JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Akihojiwa katika Kituo cha ITV, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla, amesema "CCM ina uwezo mkubwa wa kujaza Mikutano bila wasanii, CCM ina wanachama milioni 12, CCM ndio chama kikubwa Tanzania, CCM ndio chama namba moja Afrika"

Ameongeza "CCM ni chama kikubwa, kina mtaji wake wa Wananchi na wanachama, Wasanii ni sehemu ya ratiba ya Burudani lakini sio kigezo cha kujaza Watu katika Mikutano."

Soma https://jamii.app/MikutanoCCMWasanii

#JamiiForums #Democracy #Uwajibikaji #Accountability
Ni muhimu kwa anayehitaji kusajili laini yake kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anaweka alama ya kidole mara moja, na ikiwa ipo haja ya zoezi kurudiwa ni muhimu wakala akatoa hakikisho kwamba zoezi halilengi kuchukua alama ya kidole mara mbili

Ikiwa Kitambulisho chako kimetumika na wakala kusajilia laini za Watu wengine bila ridhaa na idhini yako fika katika dawati la Huduma kwa wateja la Mtandao husika ili kutoa taarifa itakayowezesha kufutwa kwa namba ambazo huzitambui

Ni muhimu kuchukua hatua hii ili kulinda Taarifa zako binafsi katika kitambulisho cha NIDA zisitumike vibaya kwenye matukio ya uhalifu

Mjadala zaidi https://jamii.app/UsirudieAlamaZaVidole

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
👍1
Chama cha ACT Wazalendo kimezungumzia madai ya kushikiliwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Paulo Kaheza, kwa kusema “Tunaitaka Serikali imuachie huru mara moja na bila masharti yoyote na iache nia ya kuwakamata viongozi wengine, badala yake iongezwe bajeti ya Serikali kutoa ajira takribani 65,000 kila mwaka.”

Aidha, Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi ameandika “Habari hii imenishangaza. Kwa hoja walizozitoa hazina ujinai wowote, iwapo kweli Kiongozi huyu amekamatwa, litakuwa ni shambulio dhidi ya Katiba na Uhuru wa Maoni.... Raia huyu aachiwe mara moja. Hoja zao (NETO) zinajibika na wana #Haki ya kupewa majawabu.”

Awali, ilidaiwa kuwa Kaheza alikamatwa akiwa nyumbani kwake Geita, Februari 24, 2025, JamiiForums imepiga simu ya Kamanda wa Polisi Geita mara kadhaa, imepokelewa na msaidizi wake ambaye mara zote amesisitiza Kamanda, Sofia Jongo yupo kwenye kikao

Soma https://jamii.app/GeitaPolisiFeb25

#JamiiForums #Governance #JFMatukio #CivilRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Paulo Kaheza ameachiwa kwa dhamana Februari 25, 2025 huku simu zake mbili zikishiliwa na Jeshi la Polisi

Taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imesema Joseph amehojiwa kuhusu NETO na makundi ya Mtandao wa kijamii wa WhatsApp yanayojulikana kwa jina la NETO

Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa THRDC iliwaagiza mawakili Benard Otieno na Vianey Mbuya kufuatilia dhamana ya Joseph katika kituo cha Polisi kati mjini Geita, ambapo baada ya kufika hawakumkuta na badala yake waliambiwa waende kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Geita ambaye ndio alikuwa anamshikilia Mwalimu Kaheza

Soma https://jamii.app/KiongoziNETOAachiwa

#JamiiForums #Governance #JFMatukio #CivilRights
1👍1
Mwanachama wa JamiiForums.com anaomba Ushauri wa kujua tatizo linalomkabili la kuchukiwa na Watu Kazini linasababishwa na nini?

Anasema kwa sasa yupo kwenye Kazi yake ya 4 na ameshachoka kutafuta Kazi mpya kila wakati hali hiyo inapojitokeza tena

Mjadala zaidi https://jamii.app/KuchukiwaKazini

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons
Katika kila Uchaguzi, tuna nafasi ya kufanya maamuzi yatakayobadili hatma yetu na vizazi vijavyo. Uongozi unaojengwa kwa rushwa na kununua kura hauleti maendeleo ya kweli bali huzalisha viongozi wanaoweka maslahi yao mbele, wakisahau mahitaji ya Wananchi.

Kiongozi bora huongoza kwa uadilifu, uwazi, na mipango thabiti ya kuleta mabadiliko chanya kwa jamii

Tusiruhusu pesa zipotoshe maamuzi yetu, tukemee vikali #Rushwa ya Uchaguzi

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Transparency
👍1
Je, kusifia kupita kiasi kunadhoofisha Uwajibikaji? Tunawezaje kusawazisha pongezi na ukosoaji ili viongozi wawajibike bila kuhisi wanashambuliwa?

Jiunge nasi kwenye mjadala huu wa kujadili dhana ya 'Uchawa' katika muktadha wa #Uwajibikaji na mustakabali wa Demokrasia yetu

Ni Alhamisi hii, Februari 27, 2025 kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku kupitia #Xspaces ya #JamiiForums

Kujiunga, bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

#UchawaNaUwajibikaji #MjadalaWazi #UwajibikajiKwanza
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala kuhusu ubora wa Miundombinu ya Afya ya Mnada wa Kibamba ambapo anasema Vyoo vinavyotumika si salama

Amehoji, Viongozi wa Afya wa Wilaya ya Ubungo wapo wapi? Hakuna viwango vya usalama wa Afya vinavyopaswa kuzingatiwa kabla ya eneo kuruhusiwa kutoa huduma za chakula?

Ametoa wito kwa mamlaka kushughulikia changamoto hiyo kabla ya kuibuka kwa mlipuko wa magonjwa

Soma https://jamii.app/MnadaWaMbuzi

#JamiiForums #PublicHealth #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Mdau anasema zoezi la kujiandikisha ili kupata Vitambulisho vya Taifa (#NIDA) lililofanyika Februari 24 na 25, 2025 katika Kata ya Nsololo Wilayani Uyui, limewavunja moyo wengi kwa kuwa kuna idadi kubwa ya Watu ambao hawajakamilisha mchakato huo

Anadai Watu waliojitokeza ni wengi, hivyo kukawa na uhaba wa vifaa, upungufu wa timu ya kuhudumia, misuguano ya hapa na pale na wengine kufikia hatua ya kupigana, pia wenye Mahitaji Maalum wakiwemo Walemavu, Wazee, Wajawazito na wenye Watoto Wadogi, hawakupewa kipaumbele

Mdau anaongeza baadhi ya Watu waliuziwa fomu za kujiandikisha kwa Tsh. 200, ikiwa ni gharama ya kutoa nakala (photocopy), anatoa wito mchakato huo urejeshwe na ikiwezekana waongeze Vituo kwani Watu wengi watakosa Vitambulisho

Soma https://jamii.app/NIDANsololo

#JamiiForums #JFMatukio