JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UEFA 2022/23: GUARDIOLA KOCHA BORA, HAALAND MCHEZAJI BORA

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha bora kwa timu za Wanaume kwa msimu uliopita baada ya kuiwezesha timu yake kutwaa Ubingwa

Aidha, Mshambuliaji wa timu hiyo, Erling Haaland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume kwa msimu uliopita. Alikuwa Mfungaji Bora akiwa na Magoli 12

#JamiiForums #UCLDraw #UCL
πŸ‘10❀3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
WAZIRI WA FEDHA: DOLA SIO HELA YETU, MATUMIZI YAMEKUWA MAKUBWA KULIKO BIDHAA TUNAZOUZA NJE

Akifafanua kuhusu kuadimika kwa Dola ya Kimarekani Nchini Tanzania, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema njia zinazotumika kupatikana kwa fedha hizo Nchini kuwa ni kupitia Mikopo, Misaada au Mauzo ya Nje huku akisisitiza Dola si fedha inayotengenezwa nchini
-
Amesema β€œMatumizi yetu ya Dola yamekuwa makubwa kuliko bidhaa Tunazouza Nje, Mitambo na Vifaa vingi tunayojengea Bwawa la Mwalimu Nyerere na Reli vinanunuliwa kwa Dola, hata Deni la Nje pia linalipwa kwa Dola, hivyo hakuna usawa kati ya vitu vinavyotuletea Dola na matumizi tunayoyatumia.”

Vipi Mdau, una maoni gani kuhusu kauli ya Waziri wa Fedha?

Soma https://jamii.app/MwiguluUfafanuzi

#Governance #Uchumi #EconomyCrisis #Diplomacy #JamiiForums
πŸ‘Ž11πŸ‘4❀3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Benki Kuu ya Tanzania ilitoa Dola za Marekani na kuingiza kwenye mzunguko Mwaka 2011/12 wakati wa Mdororo wa Kiuchumi Duniani kisha ikatoa tena Mwaka 2022 kutokana na athari za #COVID19

Amesisitiza Tanzania ina akiba ya Dola za Marekani Bilioni 5.2 ambayo inaweza kutumika kwa Miezi 4.5 na ambayo haiwezi kutolewa yote kwa kuwa kuna ukame wa Fedha hizo sehemu nyingi

Soma https://jamii.app/MwiguluUfafanuzi

#Governance #Uchumi #Diplomacy #JamiiForums
πŸ‘9❀6πŸ‘Ž1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS SAMIA: MABADILIKO SI ADHABU, MLIOTEULIWA MTULIE, MTUMIKIE WATU

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati akiwaapisha Viongozi Wateule Ikulu dogo ya Tunguu, Zanzibar, Septemba Mosi, 2023 ambapo amesisitiza β€œSisi ni Watumishi wa Watu, mahusiano ni jambo zuri sana. Ukijipandisha unataka kukaribia Mbinguni hautatumikia Watu, upole si ujinga"

Soma https://jamii.app/UapishoTunguu

#Governance #JamiiForums
❀5πŸ‘2πŸ‘Ž2
Kumwekea Mtoto ahadi ya Ndoa kabla ya Kuzaliwa kunamnyima Fursa za kujifunza na Kujenga Maisha Bora

#JamiiForums #JFWomen #GenderEquality #ChildRights #HumanRights #HakiMtoto
πŸ‘3πŸ‘Ž3❀2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
NAIBU WAZIRI: MWANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI AKISTAAFU ANAPATA KIASI KIKUBWA KULIKO ALICHOCHANGIA

Naibu Waziri amesema hivyo baada Mbunge Sophia Mwakagenda kuhoji Mifuko ya Hifadhi ya Kijamii inapotumia Fedha za Wachangiaji kufanya uwekezaji na biashara, je, Wachangiaji wananufaikaje na wanapata nafasi ya kujua faida inayopatikana?

Je, unadhani kipi kiboreshwe katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kumnufaisha Mwanachama?

Soma https://jamii.app/BungeSept1

#Governance #JamiiForums
πŸ‘5πŸ‘Ž1
Kuuza au kuchakata taarifa binafsi kinyume na madhumuni ya awali ya ukusanyaji wa taarifa hizo ni uvunjifu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Kwa mfano, Kampuni ya simu A kuuza au kutoa namba ya simu kwa kampuni B kwa madhumuni ya kutuma matangazo ya biashara au michezo ya kubeti ni kosa linaloweza pelekea kampuni zote mbili kulipa faini isiyopungua millioni moja na isiyozidi bilioni tano

Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 60 (1) (4) na 60 (6) (b)

#JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #JamiiForums
πŸ‘9
LINDI: Watumishi wa Chama cha Ushirika wa Masoko ya Kilimo (AMCOS) ambao ni Said Akili Mtureni, Karani wa Tawi la Naungo 'A' Nanjirinji na Afai Rajab Mbwani Karani wa Tawi la Mawelenje, Nanjirinji wamefikishwa Mahakamani kwa Makosa 2 ya Wizi na Kughushi Saini

Kosa la kwanza ni kuiba Ufuta uliopelekwa na Wakulima kwenye Matawi yao, Said Akili Mtureni anadaiwa kuiba (Kilogramu 1,250, Thamani ya Tsh. 3,016,250) na Afai Rajab Mbwani (Kilogramu 2,005, Thamani ya Tshs. 4,838,065).

Kosa la pili ni kughushi Saini ya Mjumbe wa Bodi katika Matawi yao ili Stakabadhi za Mazao zioneshe Ufuta ulipokelewa. Washitakiwa wameshindwa kukamilisha masharti ya dhamana na hivyo wamerudishwa Mahabusu

Soma https://jamii.app/AMCOSLindi

#JamiiForums #Governance #KemeaRushwa #JFUwajibikaji23 #SerikaliBilaRushwa
πŸ‘10
Mila ya kumwekea Mtoto ahadi ya Ndoa kabla hajazaliwa ni ukiukwaji wa #HakiZaBinadamu kwa Mtoto ambaye anapaswa kuzaliwa na uhuru wa kuamua Maisha yake ya baadaye

Kumnyima Mtoto uwezo wa kuchagua mwelekeo wa Maisha ya baadaye humzuia kupanga na kutimiza ndoto zake, hivyo kumweka katika mzunguko wa Umasikini na utegemezi

Soma https://jamii.app/AhadiZaNdoaKablaYaKuzaliwa

#JamiiForums #HakiMtoto #JFWomen #JFToons #HumanRights #Governance #WomenRights #ChildRights
πŸ‘7πŸ‘Ž1
TABORA: Mahakama ya Wilaya ya Tabora imemwachia huru Denis Kantanga, (Aliwahi kuwa Askari Polisi nafasi ya Konstebo) aliyeshtakiwa kwa makosa 2 ya Kuomba na Kupokea Rushwa ya Tsh. 18,000,000 ili amsaidie Mtuhumiwa wa Kesi ya Mauaji

Mahakama ilimhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili Jela au kulipa faini ya Tsh. 500,000 kwa kila kosa ambapo Mshitakiwa alilipa Faini ya makosa yote (Tsh. 1,000,000) na Kurejesha Tsh. Milioni 18 alizopokea kwa njia ya Rushwa

Vipi Mdau, una maoni gani kuhusu kiwango cha adhabu zinazotolewa katika Kesi za Rushwa?

Soma https://jamii.app/Ex-CopTBR

#JamiiForums #Governance #KemeaRushwa #JFUwajibikaji23 #SerikaliBilaRushwa
πŸ‘7
ZIMBABWE: Chama Kikuu cha Upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC), kimetangaza Maandamano kwa lengo la kushinikiza kufutwa Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa Ushindi Mgombea wa Chama Tawala, Rais #EmmersonMnangagwa

Maandamano yatafanyika katika Majimbo 10 huku CCC ikiwaomba Wanaharakati kusambaza ushahidi wa Udanganyifu uliofanyika. CCC ina Siku 7 za kuwasilisha Pingamizi la Matokeo Mahakamani ingawa Wachambuzi wanasema njia za Kisheria haziwezi kusaidia kwasababu ZANU-PF inadhibiti Mahakama

Soma https://jamii.app/CCCProtests

#JamiiForums #Democracy #SocialJustice #Governance #ZimbabweDecides
πŸ‘6❀2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jonathan Lee Riches, Binadamu mwenye rekodi ya kufungua kesi nyingi duniani. Alifanikiwa kufungua kesi takriban 2,600 katika Mahakama mbalimbali Duniani

#JamiiForums #FahamuZaidi #Entertainment
😁14πŸ‘1🀩1πŸ₯±1
DKT. SLAA AVULIWA HADHI YA UBALOZI

Rais Samia Suluhu Hassan amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Willibrod Slaa.

Dkt. Slaa aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Balozi, Novemba 23, 2017

Julai 21, 2023, Mdau kupitia mtandao wa JamiiForums.com alidokeza kuwa Dkt. Slaa angekamatwa na angevuliwa Ubalozi

Julai 22, 2023, Dkt. Slaa akiongea na wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam alinukuliwa akisema β€œNajua maneno hayo ni makali, nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini, najua ninachosimamiaβ€œ

Soma zaidi https://jamii.app/SlaaAvuliwaUbalozi

#JamiiForums #Governance #JFSiasa
πŸ‘18❀1
AFRIKA KUSINI: Afisa wa Ubalozi Mwandamizi wa Tanzania Nchini humo, Peter Shija amethibitisha Watanzania 5 wamefariki na wengine 3 wamelazwa Hospitali baada ya jengo walilokuwa wakiishi kuteketea kwa Moto

Imeelezwa kuwa Jengo hilo lililokuwa chini ya umiliki wa Jiji la Johannesburg, lilitelekezwa na kuanza kutumiwa Watu waliokosa makazi, wengi wao wakiwa Wahamiaji wasio na vibali

Kwa mujibu wa Afisa Ubalozi huyo, zaidi ya Watanzania 150 walikuwa wakiishi ndani ya Jengo hilo kabla ya kuteketea kwa moto ambao umesababisa vifo vya Watu zaidi ya 74.

Soma https://jamii.app/TZDiedInSA

#JamiiForums #Governance #JFMatukio
πŸ‘5😒4
GABON: Muungano wa Upinzani wa #Alternance2023, ambao unadai kuwa ni mshindi halali wa uchaguzi wa Agosti 26, unasema Jeshi halioneshi dalili za kurudisha madaraka kwa Serikali ya Kiraia, hivyo wametoa wito kwa Jumuiya za Kimataifa kuhimiza kurejeshwa kwa Utawala wa Kiraia

Hata hivyo Kiongozi wa Kijeshi Nchini humo, Jenerali #BriceOliguiNguema ameahidi kuirejesha nchi hiyo kwenye demokrasia, ambapo amesema Taasisi za Serikali nchini humo zitafanywa kuwa za kidemokrasia zaidi kwa kuwa Utawala wa Kijeshi ni "kwa muda tu"

Soma https://jamii.app/JeshiUtawalaGabon

#JamiiForums #Demokrasia #Democracy #GabonCoup #Governance #AfricaMilitaryCoups
πŸ‘4❀1
MDAU: TABORA MJINI HALI TETE, PETROLI INAPATIKANA KWA TABU

Anadai kuna vituo vichache vinavyouza mafuta hayo yakiwa yanapatikana kwa tabu na hakuna maelezo kutoka kwenye Mamlaka zote juu ya changamoto husika

Anadai kuna taarifa baadhi ya Wafanyabiashara wanaficha mafuta kwa kuwa wiki ijayo Mamlaka ya Nishati na Maji (#EWURA) inatarajiwa kutangaza bei mpya ya mafuta, hivyo wanatarajia bei ikipanda watapata faida kubwa

Soma https://jamii.app/NishajiTabora

#JFHuduma #JFUwajibikaji23 #JamiiForums
πŸ‘2
KENYA: Mbunge wa Kisumu Mashariki, #ShakeelShabbir amelieleza Bunge kuwa amepokea Malalamiko ya Wananchi 5 waliodai kupata shida za Kiafya ikiwemo maumivu ya Macho kutokana na Usajili wa Mboni ya Jicho waliofanyiwa na Kampuni ya Sarafu Mtandao ya Worldcoin

Waziri wa Afya, #SusanNakhumicha amekiri Kifaa hicho hakikufanyiwa majaribio ya uchunguzi kabla ya kutumika na hivyo, waliopata matatizo watafute msaada wa matibabu

Ikumbukwe, Kampuni ya #Worldcoin inayojihusisha na Biashara ya Sarafu Mtandao (Cryptocurrency), inatuhumiwa kusajili Wateja wake kwa kuchukua Taarifa zao kupitia Mboni ya Jicho

Soma https://jamii.app/DataCoinKE

#JamiiForums #DataProtection #Governance #DataPrivacy #Accountability
πŸ‘6😁3
Je, ulikuwa upande gani kwenye Mdahalo huu shuleni? Tukumbushe 'points' zako

#JamiiForums #JFStories
πŸ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Amesema CCM ilikataa Mapendekezo yote ambayo kama yangefuatwa, #KatibaMpya ingepatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Ameeleza Mei 30 2023 CCM iliyakataa mapendekezo hayo kwa Maandishi, ambapo Mei 31, 2023, katika Mkutano wao wa Mwisho, #CHADEMA ilitoa msimamo wa Chama kuwa mazungumzo yataendelea endapo Rais Samia Suluhu atabadili msimamo wa Chama chake kwenye jambo hilo

Ameeleza baada ya hoja zao kukataliwa walikaa Kikao cha Kamati Kuu na Maazimio ya Kikao hicho yatatangazwa rasmi na Mwenyekiti wa Chama hicho, #FreemanMbowe

Ameongeza, "Maridhiano yalishakufa, wametukatalia, kwa hiyo sio suala la sisi kujitoa ni kwamba hoja zetu zote zimekataliwa, zote. Na uthibitisho ni kauli ya Waziri Ndumbaro ya juzi kwamba nyie watu mnahitaji kufundishwa Katiba ya sasa kwa Miaka 3 ndio tuanze mazungumzo ya Katiba Mpya. They are not interested"

Soma https://jamii.app/MaridhianoYamekufa

#Demokrasia #Democracy #Governance
πŸ‘10😨3