JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mwanasiasa Dkt. Willbroad Slaa (76) anayekabiliwa na kesi Namba 993/2025 akituhumiwa kusambaza taarifa za uongo kwenye Mtandao wa X, hajafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Machi 4, 2025

Hata hivyo baada ya kuona Dkt. Slaa hajafikishwa Mahakamani, Mawakili wa upande wa utetezi kupitia Melikior Sanga wameeleza ni haki yake kuwepo Mahakamani wakati shauri lake linatajwa

Zimepita Siku 40 tangu Dkt. Slaa alipotiwa kizuizini na kufunguliwa kesi hiyo akidaiwa kutenda kosa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya Mwaka 2015

Soma https://jamii.app/SlaaFeb19

#JamiiForums #JFMatukio
LINDI: Timu ya #Simba imepata ushindi wa Magoli 3-0 dhidi ya #NamungoFC katika mchezo wa #LigiKuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, wafungaji wakiwa ni Jean Ahoua (45, 72) na Steven Mukwala (90+2)

Matokeo hayo yanaifanya Simba ifikikishe alama 50 katika michezo 19 ikiwa nafasi ya 2, nyuma ya #Yanga yenye pointi 52 katika michezo 20. Namungo FC yenyewe imesaliwa na alama 21 ikiwa na michezo 20 na ipo nafasi ya 12

Soma https://jamii.app/NamungoFCSimba

#JamiiForums #JFSports
Baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yanatarajiwa kuathirika kwa kukosa Umeme kwa nyakati tofauti kati ya Februari 22 hadi 28, 2025 kutokana na maboresho ambayo yatafanywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa maboresho yatafanyika katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo kilichopo Dar katika tarehe tajwa yakilenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake kufuatia ongezeko la mahitaji ya matumizi ya Umeme

Imeeleza hali hiyo imesababisha Kituo hicho kuzidiwa na hivyo kulazimu kufungwa kwa Mashineumba (Transformer) mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji ya maeneo tajwa.

Soma https://jamii.app/UmemeTangazoFeb19


#JFHuduma #ServiceDelivery #JamiiForums #Accountability
πŸ‘2❀1
Miongoni mwa Athari za Rushwa kwenye Uchaguzi ni Huduma mbovu za Afya, Elimu duni, Miundombinu mibovu, kukosekana kwa Maji safi na Ukosefu wa Ajira, hivyo Chagua kwa hekima

Viongozi wanaonunua kura hawajali maslahi yako. Wanatafuta nafasi ya kurudisha pesa walizotumia kwa njia zisizo halali, huku Wananchi wakiendelea kuteseka

Kataa Rushwa kwenye Uchaguzi ili kuhakikisha tunapata Viongozi wanaojali Maendeleo ya Taifa letu

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
πŸ‘1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema baadhi ya Wanachama na Viongozi wanaotaka kugombea wameanza kupitisha fomu ili watangazwe kuwa wagombea pekee na kupita bila kupingwa

Amesema hayo Februari 19, 2025 wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo kwa Makatibu wa matawi na kata Wilaya ya Dodoma

Soma https://jamii.app/HakunaMgombeaKupingwa

#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Kuelekea2025
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 inatoa Haki mbalimbali kwa mmiliki wa taarifa binafsi ili kuhakikisha faragha na ulinzi wa taarifa zake.

Soma https://jamii.app/HakiMhusikaTaarifaBinafsi

#JamiiForums #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Jeshi la Polisi limedhibiti maandamano ya Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Februari 19, 2025 katika Wilaya ya Ilemela na Nyamagana

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafugwa, amesema maandamano hayo hayakuwa na uhalali wa kisheria na Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua Mtu au kikundi cha Watu watakaoandamana kinyume na sheria

CHADEMA Kanda ya Victoria walikusudia kufanya Maandamano ya Amani kwenda kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, yakihusu kutoweka kwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo.

Soma https://jamii.app/MaandamanoCHADEMAKupigwaMarufuku

#JamiiForums #Demokrasia #HumanRights #Democracy
πŸ‘1
Unamshauri nini mdau huyu wa JamiiForums.com anayefikiria kumshtaki Mama wa Mtoto wake kwa kutowatumia pesa ya Matumizi licha ya kuwa na kazi?

Mjadala https://jamii.app/MatumiziYaMtoto

#JamiiForums #LifeStyle #Maisha #LifeLessons
SONGWE: Uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umesema uvamizi wa Hifadhi za Barabara unaofanywa na Wafanyabiashara wadogo (Machinga) na upitishaji wa Mifugo kwenye Barabara unachangia uharibifu wa Miundombinu hiyo na kuhatarisha Usalama wa Vyombo vya Usafiri, Abiria na Wananchi kwa ujumla

Meneja wa #TANROADS Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga, amebainisha maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Mlowo Wilayani Mbozi, pamoja na Mpemba na Tunduma Wilayani Momba

Ameeleza kuondoa hali hiyo TANROADS inaendelea kutoa Elimu kwa Wadau mbalimbali kupitia mikutano na semina, pamoja na kushirikiana na Viongozi wa ngazi tofauti ili kuwajulisha Jamii madhara yanayojitokeza

Soma https://jamii.app/TANROADSSongwe

#JFMatukio #ServiceDelivery #JamiiForums
#MICHEZO: Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Wakili Simon Patrick, ameandika β€œUkweli usiofichika ni kwamba Yanga na Simba zimekuwa kubwa na zenye nguvu kuliko Mamlaka za Soka Nchini. Wasimamizi wa Soka letu wako tayari kuzibeba hizi timu ili kuwafurahisha Watu kuliko kutenda Haki.”

Ameongeza β€œKadri muda unavyosonga, Ligi inayoitwa ya nne kwa ubora Afrika inazidi kuwa Ligi ya vituko kiasi kwamba inakuwa aibu kuisifia mbele ya Watu wenye Akili. Waamuzi wa Namungo 0-3 Simba (Februari 19, 2025) wamechezesha kwa maelekezo mpaka wao wameona aibu kwa vituko walivyofanya.”

Mdau una maoni gani kuhusu mtazamo huu?

Soma https://jamii.app/WaamuziLigiKuu

#JFSports #JamiiForums #KemeaRushwa2025 #Accountability
Mdau wa JamiiForums.com anasema hawaelewi watu wanaosema kujenga nyumba na kuzika pesa badala ya fursa ya uwekezaji wenye faida kubwa baadae

Amehoji, hivi Mtu aliyejenga Nyumba #Kariakoo Miaka ya 1970 kwa Tsh. laki 1 halafu amekuja kuiuza Mwaka 2021 kwa Tsh. Bilioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?

Vipi mdau, upi mtazamo wako?

Mjadala https://jamii.app/GharamaKujenga

#JamiiForums #LifeTips #LifeStyle #JFChitChats
πŸ‘1