JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#ELIMU: Matokeo ya Mitihani ya Upimaji Kitaifa kwa Wanafunzi wa Darasa la 4 na Kidato cha Pili iliyofanyika Oktoba na Novemba 2023 yameonesha Wanafunzi 147,837 (8.73%) wa Darasa la 4 hawakufanya Mtihani. Wanafunzi 257,396 sawa na (16.66%) wamefeli kwa kupata Daraja E

Aidha, Wanafunzi 64,160 wa Kidato cha Pili sawa na (8.44%) hawakufanya Mtihani. Waliopata Daraja 0 ni 102,028 (14.69%). Ufaulu kwa Darasa la 4 ni 0.39% na Kidato cha Pili ni 0.62%

Zaidi, soma https://jamii.app/NECTAMiddle

#JamiiForums #Governance #JFHakiElimu #SocialJustice #Accontability #JFDATA #JFSC
👍52
DAR: Matukio mbalimbali wakati wa warsha iliyoandaliwa na JamiiAfrica, kuwakutanisha Wanahabari na Wadau wa Habari kupeana elimu kuhusu umuhimu wa kuripoti Habari na taarifa zenye maslahi ya Umma, lengo likiwa ni kuhamasisha Utawala Bora na Uwajibikaji

Warsha hiyo ya siku moja ilifanyika katika Hoteli ya Protea, Februari 19, 2025, ambapo Washiriki waliuliza maswali, kubadilishana uzoefu na kugusia ufahamu wao kuhusu lengo husika

Soma https://jamii.app/MbwaMtaani

#JamiiForums #JFMatukio #Accontability #FreedomOfExpression
MBEYA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Wakala wa Barabara Tanzania (#TANROADS) kushughulikia Matengenezo ya barabara ya Ibanda hadi Kyela Mjini, akidai kuwa baadhi ya sehemu zimeharibika na si salama kwa Watumiaji kutokana na mashimo mengi yaliyodumu kwa muda mrefu.

Anadai barabara hiyo imekuwa chanzo cha ajali na kuhoji kama Serikali itasubiri mpaka madhara makubwa yatokee ndipo iingilie kati.
  
Soma https://jamii.app/BarabaraIbandaKyela

#JamiiAfrica #JamiiForums #ServiceDelivery #Accontability