Je, tabia ya 'uchawa' inachangia vipi kuzorota kwa Uwajibikaji nchini? Ni kwa namna gani tunaweza kujenga Jamii inayowataka Viongozi wawajibike badala ya kuwasifu hata pale wanapokosea au kutimiza majukumu yao?
Kufahamu haya na mengine, tafadhali jiunge nasi katika Mjadala muhimu wa Uwajibikaji kupitia Xspaces ya JamiiForums, Alhamisi ya Feb. 27, kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku
Washiriki watapata fursa ya kusikiliza, kutoa maoni au hata kuuliza maswali
Kujiunga Bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Akizungumza na Wananchi wa Lushoto, Rais Samia Suluhu Hassan, amemwambia Mbunge wa Bumbuli, January Makamba "Sisi wamama mnatujua, ukimkera Mama anakupiga kofi, anakufichia Chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia Chakula, lakini leo namrudisha kwa Mama. Haya Mwanangu njoo"
Ameyasema hayo leo Februari 24, 2025 katika ziara yake Mkoani Tanga
Soma https://jamii.app/JanuaryRudiKwaMama
#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu2025

🕊1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wassira, amesema ana uzoefu wa kutosha kuweza kufanya majukumu anayotakiwa kwa wakati bila kujali umri alionao, ambapo kwa sasa ana umri wa Miaka 80
Amesema "Hakuna mshahara, kuna posho posho za kwenda Mbeya au Mwanza labda. Hizo unaweza ukaajiriwa wewe ukaishi?. Sisi chama chetu ni chama cha kujitolea. Wanaolipwa ni Watu wa Serikali."
Ameyasema hayo akiwa katika mahojiano kwenye kipindi cha #Morning Trumpet katika kituo cha Azam leo Februari 24, 2025
Soma https://jamii.app/KujitoleaVijanaWataweza

Ikitokea Chumbani/ndani ya Nyumba yako zikafungwa CCTV Kamera, ni mambo gani utakayopunguza kuyafanya?
Mjadala zaidi https://jamii.app/CCTNdaniKwako
#JamiiForums #JFStories #JFChitChats #Maisha

Kwa mujibu wa Kifungu cha 21 (1) cha Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini za Simu Mwaka 2025 ni kosa mtu kutumia Laini ya Simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine au kuruhusu laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho chake itumiwe na mtu mwingine
Ukiukwaji wa Kifungu hiki unaweza kusababisha adhabu ya kulipa faini isiyopungua Tsh. Milioni 3 au kifungo cha muda usipongua Miezi Sita au vyote kwa pamoja
Soma https://jamii.app/KosaKumsajiliaMtuLaini
#JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #JamiiForums #TaarifaZakoMaishaYako

TANGA: Akizungumza leo, Februari 24, 2025 na Wananchi wa Lushoto, Rais #SamiaSuluhuHassan amemuagiza Waziri wa Utalii aone uwezekano wa kupitia Kanuni za Fidia kwa wanaothiriwa na Wanyama kuvamia mashamba, na kusisitiza Serikali inaendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kuwazuia Wanyama kufanya uharibifu huo
Februari 11, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alishauri viwango vya fidia vipitiwe kwa madai haviendani na uharibifu, akitolea mfano Wakazi wa Ngara waliovamiwa na Tembo wa Hifadhi ya Burigi kuwa hawakusaidiwa na Sheria ya Wanyamapori, bali iliwaumiza zaidi
Soma https://jamii.app/MazaoFidiaNgara
#JamiiForums #Governance

Mshiriki wa Shindano la Stories Of Change 2023 akiongelea kuhusu athari za Udalali lwenye Soko la Ndani ya Nchi, alishauri kuwepo kwa Sheria na Vyombo vya kudhibiti Madalali kwasababu kuna muda huwa wanajihusisha kwenye Utapeli na wizi wa mali za wateja
Soma Andiko hili https://jamii.app/UdalaliShidaSOC23
#JamiiForums #SOC2023 #Governance #Economy #Middleman

DAR: Simba imepunguzwa kasi ya kuwania ubingwa wa #LigiKuu Bara baada ya kukubali sare ya Magoli 2-2 dhidi ya Azam FC, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa
Azam FC ilianza kufunga kupitia kwa Gibrill Sillah (1), Simba ikarejea kwa nguvu na kufunga kupitia kwa Elie Mpanzu (26) na Abdulrazack Hamza (76), wakati Wanasimba wakiamini ushindi ni wao, Zidane Sereri akaifungia Azam FC dakika ya 88
Simba imefikisha alama 51 ikibaki nafasi ya Pili nyuma ya Yanga yenye alama 55, Azam ikibaki nafasi ya Tatu kwa kuwa na pointi 44 katika michezo 21
Soma https://jamii.app/SimbaAzamFCFeb24
#JFSports #JamiiFiorums #JFLigiKuu25

DEMOKRASIA: Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, imesema Halmashauri Kuu ya Chama hicho imekutana kwenye kikao chake cha kawaida Februari 23, 2025 katika Makao Makuu ya Chama kuazimia maazimio 8
Miongoni mwa Maazimio hayo ni Chama kujiridhisha kuwa maridhiano yaliyoahidiwa na Rais #SamiaHassan yamesambaratika na falsafa yake ya 4R imeota mbawa, hivyo kumtaka ajitathmini juu ya tofauti ya ahadi zake kukosekana kwa vitendo na ajiulize “Yanapojengwa mazingira ya ahadi za Rais kutoaminika, Wananchi wamuamini nani?”
Aidha, Halmashauri Kuu ya Chama hicho imeelekeza kijikite kupigania maboresho ya mfumo wa Uchaguzi nchini ikiwemo mabadiliko madogo ya Katiba, kuundwa kwa Tume Huru za Uchaguzi (NEC na ZEC) na kupinga kwa nguvu zote kura ya mapema kwa upande wa Zanzibar
Soma https://jamii.app/ACTFeb24
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 mhusika wa taarifa, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara
Aidha, mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha
Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022
#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako