JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Baada ya video kusambaa katika Mitandao ya kijamii ikionesha Wananchi wakivuka kwa miguu kwa madai wamevunja geti la Daraja la Magufuli, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ametoa ufafanuzi wa tukio hilo

Akizungumza na JamiiForums, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amesema “Hawajavunja geti, ilikuwa Jumapili (Januari 26, 2025) baada ya vivuko kusimama kutoa huduma kutokana na changamoto ya uwepo wa magugu.”

Ameongeza kuwa majani hayo yalikuwa mengi na kuweza kuathiri utendaji kazi wa vivuko hivyo Abiria wakafunguliwa geti na kupita njia ya darajani

Soma https://jamii.app/KivukoDarajaMagufuli

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability
Rushwa imekuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wa uchaguzi, hasa ndani ya Vyama vya Siasa. Hii si tu inavuruga mchakato wa Kidemokrasia, bali pia inazima ndoto na juhudi za Vijana ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika uongozi wa Vyama na Taifa kwa ujumla

Katika Mjadala kuhusu Rushwa na Uchaguzi, tutajadili changamoto wanazopitia Vijana wakemea Rushwa ndani ya Vyama pamoja na masuluhisho yake

Usikose kujiunga nasi leo Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki, bofya: https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Katika kuadhimisha Siku ya Faragha ya Taarifa Duniani, Lawyers Hub kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali akiwemo JamiiForums wameandaa Mjadala wa Sera za Akili Mnemba (AI) kuanzia Saa 8:00 Mchana hadi Saa 10:00 Jioni, leo Januari 28, 2025

Wadau watajadili kuhusu faragha na usimamizi wa teknolojia za AI, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo masuala ya AI, Ulinzi wa Taarifa na Haki za kidijitali ni muhimu wakiwa na lengo la kuhamasisha uelewa wa athari za AI katika faragha Barani Afrika

Kushiriki bofya https://jamii.app/DialogueDataPrivacy

#JamiiForums #LawyersHub #ArtificialIntelligence #AI #AkiliMnemba
👍2
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka husika kushughulikia changamoto ya Mtandao wa Polisi wa kuangalia Faini za Magari na madeni ya Leseni haraka, akidai usumbufu umekuwa mkubwa tangu mfumo huo ulipoanza kugoma kutoa mrejesho kwa Watumiaji Desemba 2024 mpaka wakati huu

Soma https://jamii.app/PoliceTMSHaifanyiKazi

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #DigitalWorld
Siku ya Faragha ya Taarifa huadhimishwa Januari 28 kila mwaka ikiangazia kuongeza uelewa kuhusu masuala ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kuhimiza Sera na Kanuni Bora za kulinda taarifa za Watu katika Ulimwengu wa Kidigitali

Pia, siku hii inalenga kuwawezesha Watu kufanya maamuzi sahihi ya kulinda taarifa zao na kushinikiza maboresho ya Sheria za Faragha

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Chukua Udhibiti wa Taarifa Zako" ikilenga ikiwakumbusha Watu kufanya maamuzi sahihi kuhusu taarifa zao

Soma https://jamii.app/DataPrivacyDay

#JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #DataPrivacyDay2025 #TakeControlofYourData
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Baadhi ya Wananchi wanaotakiwa kupisha Ujenzi wa Bandari Kavu eneo la Nandanga, Kata ya Mpemba, Halmashauri ya Mji wa Tunduma wamedai Ofisi ya Serikali ya Mtaa inashiriki kuandikisha Watu wasiohusika kwa lengo la kuwalipa fidia

Akijibu madai hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Elisha Msomba amesema “Tulitumia busara katika kuhakiki maeneo, hatukutaka kutumia Sheria Mtu alete nyaraka kwa sababu wengi wanamiliki mashamba.”

Upande wa Diwani wa Kata, Jimmy Mtawa amesema “Sijapata hayo malalamiko, Wananchi wafike ofisini kwangu tushughulikie malalamiko hayo”

Soma https://jamii.app/MpembaSongwe

#JFMatukio #JamiiForums
Ni kweli kuwa mazingira au uwepo wa #Rushwa umekuwa ukiathiri ushiriki wa Vijana wengi katika michakato ya Uchaguzi?

Unakaribishwa kushiriki kwa kuchangia na kusikiliza mjadala wa “Uwepo wa Rushwa Katika Uchaguzi: Je, Vijana Wanapata Nafasi ya Kushiriki Kuleta Mabadiliko?” ili pamoja tujadili na kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya Vyama vya Siasa na uchaguzi kwa jumla

Mjadala huu utafanyika kupitia #XSpaces ya JamiiForums, leo Jumanne Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku

Kushiriki, bofya: https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba ambao ndio Waratibu wa Mafunzo ya Walimu kuhusu Mitaala mipya ya Kidato cha Kwanza amesema “Mafunzo yanafanyika katika ngazi ya Shule. Hata hivyo, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu baina ya Walimu, Shule zaidi ya mbili zinaweza kukutana katika ngazi ya Kata au Tarafa."

Ameeleza utaratibu wa Washiriki kupatiwa chai pekee sio tu kwa ajili ya Arusha au Mwanza tu bali unafanyika hivyo kote Nchini na kuwa wamefanya hivyo katika Mikoa 23 na wanatarajia kukamilisha mchakato Januari 31, 2025."

Ufafanuzi huo umekuja baada ya Wadau wa JamiiForums.com kueleza Walimu washiriki wanapatiwa Tsh. 3,000 ya chai kwa siku na wengine hawapati kabisa hali ambayo iliwafanya baadhi yao wahoji kama huo ndio utaratibu

Soma https://jamii.app/TETPoshoMitaala

#JamiiForums #Governance
1👍1
Taasisi za Uwajibikaji zinashirikianaje na vijana katika kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji kwenye mchakato wa Uchaguzi?

Kufahamu hili na mengine, usikose kujiunga nasi katika Mjadala kuhusu Rushwa na Uchaguzi, Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki, bofya: https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
👍1
Mdau wa JamiiForums.com ameeleza umuhimu wa kuchana na kuharibu karatasi au tiketi zenye taarifa binafsi ili kujiepusha kuingia kwenye matatizo na kulinda usalama wako

Mdau, umeshawahi kushudia tukio lilitokea kutokana na matumizi mabaya ya taarifa zako binafasi, ilikuwaje?

Soma https://jamii.app/UtunzajiTaarifaBinafsi

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #JFUwajibikaji #Accountability
👍1