #Accountability
πŸ‘1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
❀1