JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Haki za wachache ni za muhimu kama yalivyo Matamanio ya wengi; Viongozi wa Kidemokrasia huhakikisha pande zote zinazingatiwa kwa usawa.

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #GoodMorning #AmkaNaJF #Quotes
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Barabara ya Kitunda - Banana imeendelea kuwa kero kubwa kwa Watumiaji kutokana na uwepo wa mashimo kiasi kwamba kuna Gari nyingi zikiwemo Daladala zimebadilishiwa ‘ruti’ na kusababisha Watu wengi kukosa usafiri

Soma https://jamii.app/KitundaBananaRoad

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
Mdau wa JamiiForums.com anasema kumbukumbu za Binamu yake alivyokuwa akimnyanyasa Kingono Utotoni zinamtesa na anaumia akikumbuka ambavyo Mama yake hakulipa uzito suala hilo, kila alipomwambia kinachoendelea

Anasema changamoto anazozipitia sasa ni kukosa Imani na Ujasiri wa kukaa na Ndugu zake wa kiume sehemu moja, anashindwa kulala gizani kwa Miaka 29 sasa, anapenda Watoto ila hataki Kuzaa na kuna muda anatamani kufa sababu anaona Kifo kitakuwa zawadi kwake

Soma zaidi https://jamii.app/NduguKuharibuWatoto

#JamiiForums #Maisha #ChildAbuse #SexualViolence
#MICHEZO: Yanga imesema baada ya maelezo ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuitaka Klabu hiyo kurejea katika Mamlaka za Tanzania kuhusu suala lao la kutocheza dhidi ya Simba, msimamo wao ni kuwa hawana imani na hawako tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhuluma

Yanga imeeleza sababu za kufanya hivyo ni kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya Timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania

Taarifa ya Klabu hiyo imeeleza kuwa Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania Haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhuluma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za Soka kwa maslahi mapana ya Maendeleo ya Soka Nchini

Soma https://jamii.app/YangaTamko

#JFSports #JamiiForums
👍2
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024, anasema ifikapo Mwaka 2035 Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (UVIMADA), itakuwa janga kubwa zaidi kwani Tanzania imo kwenye orodha ya Nchi 14 za Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye kiwango kikubwa cha UVIMADA

Anapendekeza uanzishwe Mfumo maalumu wa kukusanya taarifa (Kanzi Data) za Kimaabara za Wagonjwa wenye UVIMADA, utakaoratibiwa kwenye ngazi ya kanda ili kufuatilia ukubwa wa Janga, kupanga mipango Kisera na kibajeti, kuratibu tafiti pamoja na kutoa miongozo

Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/UVIMADASOC2024

#JamiiForums #JamiiAfrica #PublicHealth #Afya
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MANYARA: Suzana Samweli (13), Mwanafunzi wa Darasa la 6, Mkazi wa Kata ya Galapo, Wilaya ya Babati ameuawa kikatili na mwili wake kukutwa umetupwa shambani

Familia ya marehemu imesema Suzana hakurudi nyumbani Jioni ya Aprili 29, 2025, baada ya kutoka shuleni na mwili wake ukapatikana shambani Mei 1, 2025, ikielezwa alibakwa na kutobolewa macho

Akizungumza na Kituo cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Ahamed Makarani amesema wanamshikilia Elias Daniel (26), Mkazi wa Kijiji cha Gedamar kwa mahojiano zaidi, pia yapo matukio mengine ya aina hiyo ambayo hayakuripotiwa Polisi

Soma https://jamii.app/MwanafunziAuawa

#JamiiForums #JFMatukio #HumanRights
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema wanamshikilia Mtu mmoja aliyedaiwa kuchapisha taarifa kwenye Ukurasa wa X (Twitter) akiandika “Siku za Padre Kitima zinahesabika”

Muliro amesema "Amekamatwa na anahojiwa, anaitwa Frey Edward Cossey (51), Mkazi wa Dodoma na Mbezi Beach Makonde kufuatia chapisho lake la vitisho dhidi ya Padri Charles Kitima alilolitoa kwenye Mitandao ya Kijamii siku chache kabla ya tukio."

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, alishambuliwa na kujeruhiwa Aprili 30, 2025 ikiwa ni siku mbili baada ya andiko hilo la Mtandaoni

Soma https://jamii.app/MuliroMei5

#JFMatukio #Accountability
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Dorothy Jonas Semu, Kiongozi wa Chama cha #ACTWazalendo akizungungumza katika sherehe za kutimiza Miaka 11 ya Chama hicho amesema hawapo tayari kususia Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kuwa watapambana wakati wakishiriki na watashiriki wakiwa wanapambana

Amesema “Huu ni Mwaka wa kuinusuru Zanzibar, Mwaka wa maamuzi. Ni Mwaka wa kukata kiu ya muda mrefu ya Wazanzibari ya kupata Zanzibar mpya, #Zanzibar moja na yenye Mamlaka kamili.”

Ameongeza kuwa ACT inapendekeza; Wakurugenzi wa Halmashauri wasisimamie Uchaguzi, Wajumbe wapya wa INEC wateuliwe, Kura haramu zidhibitiwe, Wagombea wasienguliwe ovyo, Mawakala wawe huru na Vyombo vya Dola visishiriki hujuma kwenye Uchaguzi.

Soma https://jamii.app/ACTMei5

#UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy #Siasa
👍2
Bunge la Ulaya linatarajia kufanya mjadala Mei 7, 2025 kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ikiwemo ya Uhaini ambayo kama atakutwa na hatia moja ya adhabu yake ni kifo

Taarifa ya tovuti ya Bunge hilo imeeleza kuwa Mjadala huo utagusia masuala ya Haki za Binadamu, Demokrasia na Uhuru, ambapo mjadala utafanyika kuanzia Saa 8:00 Mchana hadi Saa 5:00 Usiku

Baada ya mjadala huo, Wabunge wa Bunge hilo watakuwa na ratiba ya kupiga Kura, kesho yake Mei 8, 2025

Soma https://jamii.app/BungeLaUlaya

#JamiiForums #Democracy
🔥1
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akishauri watu kupunguza matukio ya kimahaba mbele ya Wazazi siku ya harusi, kama kulishana keki mdomo kwa mdomo

Unadhani ni mambo gani hayapaswi kufanyika ukumbini siku ya harusi?

Mjadala https://jamii.app/ScenesZaHarusi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeStyle
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kiongozi wa Chama cha #ACTWazalendo, Dorothy Jonas Semu, amesema Chama chao kimetangaza kupigania maboresho ya Mfumo wa Uchaguzi hadi dakika ya mwisho na kuwa Chaguzi tatu zilizopita zimewaonesha sura halisi ya adui yao kuwa sio CCM tu bali Vyombo vya Dola

Ameongeza “Tupaze Sauti zetu hadi Uchaguzi Mkuu 2025 uwe huru, wa haki na wa kuaminika. Madai yetu sita yawe ndio wimbo wetu kuanzia saa hadi Oktoba.”

Soma https://jamii.app/ACTMei5

#UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy #Siasa
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Mdau anadai kivuko kinachounganisha Pangani na Bweni kimekuwa na hitilafu za mara kwa mara na kimegeuka kero kwa Watumiaji kutokana na kukwama mara kadhaa kwenye Maji

Anadai athari zinazojitokeza ni hofu kwa Watumiaji, kutishia soko la Watalii akitoa mfano maeneo kama Pwani ya Ushongo yenye Hoteli na nyumba binafsi za kulaza wageni yameathiriwa na usafiri huo kwa kuwa Daraja linalojengwa bado haijaruhusiwa kutumika muda wote

Anadai athari nyingine ni usambazaji wa Bidhaa pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi kukwama. Anatoa wito kwa Mamlaka husika kuchukua hatua kwa kuwa athari zinazojitokeza ni kubwa

Soma https://jamii.app/KivukoPangani

#ServiceDelivery #JamiiForums #HudumaZaKijamii #JFMdau2025 #JamiiAfrica
👍4
Hatuwezi kurudisha Muda nyuma na hatuwezi kubadili yaliyopita, lakini matendo yetu ya leo yanaweza kuamua kile ambacho kesho yetu itakibeba

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning
👍21
Mchezo wa #Yanga dhidi ya #Simba wa Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Bara 2024/25 ambao uliahirishwa, sasa umepangwa kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa

Ikumbukwe, Yanga imetangaza kuwa haitashiriki mchezo huo na tayari iliwasilisha malalamiko yao kwa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), lakini shauri lao likakwama, wakatakiwa kurejea katika Mamlaka za Nchini, jambo ambalo wamesema hawawezi na hawatacheza Mchezo huo

Mdau, unadhani Yanga watashikilia msimamo wao au ‘mbungi’ itapigwa?

Soma https://jamii.app/DerbyJune15

#JFSports #JamiiForums #KariakooDerby
🤣2
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa baadhi ya akaunti zao rasmi za Mitandao ya Kijamii zimedukuliwa

Taarifa imeeleza ”Tunaarifu kuwa akaunti zetu za X (zamani Twitter) - ChademaTZ na YouTube - Chadema Media zimeingiliwa na Wadukuzi, taarifa rasmi za CHADEMA zinapatikana kupitia akaunti ya muda ya X: @ChademaTZ2

Imeongeza “Tunaendelea kuchukua hatua za kiusalama na Kisheria kurejesha udhibiti, kwa sasa, tunaomba wafuasi wawe makini na kupuuza taarifa zinazochapishwa kwenye akaunti zilizodukuliwa hadi tutakapotoa taarifa rasmi ya kurejesha udhibiti.”

Soma https://jamii.app/CHADEMAKudukuliwa

#JamiiForums #Accountability #JFDigital #Kuelekea2025
👍1