MOROGORO: WATEJA WAPYA WA MAJI HAWAJAUNGANISHIWA HUDUMA KWA MIEZI 6
Mdau wa JamiiForums.com anadai baadhi ya wakazi wa Manispaa ya #Morogoro hawajapata huduma hiyo kwa miezi 6 iliyopita huku majibu wanayopewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kuwa hakuna Mita
Mkurugenzi Mtendaji wa #MORUWASA, Mhandisi Tamimu Katakweba amesema “Kweli hakuna Mita kwenye soko, kuna Mzabuni atatuletea Mita 2,000 mwezi mmoja kutoka sasa. Tunazohitaji ni Mita class C lakini zilizopo sokoni ni A na B ambazo hazifai.”
Soma https://jamii.app/MajiMoro
#JFHuduma #JFUwajibikaji23

👍3❤2
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Kata ya Lukobe, Morogoro anasema miradi mingi ya Barabara imetelekezwa, hakuna hata ukatabati wa kawaida hivyo hazipitiki kwa sababu zina mitaro na mashimo makubwa. Pia, ujenzi wa Mfereji wa kuzuia mafuriko kandokando ya Barabara kati ya Kwa Wagogo hadi Mgudeni umetelekezwa na sasa mifereji imegeuka mahandaki na mazalia ya Mbu
Ameeleza Mradi mwingine dhaifu ni wa Mamlaka ya Maji (#MORUWASA) ambapo Mamlaka hiyo imechimba Mitaro ya kupitisha Bomba za Maji kando kando ya mifereji (mahandaki) iliyotelekezwa na #TARURA na kwa pamoja wamevuruga hata njia za waenda kwa miguu hivyo kukatisha mawasiliano ya barabara kati ya Mgudeni na sehemu za jirani
Mdau amemuomba Rais Samia Suluhu aingilie kati na kuwajibisha Viongozi wao waliolala
Soma https://jamii.app/ChangamotoMorogoro
#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Governance

❤1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewataka Watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (#MORUWASA) kutobaki Ofisini badala yake waingie mtaani kushughulikia changamoto za Wananchi wanaolalamikia huduma
Amesema “Watu walikosa Huduma ya Maji kwa wiki tatu Morogoro, nikapata taarifa, nikamuuliza Mtendaji, anachoeleza ni tofauti. Unamwambia nenda Mafiga na Tumbaku, wakafanya marekebisho na Wananchi wakapata maji, huo ni uzembe, mambo kama hayo hatuwezi kukubali.”
Waziri Aweso amefanya ziara ikiwa ni siku chache tangu Mdau wa JamiiForums.com alipolalamikia juu ya Huduma ya #MORUWASA, akisema Wananchi wanateseka kwa kutopata huduma ya maji na kumwomba Waziri afanye ziara kujionea kinachoendelea
Soma https://jamii.app/MajiMoroAweso
#ServiceDelivery #JFUwajibikaji #JamiiForums

👍3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi, Meneja wa usambazaji Maji, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (#MORUWASA), Mhandisi Thomas Ngulika, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo
Waziri Aweso amefanya maamuzi hayo Julai 23, 2024 alipofanya ziara
Ikumbukwe Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakilalamikia kukosekana kwa Huduma ya Maji Mkoani hapo na kutoridhishwa na utendaji wa Mamlaka hiyo
Soma https://jamii.app/MenejaMORUWASA
#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #ServiceDelivery #Governance #JFuwajibikaji #KeroYaMaji

👍5
Wadau wa JamiiForums.com walivyotoa maoni na malalamiko kuhusu Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (#MORUWASA) kwa nyakati tofauti hadi hatua ya Waziri wa Maji, Waziri Aweso kufika eneo la tukio na kuanza kuchukua hatua
Soma https://jamii.app/MenejaMORUWASA
#JFHuduma #Accountability #ServiceDelivery #Governance #JFuwajibikaji #KeroYaMaji #JamiiForums

MOROGORO: Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amemteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (#MORUWASA)
Awali alikuwa Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar (DAWASA) ambapo amechukua nafasi ya Mhandisi Tamimu Katakweba
Aidha, Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya Wataalamu watakaofanyia kazi changamoto za upatikanaji wa Maji Manispaa ya Morogoro na maeneo yote yanayohudumiwa na MORUWASA katika kipindi ambacho utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji unaendelea
Ikumbuke kwa nyakati tofauti kuanzia mwanzoni mwa Mwaka 2024 hadi 2025 Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wamekuwa wakidai kuna changamoto ya huduma ya Maji Morogoro na licha ya kulalamika bado hatua zimekuwa hazichukuliwi inavyotakiwa.
Soma https://jamii.app/MoroMajiHuduma
#HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #Accountability #JamiiForums

👍1