Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Kitaifa (NEMA) imeielekeza Halmashauri ya Kaunti ya Jiji la Nairobi kuondoa taka zilizoachwa nje ya Makao makuu ya Kampuni ya Kenya Power and Lighting Company (KPLC), kufuatia mzozo unaoendelea kuhusu gharama za Huduma ambazo hazijalipwa
Pamoja na kumwaga Uchafu, Halmashauri ya Jiji la #Nairobi imeziba njia ya Maji taka katika ofisi za KPLC katikati ya jiji la Nairobi, hali iliyosababisha kutiririka kwa Majitaka Barabarani na kuhatarisha Mazingira
KPLC inailaumu Kaunti ya Nairobi kwa kushindwa kulipa deni lake la Umeme linalofikia Ksh. Bilioni 3 (Tsh. 60,583,158,475), huku kaunti nayo ikidai KPLC ina deni la Ksh. Bilioni 4.8 (Tsh. 96,933,053,559.80) kama ada kwa matumizi ya Ardhi ya Umma na Miundombinu kwa ajili ya nyaya za Umeme (wayleave fees)
Soma https://jamii.app/KLPCvsCityHall
#JamiiForums #JFMatukio #KenyaPower #NairobiCityCouncil #Kplc #NCC

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 37, inaeleza mhusika wa taarifa ana Haki ya kulipwa fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji wa Taarifa iwapo atapata madhara kwa sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria hiyo
Endapo Tume itajiridhisha na maombi ya mhusika wa taarifa kuwa amepata madhara katika mazingira yanayompatia haki ya kulipwa fidia inaweza kuamuru kurekebishwa, kuzuiwa, kufutwa au kuharibiwa kwa taarifa hizo.
Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako

Unamshauri Mdau afanye nini hapa, aondoke au aendelee kuziba Masikio kwenye Masimango anayopewa na 'Shosti' wa rafiki yake?
Mjadala zaidi https://jamii.app/KukaaRafikiMafumbo
#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons

DAR: Leo, Februari 26, 2025 Mahakama Kuu imemhukumu kunyongwa hadi kufa Khamis Luwonga, kwa kumuua Mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia Magunia mawili ya Mkaa Mei 15, 2019
Luwonga alitenda kosa hilo Nyumbani kwake Gezaulole, Wilayani Kigamboni ambapo inadaiwa masalia ya Mwili na Majivu alikwenda kuyazika Shambani na kupanda Migomba juu yake
Soma https://jamii.app/HukumuLuwonga
#JamiiForums #JFMatukio
Luwonga alitenda kosa hilo Nyumbani kwake Gezaulole, Wilayani Kigamboni ambapo inadaiwa masalia ya Mwili na Majivu alikwenda kuyazika Shambani na kupanda Migomba juu yake
Soma https://jamii.app/HukumuLuwonga
#JamiiForums #JFMatukio
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa inatarajia kuanza mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya Uchaguzi, kesho Februari 27, 2025 zoezi ambalo litaendelea hadi Machi 26, 2025
Mwenyekiti wa #INEC, Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele amesema maombi yote ya mchakato huo yawasilishwe INEC ndani ya muda huo unaofanyika kwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya 18(1) ya INEC ya Uchaguzi za Mwaka 2024
Ameeleza, wenye maombi wahakikishe yanajadiliwa katika Kamati ya Ushauri ya Wilaya, kisha yawasilishwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwaajili ya kujadiliwa katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa awasilishe Tume mapendekezo yaliyopitishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na viambatanisho vyote
Soma https://jamii.app/UgawajiMajimbo
#JamiiForums #Uchaguzi2025 #Kuelekea2025 #HakiZaKiraia #Democracy

Mdau wetu Kijana, na wewe Mwaka huu (2025) una mpango wa kugombea nafasi gani kwenye Uchaguzi Mkuu?
Tembelea Mjadala huu zaidi https://jamii.app/VijanaKugombea
#JamiiForums #Demokrasia #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu25

Unadhani mfumo wetu wa #Elimu unachangia kwa namna yoyote katika kukuza au kupunguza ‘uchawa’? Una maoni gani katika eneo hili?
Ili kutoa maoni yako usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unazorotesha Uwajibikaji?" Alhamisi ya Februari 27, 2025 kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa

👍2
MICHEZO: Kocha Erik ten Hag ametoa kauli ambayo inaonesha kuna uwezekano wa kutorejea kufundisha Soka badala yake akaelekeza nguvu kwenye kazi zake binafsi
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa #ManchesterUnited, Miezi minne iliyopita kisha nafasi yake kuchukuliwa na Ruben Amorim, #TenHag amesema anajihusisha na usimamizi wa Kampuni ya Familia yake na kuwa suala la kufundisha anaweza kuanza kulifikiria kuanzia Julai 2025
Familia ya Ten Hag ni moja kati ya familia tajiri Nchini Uholanzi ikiwa na uwekezaji kwenye majengo, hivyo anasimamia Miradi iliyoanzishwa na Baba yake Mwaka 1967
Soma https://jamii.app/TenHagCareer
#JamiiForums #JFSports

👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Ndolezo Petro, kutoka #ACTWazalendo ameitaka Serikali kumuachia huru Katibu wa Umoja wa Walimu wasio na Ajira Tanzania (NETO), Daniel Edger Mkinga, baada ya kudaiwa amekamatwa akiwa Kibaha Miembe Saba (Pwani) Nyumbani kwake
Awali, Makamu Mwenyekiti wa NETO, Agness Mpundi, alisema “Tunaomba Wanasheria wenye mapenzi mema na Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu watusaidie kupata Uhuru wake. NETO sio Chama cha kisiasa, genge la Wahalifu wala haina nia yoyote ovu dhidi ya Amani ya Nchi yetu, adhima kuu ya NETO ni kuomba Ajira za Walimu wa Serikali na kusisitiza kufanyia kazi makala tuliyoiandikia Serikali.”
Soma https://jamii.app/NdolezoOnNETO
#JamiiForums #Governance #JFMatukio #CivilRights

Kumbuka kulinda taarifa zako na usikubali kuziweka wazi au kumpa mtu mwingine bila kujua lengo na matumizi ya taarifa zako
Usipolinda taarifa zako zinaweza kutumika katika Matukio ya Uhalifu kama vile Uwizi na Utapeli wa Mtandaoni
Mjadala zaidi https://jamii.app/PrivacyIsPower
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Usipolinda taarifa zako zinaweza kutumika katika Matukio ya Uhalifu kama vile Uwizi na Utapeli wa Mtandaoni
Mjadala zaidi https://jamii.app/PrivacyIsPower
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Mgombea anayetoa pesa ili achaguliwe siyo Kiongozi wa Watu bali ni Mfanyabiashara anayewekeza ili avune baadaye
Akiingia madarakani, atatafuta kurudisha pesa zake kwanza, siyo kuboresha maisha ya Wananchi.
Kiongozi wa kweli hahongi Wapigakura, anasimama kwa hoja, uwezo na maono ya kweli ya kuleta maendeleo
Epuka ‘Matapeli wa Siasa’, Kataa Rushwa ya Uchaguzi
#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Transparency

MOROGORO: Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, alisema hayo alipotembelea washiriki wa mafunzo ya Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya Jimbo katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Februari 23, 2025
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Machi 1, 2025 hadi Machi 07, 2025, katika Mikoa ya Morogoro na Tanga (Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga)
Soma https://jamii.app/MoroUandikishaji
#JamiiForums #Uchaguzi2025 #Kuelekea2025 #HakiZaKiraia #Democracy #JFNukuu #JFQuotes