Usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Alhamisi hii ya Februari 27, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia #Xspaces ya JamiiForums
'Washtue' ndugu, jamaa au marafiki ili wawe sehemu ya Mjadala huu muhimu kwa kesho ya Nchi yetu
Washiriki watapata fursa ya kutoa maoni au mapendekezo na kuuliza maswali kwa Wazungumzaji wetu
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa

❤1👍1
DAR: Mwanachama wa JamiiForums.com anadai kuna baadhi ya bidhaa zikiwemo za Vyakula ambazo zimepitiliza muda wake wa matumizi lakini bado zipo sokoni, akitoa mfano anadai amekutana na hali hiyo maeneo ya Salasala Kwa Mtenga
Anashauri Wanunuaji wawe na kawaida ya kuzingatia kuangalia taarifa kwenye vifungashio ili kukwepa madhara ya kiafya, pia anahoji wale wauzaji wa mwisho wakibaini bidhaa walizonazo “zime-expire” wanazipeleka wapi?
Anashauri Mamlaka ziweke msisitizo wa wauzaji wa kati kukaguliwa kabla ya kupeleka bidhaa kwa muuzaji wa mwisho ambaye ndiye anayemuuzia mtu wa mwisho, amesema anajua maelekezo hayo yapo kwenye karatasi lakini yafanyike kwa vitendo
Soma https://jamii.app/BidhaaUkaguzi
#JamiiForums #PublicHealth #Accountability

👍1
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 61 inaeleza Mtu kuharibu, kufuta, kupotosha, kuficha au kubadilisha Taarifa Binafsi kinyume na Sheria ni kosa
Endapo atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Tsh. 100,000 na isiyozidi Tsh. Milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja
Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako

DAR: Mshtakiwa katika Kesi Namba Cc. 5866, Baraka Benedicto ambaye anashtakiwa kwa kosa la ulawiti, ameshindwa kutoa utetezi wake kama ilivyopangwa kwa maelezo kuwa anaumwa licha ya kufanikiwa kufika Mahakamani, jana Februari 26, 2025
Kesi hiyo ambayo ilifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 2024 siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuomba Mamlaka kuchukua hatua kumsaidia mtoto husika, ilitajwa kwa ajili ya mshtakiwa kutoa ushahidi wake ikiwa ni baada ya mashahidi wa Jamhuri kutoa ushahidi wao
Baada ya hoja hiyo, Mahakama kupitia Hakimu Nabwike Mbaba imeahirisha Shauri hilo hadi Machi 3, 2025, ambapo mshtakiwa atakuja kutoa ushahidi wake.
Soma https://jamii.app/MahakamaniFeb27
#CivilRights #JamiiForums #HumanRights

DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mwanasiasa mkongwe Dkt. #WillibrodSlaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo
Dkt. Slaa alishtakiwa kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter)
Soma https://jamii.app/SlaaAachiwa
#JamiiForums #Governance

DAR: Kesi Namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39) mkazi wa Salasala, Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi-Africana anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi imetajwa Februari 26, 2025 kisha kuahirishwa baada ya Mahakama kuelezwa kuwa Afisa aliyetakiwa kumuandaa shahidi alipata udhuru
Baada ya Wakili wa Jamhuri kuwasilisha sababu hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa kesi hiyo imeahirishwa mpaka Machi 24, 2025 ambapo itakuja kwaajili ya kutajwa
Mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani siku chache baada ya Mwanachama wa Jamiiforums.com kuhoji sababu za kutofikishwa mahakamani kwa Watuhumiwa aliodai wanahusika na vitendo vya ukatili katika Shule hiyo. Baada mshtakiwa kufikishwa Mahakamani alisomewa shtaka la ulawiti lakini alikana kuhusika.
Soma https://jamii.app/SalehAyoubDeb27
#JamiiForums #JFMatukio #CivilRights

Ni kwa jinsi gani Vyama vinaweza kushirikiana kuhakikisha Uwajibikaji unakuwa sehemu ya Utamaduni wa Kisiasa, badala ya 'Siasa za kupambana' kwa misingi ya itikadi pekee?
Kutoa maoni na mapendekezo yako shiriki katika Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Alhamisi hii ya Februari 27, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Kutoa maoni na mapendekezo yako shiriki katika Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Alhamisi hii ya Februari 27, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Unakubaliana na Hoja ya Mdau huyu? Umeshawahi kupitia changamoto yoyote Kazini iliyosababishwa na 'Ukabila'?
Mjadala zaidi https://jamii.app/UkabilaMaofisini
#JamiiForums #JFStories #JFChitChats #Maisha #LifeLessons

Mjadala wa "Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" upo hewani muda huu kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku, kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Hii ni nafasi yako kusikiliza hoja za Wadau na Wananchi mbalimbali na kushiriki ikiwemo kwa kuuliza maswali
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Hii ni nafasi yako kusikiliza hoja za Wadau na Wananchi mbalimbali na kushiriki ikiwemo kwa kuuliza maswali
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
👍1
Akizungumza katika Mjadala wa “Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Mwandishi wa Habari (The Chanzo), Khalifa Said amesema “Hautakiwi kushangaa kuona siku hata usiyemtegemea akajiunga kwenye timu ya hao wanaoitwa 'Machawa' kwa kuwa atakuwa anafanya hivyo ili kuweza kuishi”
Amesema kuwa hao Watu wanaoitwa Chawa wanafanya hayo ili waweze kuishi, hao Watu wamekuwa na ujasiri wa kujiunga nao ili nao wapate shea ya keki ya Taifa
Ameongeza kwa kusema kuwa kila mtu anataka kuishi maisha mazuri hivyo uchawa sio sababu ya kukosekana kwa Uwajibikaji, matumizi mabaya ya madaraka ndio chanzo
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Amesema kuwa hao Watu wanaoitwa Chawa wanafanya hayo ili waweze kuishi, hao Watu wamekuwa na ujasiri wa kujiunga nao ili nao wapate shea ya keki ya Taifa
Ameongeza kwa kusema kuwa kila mtu anataka kuishi maisha mazuri hivyo uchawa sio sababu ya kukosekana kwa Uwajibikaji, matumizi mabaya ya madaraka ndio chanzo
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Akichangia katika Mjadala wa “Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Mkuu wa Idara ya Programu (TCD), Carlos Buto amesema “Ipo mifano ya Nchi kadhaa, mfano Nchi za Magharibi kama Norway, Ujerumani, Canada ukiangalia siasa zao sio za kubebana kwa mambo ya kusifiana, yanaziangatia hoja na Utendaji wa Taasisi”
Ameongeza kwa kusema kuwa Boksi la Kura linaamua namna gani unamwajibisha Kiongozi, hivyo kama kiongozi hana mwenendo mzuri wa utendaji Kura yako ndio itakayomuwajibisha
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Ameongeza kwa kusema kuwa Boksi la Kura linaamua namna gani unamwajibisha Kiongozi, hivyo kama kiongozi hana mwenendo mzuri wa utendaji Kura yako ndio itakayomuwajibisha
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
👍1
Akizungumza katika Mjadala wa “Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Mkurugenzi wa Uchechemuzi (Twaweza), Annastazia Rugaba amesema kuwa #Uchawa unachangiwa na vitu vingi ikiwemo ukosefu wa Ajira
Ameongeza kwa kusema kuwa #Uchawa ni aibu kwani kuna watu wanafanya vitu vya aibu kwenye Jamii mpaka unawaonea huruma
Amesema “Inatakiwa Wananchi wafahamu kuwa kodi yao ndio ambayo inawezesha mafanikio ya Serikali ikiwemo miradi inayozinduliwa na Viongozi wa Serikali"
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Ameongeza kwa kusema kuwa #Uchawa ni aibu kwani kuna watu wanafanya vitu vya aibu kwenye Jamii mpaka unawaonea huruma
Amesema “Inatakiwa Wananchi wafahamu kuwa kodi yao ndio ambayo inawezesha mafanikio ya Serikali ikiwemo miradi inayozinduliwa na Viongozi wa Serikali"
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
👍1
Akichangia katika Mjadala wa “Je, 'Uchawa' unakwamisha Uwajibikaji?" Mwaura Robert (Mdau) amesema kuwa #Uchawa haupo tu kwenye Siasa kuna wakati ulifika hadi katika Mamlaka za Kisheria, uamuzi ulifanyika huku mhusika anayefanya maamuzi akilenga kupandishwa cheo
Ameongeza kuwa Watu ambao wanatokana na upendeleo wanapofanya kazi duni hawawezi kuwajibishwa
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Ameongeza kuwa Watu ambao wanatokana na upendeleo wanapofanya kazi duni hawawezi kuwajibishwa
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
👍1
Mkurugenzi wa Uchechemuzi (Twaweza), Annastazia Rugaba amechangia mjadala kwa kusema “Wakati mwingine Uchawa unaharibu Viongozi, wapo wanaoingia wakiwa na nia ya kufanya mabadiliko kweli lakini kwa kuwa tunakuwa na tamaduni ya kuwasifia sana, wanazoea na inapotokea wanahojiwa wanakuwa wakali”
Ameongeza kwa kusema kuwa “Tusipopambana na umasikini itakuwa ngumu sana kuondokana na #Uchawa. Viongozi wanajua hilo ndiyo maana wanatamani Machawa waendelee”
Amesema kuwa #Uchawa huweza kuzuia Uwajibikaji kwa sababu Watu wenye Uhaba wa rasilimali mara nyingi hujikita zaidi katika kukidhi mahitaji ya msingi kuliko kufuatilia utendaji wa Viongozi
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Ameongeza kwa kusema kuwa “Tusipopambana na umasikini itakuwa ngumu sana kuondokana na #Uchawa. Viongozi wanajua hilo ndiyo maana wanatamani Machawa waendelee”
Amesema kuwa #Uchawa huweza kuzuia Uwajibikaji kwa sababu Watu wenye Uhaba wa rasilimali mara nyingi hujikita zaidi katika kukidhi mahitaji ya msingi kuliko kufuatilia utendaji wa Viongozi
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Mkuu wa Idara ya Programu (TCD), Carlos Buto akichangia katika mjadala amesema kuwa #Uchawa unaanzia katika ngazi ya Familia zetu na ni ngumu kuuondoa katika ngazi ya Taifa
Ameongeza kwa kusema tunatakiwa kubadilisha mifumo yetu ya Kisiasa, pia kutambua mchango wa Vyombo vya Habari na kuangalia vina uwezo gani wa kujiendesha
Amesema “Kunapokuwa na ombwe hasa katika Mitandao ya Kijamii wapo watu wanatumia fursa hiyo kupeleka ujumbe vile wanavyoona inafaa na hiyo inaweza kuwa moja ya njia ya kuwaharibu Vijana"