Baada ya Wadau kudai kupata mkanganyiko juu ya matumizi ya Nembo katika 'Podium' (Meza ya Kutolea Hotuba) ya Rais, huku baadhi wakidai alama ya ‘Bibi na Bwana’ imeondolewa, Msemaji wa Serikali ametolea ufafanuzi suala hilo
Kupitia Jukwaa la #JamiiCheck ndani ya JamiiForums.com, Gerson Msigwa anafafanua kuwa Podium yenye Pembe (ambayo haina Bibi na Bwana) ni Nembo ya Rais (Presidential Seal), inatumika kuonesha uwepo wa Rais, ile nyingine ni Nembo ya Serikali (Coat of Arms), Rais anaweza kuitumia kutambulisha yeye ndie Mkuu wa Serikali
Anaongeza kuwa kutokuwepo kwa nembo hizo hakuondoi Urais wake na hakuna Kanuni wala Sheria inayotoa mwongozo kwa Rais juu ya matumizi ya nembo hizo. Matumizi yanaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Itifaki kulingana na mazingira
Soma https://jamii.app/NemboYaTaifa
#Governance #JamiiForums

👍8❤2👎1
#MICHEZO: Timu ya Soka ya #Getafe ya #Spain imemsajili Mshambuliaji, #MasonGreenwood kutoka #ManchesterUnited kwa mkopo kwa Msimu mmoja
Greenwood alisimamishwa kucheza Ligi Kuu ya England (#EPL) tokea Januari 2022 kutokana na mashtaka mbalimbali yakiwemo jaribio la ubakaji na unyanyasaji wa kingono, ambapo mashtaka hayo yalifutwa mwezi Februari
Soma https://jamii.app/GreenwoodGetafe
#JamiiForums #JFSports

👍5❤1
MDAU: MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO KUTOPOKELEWA SHULE KISA HAJAMALIZA MICHANGO NI USUMBUFU
Anadai Mtoto wake ambaye amepangiwa kujiunga Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibaigwa Girls, Dodoma akitokea Mkoani #Mtwara amekataliwa na Mwalimu Mkuu na Makamu wake kwa kuwa Mzazi amelipa nusu ya Fedha za michango
Anaomba Wizara ya Elimu na Mamlaka zinazohusika ikiwemo TAMISEMI kuwasaidia Wazazi na Walezi wanaopata changamoto kama hiyo, akidai kuna gharama nyingine ambazo zinajitokeza kabla ya Mwanafunzi kufika kituo alichopangiwa, hivyo kupungukiwa Fedha sio jambo la ajabu
Soma https://jamii.app/MalalamikoShule
#JFMatukio #JFHakiElimu #Governance #JamiiForums

❤2👍2
Chelsea imeendelea kuwa na mwanzo wa kusuasua katika #PremierLeague 2023/24 baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Nottingham Forest kwenye Uwanja wa Stamford Bridge
-
Michezo minne ya ligi hiyo iliyopita, Chelsea imeshinda moja, sare moja na kupoteza mbili
-
Matokeo mengine ya ligi hiyo: Sheffield United 2-2 Everton, Brentford 2-2 AFC Bournemouth, Burnley 2-5 Tottenham Hotspur (Son Heung-min amefunga magoli matatu ‘hat trick’), Manchester City 5-1 Fulham (Erling Haaland amefunga hat trick)
-
#JFSports #JamiiForums

👍3❤1
Ratiba ya michuano hiyo imepangwa leo Septemba 2, 2023 ambapo #Simba inatarajiwa kuanza kwa kuikaribisha #AlAhly ya Misri, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa Oktoba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam
Michuano hiyo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (#CAF), pia inatambulika kwa jina la African Football League inashirikisha timu 8, inaanzia Hatua ya Robo Fainali ikiwa katika mfumo wa mtoano
Mechi nyingine za Robo Fainali; TP Mazembe vs Espérance Sportive de Tunis, Enyimba FC vs Wydad Athletic Club, Atlético Petróleos de Luanda vs Mamelodi Sundowns
Soma https://jamii.app/SuperLeague

👍10
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#JFDATA: Nchi za Afrika zimeendelea kukumbwa na Mapinduzi mfululizo ya Serikali na mengi kati yake yakifanywa na Vikosi vya Kijeshi ambavyo vimekuwa vikidai vinalenga kubadili Mifumo isiyoheshimu #UtawalaBora
Tangu Mwaka 1952 hadi 2023, kumekuwa na takriban matukio 216 ya Mapinduzi, 108 yalishindikana, 108 yamefanikiwa. Mataifa 45 kati ya 54 Barani Afrika yamepitia wastani wa jaribio moja la Mapinduzi tangu 1950
Katika kipindi cha miaka 3 (2021/23), Serikali za Nchi 7 (Chad, Mali, Guinea, Sudan, Burkina Faso, Niger na Gabon) zimepinduliwa na Majeshi
Unadhani nini hasa kinachochea Mapinduzi ya Serikali Barani Afrika?
Soma https://jamii.app/CoupDeTat
#JamiiForums #Governance #Democracy #Accountability

👍6
Wamiliki hao wa klabu hiyo ya #England wanatarajiwa kufuta mpango husika wakidai kuwa Wawekezaji hawajafikia kiwango cha bei ambacho wanakitaka ili kuiachia klabu, ambapo wao wanataka Pauni Bilioni 10 (Tsh. Trilioni 31.4)
Ikiwa uamuzi huo utafanyika unaweza kuibua hasira za baadhi ya mashabiki wa United ambao wamekuwa wakiamini Familia ya Glazer ni chanzo cha timu yao kutofanya vizuri kutokana na uwekezaji mbovu
Wawekezaji waliosalia kwenye mchakato wa kuinunua #ManchesterUnited ni Sheik Jassim wa Qatar na Sir Jim Ratcliffe wa Uingereza
Soma https://jamii.app/ManUNotForSale

👍3🤬2❤1🔥1
Stendi hiyo ya mizigo iliyopo Wilaya ya Bariadi, eneo la Nyaumata, ipo Kilometa 7 kutoka katikati ya Mji na inadaiwa iligharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 1 wakati wa ujenzi wake imekuwa haitumiwi na Wafanyabiashara
Mdau wa JamiiForums.com anayeishi jirani na eneo hilo anadai Wafanyabiashara hawataki kutumia Stendi hiyo kwa kuwa hakuna miundombinu ya kuwezesha usalama wa bidhaa hasa nyakati za mvua, hakuna sehemu ya kujikinga na jua, hakuna stoo na hakuna ulinzi wa uhakika
Mdau anauliza nani alipendekeza mradi huo na kwa nini Mamlaka zipo kimya?
Soma https://jamii.app/StendiBariadi
#JFHuduma #JFUwajibikaji23 #Governance #JamiiForums

❤3👍3
KENYA: Kiongozi wa Kamati ya Kitaifa ya Majadiliano, Kalonzo Musyoka amesema, kwasasa Upinzani Nchini humo unamtambua #WilliamRuto kama Rais baada ya kuonesha jitihada za kutafuta muafaka kati ya Serikali na upande wa Upinzani ukiongozwa na #RailaOdinga
Amesema Rais ameonesha ukomavu na msimamo wa Serikali kwa kuunga mkono mazungumzo yanayoendelea kwa pande mbili, licha ya upinzani kutoka kwa Naibu wake, #RigathiGachagua
Soma https://jamii.app/DialogueKE
#JamiiForums #Democracy #Governance #Accountability

👍5❤1🥰1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa sababu za Serikali ya Tanzania kukataa kutumia Mbegu za GMO (Genetically Modified Organism) akidai mbali na sababu za Kiafya, kuna Ubora na suala la umiliki
Amesema “Serikali ya #Tanzania hatutumii Mbegu za #GMO lakini kama Nchi haizuii utafiti unaohusu GMO. Kingine ni suala la kibiashara, nani anaimiliki na nani atafaidika siku ya mwisho?
Soma https://jamii.app/KilimoMkutano

👍13👏1
KENYA: Gavana wa #Meru, Kawira Mwangaza amewaacha Wananchi wa Kaunti hiyo katika hali ya mshangao baada ya kuipa barabara inayounganisha maeneo ya Kirung'a na Muthalankari jina la mumewe, Murega Baichu
Vyombo vya Habari nchini humo vimeripoti kuwa barabara hiyo inaelekea nyumbani kwa Baba mkwe wa Gavana huyo, hali iliyosababisha kushutumiwa kwa upendeleo na kutumia Rasilimali za Umma kujinufaisha yeye na ndugu zake wa karibu
Soma https://jamii.app/GavanaMeru
#JamiiForums #Governance #Nepotism

👍9❤1
Akizungumza kuhusu Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika utakofanyika Sept. 5-8, 2023, Waziri wa Kilimo, #HusseinBashe amekanusha taarifa zilizopo Mtaani kuwa Bei ya Zao la Vanilla ni Tsh. Milioni 1.5 kwa Kilo
Bashe amesema "Bei ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kilo ni uongo, nimesikia iliandikwa na Gazeti, ni vizuri kutochukua taarifa ambazo hazina uthibitisho. Kwahiyo bei ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kilo haipo duniani, bei ya Tsh. Laki 5 kwa kilo haipo duniani"
Ameongeza kuwa "#Vanilla ilipanda bei miaka miwili mitatu baada ya Madagascar kukumbwa na Vimbunga kwasababu wao ni Wazalishaji wakubwa, ikasaidia Wakulima wetu kupata bei nzuri"
Soma https://jamii.app/BasheVanilla
#JamiiForums #Governance

👍10😁2
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Kanali Mstaafu, Joseph Leon Simbakalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO)
Simbakalia ni Mhandisi wa Jeshi Mstaafu kutoka Kikosi cha Wahandisi wa Umeme na Mitambo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Amewahi kushika nyadhifa nyingine za juu kwa kuteuliwa na Rais katika Serikali zikiwemo Ukuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)
Soma https://jamii.app/NARCOCM
#JamiiForums #Governance #Accountability

👍3
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imechukua hatua hiyo kama Kanuni inavyoelekeza, kwa GBP Tabora kwa kutouza mafuta kwa siku 3 wakati kukiwa na akiba ya mafuta kwenye ghala
Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa baadhi ya Wafanyabiashara wanaficha Petroli na Dizeli Mkoani humo wakati wakisubiri #EWURA itangaze bei mpya ambayo inadaiwa itakuwa kubwa na itawapa faida kubwa
Taarifa ya EWURA Tabora imeeleza kuwa baada ya kukifungia kituo hicho, hatua inayofuata ni kutakiwa kueleza sababu za kutouza mafuta na baada ya hapo Mamlaka itatoa maamuzi kama itakifungulia au kutoa adhabu kwa kituo hicho
Soma https://jamii.app/NishajiTabora
#JFHuduma #JFUwajibikaji23 #JamiiForums

👍7❤2
Goli la Martin Odegaard na mawili ya ‘jioni’ kutoka kwa Declan Rice na Gabriel Jesus yameiwezesha Arsenal kupata ushindi huo kwenye Uwanja wa Emirates katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali
Man. United ndio iliyoanza kupata goli kupitia kwa Marcus Rashford katika mchezo ambao Mwamuzi alitumia Refa Msaidizi wa Video (VAR) kubatilisha penati kwa Arsenal na goli lililofungwa na Man. United kipindi cha pili

👍8❤5🔥2😁2
UTEUZI: RAIS ATEUA NAIBU MWANASHERIA MKUU, KATIBU MKUU NA NAIBU MAMBO YA NJE
Rais Samia amemteua Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Dkt. Evaristo Longopa aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu
Pia, Rais amemteua Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje anayeshughulikia Mambo ya Afrika Mashariki
Aidha, Balozi Said Shaibu Mussa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Fatma Rajab aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania - Qatar

👍4
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama za Rufani Nchini. Walioteuliwa ni, Jaji Lameck Michael Mlacha ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu #Kigoma na Jaji Paul Joel Ngwembe aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu #Morogoro
-
Pia, Rais amewateua Jaji Mustafa Kambona Ismail aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu, #DaresSalaam na Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, #Zanzibar
-
#JamiiForums #Governance
-
Pia, Rais amewateua Jaji Mustafa Kambona Ismail aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu, #DaresSalaam na Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, #Zanzibar
-
#JamiiForums #Governance
👍6
UTEUZI: Walioteuliwa ni aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa, aliyekuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani-DSM, Wilbert Martin Chuma na aliyekuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Sharmillah Said Sarwat
-
Pia, Arnold John Kirekiano, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Martha Boniface Mpaze, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Jumuishi katika Masuala ya Mirathi na Familia-DSM na Ferdinand Hilali Kiwonde, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu
-
Vilevile, Said Rashid Ding' ohi aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Iringa, Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania-DSM, Sarah Duncan Mwaipopo aliyekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali-DSM na Ntuli Lutengano Mwakahesya aliyekuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu-Dodoma

👍7
Mila ya kumwekea Mtoto ahadi ya ndoa tangu akiwa tumboni inaimarisha wazo kwamba Wanawake hawawezi kufanya maamuzi binafsi na wanapaswa tu kufuata maagizo na mwongozo wa Mwanaume
Aidha, Wanawake waliofungwa na Mila hii wananyimwa fursa za Elimu, kujitegemea Kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Kijamii, hivyo kusababisha kudorora kwa Maendeleo ya Jamii nzima
Taarifa zaidi https://jamii.app/AhadiZaNdoaKablaYaKuzaliwa
#JamiiForums #ChildRights #ChildProtection #WomenRights #JFWomen #HumanRights #HakiZaBinadamu #HakiMtoto

👍2
Winga #JadonSancho amedai sio kweli kuwa amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwenye Kikosi cha #ManchesterUnited kwa sababu hajaonesha kiwango kizuri kama kocha wake, Erik ten Hag alivyonukuliwa, bali hivyo ni visingizio dhidi yake
Kabla ya kufungwa magoli 3-1 dhidi ya #Arsenal, Ten Hag alisema Sancho hajaonesha kiwango kizuri mazoezini ndio maana hakuwepo katika mipango yake
Baada ya mchezo huo, Sancho (23) akasema "Nimeonesha bidii mazoezini wiki hii, naamini kuna sababu nyingine ambazo siwezi kuzizungumza. Nimekuwa 'mbuzi wa kafara' kwa muda mrefu, sio haki."
Soma https://jamii.app/SanchoTenHag

👍6🥰2😁2