JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” upo hewani muda huu leo Januari 28, 2025

Shiriki kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji kwenye mchakato wa Uchaguzi kwa kuchangia katika jadala ambao unafanyika kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki bofya https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akizungumza katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta Mabadiliko?” Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ACT Wazalendo), Rahma Mwita amesema Sheria ya Rushwa ipo lakini kiuhalisia vitu vinavyotokea kwenye uhalisia ni tofauti, kuna mambo mengi yanaibuliwa kila siku na hakuna kinachofanyika

Ameongeza kwa kusema hali hiyo inafanya Watu wengine waanze kukata tamaa ya kutokuwa na Moyo wa Ushiriki katika Uchaguzi

Amesema “Suala la kuona Mtu anatoa Rushwa na kisha anafanikiwa ni jambo la kawaida na hiyo inakatisha tamaa au inawavunja Moyo Vijana. Ni kama tumeamua kuweka tick kwenye boksi lakini kiuhalisia ni tofauti”

Zaidi https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ACT Wazalendo), Rahma Mwita, amesema “Wakati mwingine wanaotoa Rushwa ni Vijana. Mimi ni Kijana na nipo kwenye ngome ya Vijana, kuna wengine unawasikia wanasema wametoa kiasi fulani cha Pesa kupata nafasi za Uongozi”

Ameongeza kuwa “Maisha yetu yalivyo tumeifanya Rushwa kuwa sehemu ya Maisha, hiyo ni kwasababu Watu waliopita nyuma yetu walikuwa wanafanya hivyo vitendo na ndio maana hata Vijana wa sasa wanaona bora waendeleze kilekile walichokikuta”

Amesema itafikia hatua Watu wataanza kujichukulia Sheria mkononi kutokana na Mazingira ya Rushwa yanayoendelea na kusababisha upendeleo kwa upande fulani

Zaidi https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala, Mwanachama wa CHADEMA, John Pambalu amesema “Sijawahi kuona TAKUKURU imeshughulika na Rushwa za kwenye Siasa licha ya kuwa tunashuhudia mara kadhaa matuo ya aina hiyo”

Amesema moja ya changamoto ya Rushwa ni kuwa aliyepokea na aliyetoa wote wanataka ndio maana wakati mwingine inakuwa na ugumu kufuatilia

Ameongeza kuwa “Sheria ya gharama za Uchaguzi ipo kama nadharia, hakuna njia ya kuiwezesha Mamlaka kukukamata kwa kuwa wewe mhusika unajua jinsi ya kujikadiria, unajaza fomu mwenyewe bila Mtu kukusimamia”

Zaidi https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia Mjadala, Mwanachama wa CHADEMA, John Pambalu amesema “Rushwa katika Uchaguzi ni jambo pana, sio pesa peke yake. Mfano kuwasafirisha, kuwashika Wajumbe na kuwahudumia mambo mengine pamoja na kuwapa ahadi mbalimbali (vyeo) kama utashinda Uchaguzi nayo ni sehemu ya Rushwa”

Ameongeza kuwa Mtu mmoja akifanya vitu pasipokuwa na makubaliano na vikao wakati wa Uchaguzi akilenga kuwapa ‘favor’ wajumbe hiyo nayo ni Rushwa

Zaidi https://x.com/i/spaces/1gqGvNNlpeeGB

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akizungumza katika Mjadala, Entesh Melaisho (TWAWEZA) amesema sheria zilizopo kuhusu Rushwa ni kama zimekuwa na faida kwa makundi fulani ya Watu, ndio maana inaonekana kuna aina ya Watu fulani au kundi fulani hawaguswi na Sheria hizo

Ameongeza kuwa “Sheria kuhusu Rushwa zipo na zinafahamika kwa wachache, hazifuatwi na kwa maana hiyo imekuwa ni hali ya kawaida”

Amesema mbali na kutafuta mbinu za kudhibiti wajumbe kwenye chaguzi lakini pia sisi wenyewe tunatakiwa kubadilika na kutambua kuwa Rushwa ni mbaya na itatupoteza

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” Christina Kapama (WAJIBU), amesema “Tuna Sheria kuhusu Rushwa lakini zinakosa Meno, hazioneshi namna gani changamoto za kifedha zinazowakuta Vijana zinaweza kutumika kuwasaidia kushiriki kwenye Chaguzi bila Rushwa kuhusika”

Akitolea mfano Taasisi za TWAWEZA na JamiiForums amesema ni Taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mafunzo kwa nia ya kutoa Elimu kuhusu Uwajibikaji na kujitambua kwa Vijana lakini changamoto inayotokea ni kuwa washiriki wanakuwa hawapo tayari hadi wanapoona kuna ahadi ya kitu fulani watapata watakaposhiriki

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” Entesh Melaisho (TWAWEZA), amesema “ili kuzuia Rushwa, AZAKI zinaweza kusimamia na kupigia kelele uwepo wa Sheria bora ambazo zinaweza kutumika kupunguza au kuondoa Mazingira ya Rushwa”

Ameongeza kuwa “AZAKI zinaweza kutumika kutoa Elimu zaidi kuhusu suala la Uwajibikaji na Haki za Kiraia, kupitia Elimu hiyo Wananchi wanaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuwafanya Viongozi wawajibike na kutimiza majukumu yao hata kama wametoa Rushwa”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” Othman Chuma (Mdau), amesema Vijana wanatakiwa kuwa na chombo cha Baraza la Taifa kwa ajili ya kuwakilisha Vijana na kuwasemea, chombo hicho kitasaidia kutoa Elimu ya kupambana na Rushwa

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” Musa D. Njoghomi (Mdau), amesema Rushwa imekuwa changamoto kubwa na kuwatia Vijana hofu ya kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi

Amesema “Ili tuweze kuwavutia Vijana waweze kushiriki, tunatakiwa kuwa na njia ya kudhibiti Rushwa, jambo gumu ni kuwa katika suala la Rushwa mtoaji na mpokeaji wote wanakuwa wanufaika ndio maana yule wa pembeni (Kijana) kwake inakuwa ngumu kufanikiwa”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Akichangia katika Mjadala wa “Uwepo wa Rushwa katika Uchaguzi: Je, Vijana wanapata nafasi ya kushiriki kuleta mabadiliko?” Stanslaus Lambart (Mdau) amesema “TAKUKURU wanapaswa kuonesha wanachukua hatua, inawezekana wanachukua hatua lakini Watu hawaoni kama wao wanatimiza hicho wanachotakiwa kukifanya”

Ameongeza kwa kusema tunapaswa kunyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe na kutoa elimu kuhusu athari za rushwa kwani watoa rushwa wana mbinu nyingi na wanazibadilisha kila siku

Amesisitiza kuwa rushwa inaendana na hali ya ubinafsi kwa kuwa unaona wewe unachokipata ndicho unachostahili hauwazi watu wengine, hilo pia linawakuta Vijana ambao wanashindwa kuwaza watu wengine au kuwaza kesho

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
1👍1
Akichangia katika Mjadala, Aristodi Furia (Mdau) amesema Rushwa huwa inaanzia ngazi ya Familia, mara nyingi Vijana wanapokuwa wadogo, wanakua wakiangalia kile kinachofanywa na Wazazi, Walezi au wakubwa wao

Ameongeza kuwa Vyombo ambavyo vinadhibiti Rushwa vinatakiwa kuboreshwa na kupewa nguvu kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Taifa, bila kufanya hivyo tukitegemea ngazi ya Taifa huku chini kunakuwa kunaoza

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaVijana #Demokrasia #MaoniYaDemokrasia #Governance #Uwajibikaji #KemeaRushwa
Kuwa mtu mwenye mtazamo chanya kwa kutumia maneno yako kwa busara ili kuleta faraja, kujenga mahusiano mazuri na kuhamasisha watu wengine katika kuwajenga

Nguvu ya maneno ni kubwa usiwe mtu wa kukatisha tamaa, kuharibu na kuletea wengine maumivu

#JamiiForums #MorningQuote #AmkaNaJF #LifeLessons #LifeTips #Maisha
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anashauri Mamlaka zinazohusika kusimamia Kampuni za Uzoaji Taka ili zizingatie usalama wa Afya wa Wafanyakazi wao kwa kuwa wengi hawajaliwi na inachukuliwa kama ni jambo la kawaida wao kutokuwa na vifaa vinavyohitajika

Jambo lingine analodai ni hatari ni kitendo cha vijana wanaozoa taka kukaa juu ya gari la Taka wakiwa hawana dhana zozote za kujikinga na harufu, au upepo unaorusha Taka wakati Gari likiwa kwenye mwendo

Anahoji Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) mko wapi? Hamuoni hayo yanayoendelea?

Soma https://jamii.app/UzoajiTakaDar

#Accountability #JamiiForums #Governance #PublicHealth
Je, Mfumo wetu wa Uchaguzi unahimiza Uwajibikaji na Uadilifu wa Viongozi?

Tunapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, ni muhimu kuchambua changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho kwa pamoja

Usikose kujiunga nasi kwenye mjadala huu kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza na kuchangia maoni kuhusu mustakabali wa Demokrasia yetu

Kushiriki Bofya https://jamii.app/MjadalaUchaguziJAN30

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Mdau, unaponunua Nguo mpya huwa unaifua kabla ya kuivaa au unavaa kwanza kisha kufua baadaye?

Tembelea Mjadala huu uliopo JamiiForums.com ndani ya Jukwaa la Urembo, Mitindo na Utanashati au bofya https://jamii.app/KufuaNguoMpya

#JamiiForums #JFStories #JFChitChats #LifeStyle