JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Kitaifa (NEMA) imeielekeza Halmashauri ya Kaunti ya Jiji la Nairobi kuondoa taka zilizoachwa nje ya Makao makuu ya Kampuni ya Kenya Power and Lighting Company (KPLC), kufuatia mzozo unaoendelea kuhusu gharama za Huduma ambazo hazijalipwa

Pamoja na kumwaga Uchafu, Halmashauri ya Jiji la #Nairobi imeziba njia ya Maji taka katika ofisi za KPLC katikati ya jiji la Nairobi, hali iliyosababisha kutiririka kwa Majitaka Barabarani na kuhatarisha Mazingira

KPLC inailaumu Kaunti ya Nairobi kwa kushindwa kulipa deni lake la Umeme linalofikia Ksh. Bilioni 3 (Tsh. 60,583,158,475), huku kaunti nayo ikidai KPLC ina deni la Ksh. Bilioni 4.8 (Tsh. 96,933,053,559.80) kama ada kwa matumizi ya Ardhi ya Umma na Miundombinu kwa ajili ya nyaya za Umeme (wayleave fees)

Soma https://jamii.app/KLPCvsCityHall

#JamiiForums #JFMatukio #KenyaPower #NairobiCityCouncil #Kplc #NCC