Katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni muhimu kutambua kuwa kiongozi wa kweli hauzi dhamira yake kwa pesa, bali hujenga uaminifu kupitia sera madhubuti na mipango thabiti kwa jamii yake.
Mpotezee mtoa rushwa! Chagua kiongozi mwenye dira na mipango inayolenga kuboresha maisha ya Wananchi wote
#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji

👍2
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haijafanya mazungumzo wala kutoa maelekezo yoyote ya kupewa leseni au kuruhusiwa kwa Kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL), tofauti na taarifa mbalimbali zinazosambaa Mitandaoni
Aidha, Hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya Maafisa wa LBL kwa kujihusisha na ulaghai ikiwemo kupokea Amana, kutoa riba na kufanya uhaulishaji wa Fedha bila leseni ya BoT
Wiki iliyopita Maafisa kadhaa wa #LBL walikamatwa katika Mikoa ya Morogoro, Mbeya, Manyara, Geita na Mtwara kwa tuhuma za kuendesha Biashara haramu ya Fedha (Upatu) bila kibali
Soma https://jamii.app/BOTLeseniLBL
#Governance #JamiiForums #DigitalWorld

👍1
DAR: Matukio mbalimbali wakati wa warsha iliyoandaliwa na JamiiAfrica, kuwakutanisha Wanahabari na Wadau wa Habari kupeana elimu kuhusu umuhimu wa kuripoti Habari na taarifa zenye maslahi ya Umma, lengo likiwa ni kuhamasisha Utawala Bora na Uwajibikaji
Warsha hiyo ya siku moja ilifanyika katika Hoteli ya Protea, Februari 19, 2025, ambapo Washiriki waliuliza maswali, kubadilishana uzoefu na kugusia ufahamu wao kuhusu lengo husika
Soma https://jamii.app/MbwaMtaani
#JamiiForums #JFMatukio #Accontability #FreedomOfExpression

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Jacob Twange amewataka Wananchi kuvumilia changamoto ya uhaba wa maji pamoja na ubovu wa Barabara katika Kata ya Kimara, akiahidi kuwa anafuatilia mipango aliyoikuta ya kuboresha huduma na miundombinu
Kwa nyakati tofauti Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto za ubovu wa Barabara, maboresho kwenda taratibu, maji kutoka kwa mgao na baadhi ya maeneo kutokuwa na maji kabisa
Soma https://jamii.app/KataYakimara
#HudumaZaKijamii #Accountability #JamiiForums

Ndani ya Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko la JamiiForums.com, Mwanachama ameanzisha Mjadala akitoa wito kwa Serikali iangalie namna ya kuanzisha Mfumo wa Mawasiliano ya Simu kati ya Wafungwa pamoja na Wapendwa wao waliopo Uraiani
Unakubaliana na hoja zake?
Shiriki Mjadala https://jamii.app/MawasilianoWafungwa
#JamiiForums #Governance
Unakubaliana na hoja zake?
Shiriki Mjadala https://jamii.app/MawasilianoWafungwa
#JamiiForums #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KIGOMA: Mahakama ya Wilaya imebatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Geza Ulole Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuamuru Uchaguzi urudiwe baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya Uchaguzi
Uamuzi huo umetokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa mtaa huo kutoka Chama cha #ACTWazalendo, ambaye hakuridhika na matokeo yaliyotangazwa
Akizungumza na Jambo TV baada ya hukumu hiyo, Wakili Thomas Msasa ameeleza moja ya sababu za kufungua kesi hiyo ilikuwa ni uwepo wa kura feki ambazo zilitumbukizwa kwenye masanduku ya kura na baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi.
Soma https://jamii.app/BatiliLGEGezaUlole
#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #CivilRights #Demoracy #HakiZaKiraia #UsawaKisheria #UchaguziSerikaliMitaa2024

Elimu bora haipaswi kuwa Haki ya wachache bali ya kila Mtoto, popote alipo
Viongozi wanapaswa kuhakikisha kila Mtoto anapata fursa sawa ya kujifunza, bila kujali mahali anapoishi
Taifa lenye Watoto wasio na Elimu ni Taifa lenye mustakabali wenye giza.
#ElimuNiHaki #JamiiForums #CivilRights #HakiZaKiraia #ElimuKwaWote #HudumaZaKijamii #ElimuKwaUsawaNaHaki

❤1
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 33 (1b) mhusika wa taarifa ana Haki ya kufahamishwa madhumuni ya Taarifa Binafsi zinazomhusu pamoja na maelezo ya wapokeaji watakaopewa taarifa hizo
Aidha, mkusanyaji hatalazimika kutoa maelezo ya ukusanyaji wa taarifa hizo iwapo zinahusika katika uchunguzi kwa mujibu wa sheria au zimezuiliwa kwa amri ya Mahakama
Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako

Mdau anadai Wanachama wa mchezo wa LBL (Leo Beneath London) ambao Serikali imeupiga marufuku, wanaelekeza kuwa ili kukomboa fedha zao zilizopo ndani ya mfumo wanatakiwa kulipa nusu ya fedha ambazo alilipia wakati anajiunga, mfano ngazi ya P3 waliolipia Tsh. 540,000 wanaelekezwa kulipa Tsh. 270,000, akieleza kuna wanaofanya hivyo na fedha hazirudi
Ameshauri, pamoja na Serikali kuwadhibiti waratibu wa LBL, Watu waache kutuma hela hizo ili kukomboa kile walichopoteza, badala yake wasubiri maelekezo ya Serikali na kwa waliopata hasara kubwa watafute njia sahihi vinginevyo watazidi kupoteza hela
Soma https://jamii.app/LBLAgain
#JFDigital #DigitalWorld #JamiiForums