JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Wizara ya Mambo ya Nje imesema inaendelea kufuatilia suala la Mtanzania Juma Ally Maganga (45) kushikiliwa Nchini Sudani Kusini kwa tuhuma za kugonga Mtu na kusababisha kifo chake

Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga, amesema “Mkurugenzi Idara ya Afrika anafuatilia kwa karibu na Ubalozi wetu Kampala. Inavyoonekana kuna mwendelezo mzuri, wamefanikiwa kuwasiliana na utingo. Kwakuwa hatuna Ubalozi Sudan Kusini mawasiliano yamekuwa shida kidogo lakini nimeomba wakipata chochote watuambie.”

Naye, Mke wa Dereva, Rehema Godfrey Mongi, amesema “Tumepata taarifa kuwa yule aliyegongwa ameshazikwa na kinatarajiwa kufanyika kikao Jumatatu (Februari 24, 2025), kuna Watanzania ambao wapo kule pia wamekuwa wakisaidia Mawasiliano ya hapa na pale.”

Soma https://jamii.app/SudanKusiniAjali

#JFMatukio #JamiiForums #Diplomacy #JFDiplomasia
2
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 (Kifungu 60 (3)(b) na 60 (6)(a)), kutoa taarifa binafsi za Mtu mwingine kama namba ya Simu bila idhini ya mwenye namba ni kosa linaloweza kukugharimu Faini isiyopungua Tsh. laki moja na isiyozidi Tsh. milioni ishirini au kifungo kwa kipindi kisichozidi Miaka kumi au vyote kwa pamoja.

Tuambie Mdau, Mtu akitoa namba yako ya Simu kwa Mtu mwingine bila kukuomba ruhusa huwa unajisikiaje?

Soma https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #TaarifaZakoMaishaYako
👍1
MOROGORO: Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amemteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (#MORUWASA)

Awali alikuwa Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar (DAWASA) ambapo amechukua nafasi ya Mhandisi Tamimu Katakweba

Aidha, Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya Wataalamu watakaofanyia kazi changamoto za upatikanaji wa Maji Manispaa ya Morogoro na maeneo yote yanayohudumiwa na MORUWASA katika kipindi ambacho utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji unaendelea

Ikumbuke kwa nyakati tofauti kuanzia mwanzoni mwa Mwaka 2024 hadi 2025 Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wamekuwa wakidai kuna changamoto ya huduma ya Maji Morogoro na licha ya kulalamika bado hatua zimekuwa hazichukuliwi inavyotakiwa.

Soma https://jamii.app/MoroMajiHuduma

#HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #Accountability #JamiiForums
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ametoa wito kwa Viongozi wa Vijana waliojitambulisha kuwa ni "Non Employed Teachers Organisation (NETO)" kufika ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo baada ya Viongozi wa chama hicho kutoa mapendekezo 16 kwa Serikali ili kuipa hadhi Kada ya Ualimu hivi karibuni

Ameyasema hayo Februari 22, 2025 wakati alipotembelea na kukagua timu inayosimamia mchakato wa ajira za Ualimu, Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro

Amesema "Nimesoma makala yao yenye kichwa cha habari 'Ombi la wahitimu wa Ualimu vyuo mbalimbali Nchini kati ya Mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo."

Soma https://jamii.app/NETOWajeOfisini

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #Accountability
KIGOMA: Timu ya #Yanga imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara, baada ya kuichapa Mashuja FC Magoli 5-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, hivyo kufikisha alama 55, ikibaki kileleni katika msimamo kwa kucheza Michezo 21

Wafungaji wa Magoli ni Duke Abuya (31), Prince Dube (47), Khalid Aucho (54) na Clatous Chama (73, 83), upande wa Mashujaa FC ambayo ilikuwa nyumbani imesaliwa na pointi 23 katika Michezo 21

Timu inayoshika nafasi ya pili ni #Simba yenye alama 50 katika Michezo 19, ikifuatiwa na #AzamFC yenye pointi 43 katika Michezo 20

Soma https://jamii.app/MashujaaYanga

#JFSports #JamiiForums #LigiKuu25
1
Tabia ya kuwasifu Viongozi bila kuwawajibisha inaweza kuathiri vipi michakato ya Kisiasa na Uchaguzi huru na wa haki? Je, kuna njia za kukomesha hali hii?

Jiunge nasi kwenye XSpaces ya JamiiForums siku ya Alhamisi, Februari 27, kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku, katika Mjadala huu muhimu kuhusu Uwajibikaji

Washiriki watapata fursa ya kusikiliza, kutoa maoni au hata kuuliza maswali

Kujiunga Bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Kauli hii inaangazia ukosefu wa usawa katika Mfumo wa Haki Jinai, ambapo wale walio na Rasilimali za Kifedha mara nyingi hupata Mawakili Bora, dhamana na rufaa, huku Masikini wakikosa Uwakilishi mzuri wa Kisheria

Haki haipaswi kuwa kwa walio na uwezo pekee, ni Haki ya kila Mtu!

#HakiKwaWote #UsawaKisheria #HakiZaKiraia #JamiiForums #CivilRights #Demoracy #RightToFairTrial
1
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Uchaguzi ni fursa yako ya kuamua hatma ya Jamii yako, lakini #Rushwa ya Uchaguzi inahatarisha #Haki hiyo ya msingi

Kila unapokubali kuuza kura yako kwa pesa au ahadi za muda mfupi, unatoa ruhusa kwa Uongozi mbovu kushamiri, Huduma za Jamii kudorora, na maendeleo yako na ya Jamii yako kudumaa

Jiulize: Baada ya uchaguzi, wale waliotoa pesa watakuwa wapi? Je, watakumbuka shida zako? Usinunuliwe!

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Democracy #ServiceDelivery #Uwajibikaji
1
Haki haipaswi kupimwa kwa maneno ya wale walioko Madarakani, bali kwa hali halisi ya wale walioko pembezoni mwa Jamii

Watu Masikini, waliotengwa na wasio na sauti mara nyingi ndiyo huathirika zaidi na udhaifu wa Mifumo ya Haki. Ili kujua kama Haki inatendeka, ni lazima uwasikilize wale wanaoihitaji zaidi.

#HakiKwaWote #UsawaKisheria #HakiZaKiraia #JamiiForums #CivilRights #Demoracy #RightToFairTrial
DODOMA: Chuo Kikuu cha Dodoma (#UDOM) kimeeleza taarifa za Wanafunzi waliositishiwa masomo Chuoni hapo kwa tuhuma za kuchezea mfumo wa Matokeo ziliwahusu Wanafunzi 170, baada ya upelelezi Wanafunzi 121 walipatikana na hatia, kikao cha Seneti ya Chuo kikapitisha waondolewe masomoni (Discontinue)

UDOM imefafanua kuwa suala hilo la kuchezea mfumo wa Mwaka 2023/24, kati yao Wanafunzi 32 hawakufika kuhojiwa na Seneti, kesi za Wanafunzi 15 zinaendelea na uchunguzi zaidi, wawili wengine hawakukutwa na hatia

Taarifa hiyo imeeleza Dirisha la Rufaa kwa Mwanafunzi ambaye yupo nje ya muda wa taratibu zilizopo anaruhusiwa wakati wowote kuomba kukata rufaa na sio kweli kuwa wamezuiliwa kukata rufaa

Soma https://jamii.app/UDOMUfafanuzi

#JamiiForums #Accountability #Elimu #DigitalWorld
1
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 mhusika wa taarifa, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara

Aidha, mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Ally Hapi, ametoa wito kwa Vyombo vya Dola kuwachukulia hatua Watu wote wanaotaka kuharibu Uchaguzi Mkuu

Hapi amesema kauli za Mwenyekiti za CHADEMA na Viongozi wengine wa Chama hicho kuhusu kuzuia Uchaguzi Mkuu hazina hoja wala mashiko, bali ni dalili za kuwa Chama hicho hakijajiandaa na Uchaguzi Mkuu ujao

Mjadala zaidi https://jamii.app/HapiCDMUchaguzi

#JamiiForums #Uchaguzi2025 #Kuelekea2025 #HakiZaKiraia #Democracy #Siasa
DAR: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Kimara ametoa wito kwa Polisi kufanya Doria, baada ya kuibuka kwa Vibaka wakiwa na Bodaboda wanaovamia Watembea kwa miguu kwa Mapanga kisha kuwajeruhi na kuwaibia

JamiiForums imewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Jacob Twange kuhusu hoja hiyo, ambapo amesema “Hilo suala kwangu ni jipya, ndio nalisikia lakini kwa kuwa aliyezungumza ni Mwananchi na sisi Viongozi tupo kwaajili ya Wananchi, basi Saa mbili kutoka sasa, mimi pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi Ubungo tutaelekea hapo.”

Ameongeza “Tutaenda kuonana na Serikali za Mtaa kisha tutazungumza na Wananchi tusikie maoni yao kujua kinachoendelea, hiyo itatusaidia kujua tunachukua hatua zipi.”

Zaidi, soma https://jamii.app/WiziMapangaKimara

#JamiiForums #Governance #JFMatukio