JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Katika mafunzo ya #UlinziWaData yaliyofanywa kwa wanahabari mbalimbali katika Ofisi za JamiiForums, waliweza kujengewa uelewa wa umuhimu kwa #Tanzania kuwa na Sheria na Mwongozo wa Ulinzi wa Taarifa binafsi za Watanzania

#JFDataProtection #DigitalRights #JamiiForums
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NI NINI?

Ni mikakati na michakato ambayo unaweza kutumia ili kulinda Taarifa zako muhimu. Hii husaidia kuzuia kupoteza, kuibwa, kutumiwa vibaya au kuharibiwa kwa Taarifa

Mkakati wa kulinda Taarifa Binafsi ni muhimu hususan kwa Shirika linalokusanya, kushughulikia au kuhifadhi Taarifa ambazo ni nyeti

#JamiiForums #PersonalDataProtection #DataProtection #UlinziWaData
KUFANYA "BACK UP" NI NJIA MOJAWAPO YA KULINDA TAARIFA ZAKO

'Back up' ni hatua muhimu ya #UlinziWaData kwani humsaidia Mhusika kutunza taarifa zake muhimu ili akipoteza kifaa chake au kikiharibika aweze kuzipata taarifa hizo

Kuna majukwaa mengi yanayotoa huduma ya Backup kama Google Drive, One Drive, Team Drive, iCloud, SugarSync, MyPCBackup, Dropbox n.k

#JamiiForums #PersonalDataProtection #DigitalRights
NJIA UNAZOWEZA KUTUMIA ILI KULINDA TAARIFA ZAKO

Ni muhimu kuweka nywila(Password) kwenye vifaa vyako vya Kieletroniki. Hakikisha vifaa vyako pamoja na Mifumo yake na Programu Tumishi (Application) ziko 'Updated'

Pia, hakikisha unatumia Programu zilizothibishwa kuwa ni salama, tumia 'Anti-Virus' iliyoidhinishwa na epuka kufungua Kiunganishi (Link) usichokitambua

Fanya 'Setting' za Kiusalama kwenye Barua Pepe, Simu na Kompyuta yako

#DigitalRights #JamiiForums #DataProtection #UlinziWaData
NAMNA YA KULINDA NYWILA (PASSWORD) YAKO

1) Usitumie Nywila (Password) moja kwenye kurasa zako zote za Mitandao ya Kijamii. Hakikisha kila mtandao unatumia #Password yake

2) Hakikisha Nywila yako ina jumla ya herufi/alama zisizopungua 16 au na zaidi (Mfano: M1m1$%678abc@£+#)

3) Usitumie maneno ya kwenye Kamusi kama nywila yako. Na usiruhusu kivinjari chako (Web browsers mfano Chrome, Opera, Firefox, Brave n.k) kuhifadhi nywila yako

#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #UlinziWaData
SIFA ZA NYWILA (PASSWORD) DHAIFU

Inahusisha Jina la Mmiliki wa Akaunti, mfano: henrik19. Hutumia herufi au namba zilizo katika mtiririko kama vile ABCDEFG au QWERTY ambazo ziko kwenye 'Keyboard'

Inahusisha tarehe, Mwezi na Mwaka wa kuzaliwa, au namba nyingine kama za Kitambulisho, Mtihani, Bima ya Afya au Hati ya Kusafiria (Passport)

Soma - https://jamii.app/NywilaDhaifu
#UlinziWaData
ULINZI WA TAARIFA KATIKA BARUA PEPE (EMAIL SECURITY)

Unashauriwa kuchagua mtoa huduma anayetoa kipaumbele cha usalama kwenye barua pepe (tumia ProtonMail, Tutanota, Hushmail au Mailvelope kwenye Gmail)

Kifaa kinachotumika kufungua Emails pia lazima kiwe salama. Hakikisha Email yako inaweza kuchuja maudhui na kutambua 'Spam Emails'

Soma https://jamii.app/EmailSecurity
#UlinziWaData
NJIA ZA KUFUNGA KIOO CHA SIMU NA USALAMA WAKE (SCREEN LOCK) - 1

SLIDE TO UNLOCK: Hii ni njia rahisi na isiyoshauriwa kutumika kwasababu ni rahisi Mtu mwingine anaweza kufungua Simu yako

PIN CODE LOCK: Hizi ni namba zinazotumika kufunga screen ya simu yako. Ni njia kongwe zaidi ya ulinzi wa Simu

PATTERN LOCK: Njia hii imekuwa ikikosolewa sana na Wataalamu wa #UlinziWaKidigitali. Inaelezwa ni rahisi kwa mdukuzi kukariri mchoro ama 'pattern' zako.

Soma - https://jamii.app/ScreenLocks
#UlinziWaData
NJIA ZA KUFUNGA SIMU NA USALAMA WAKE (SCREEN LOCK) - 2

FINGER PRINT LOCK: Njia hii inahusisha matumizi ya alama za vidole vya mmiliki wa Simu. Njia hii ni bora ingawa Mdukuzi anaweza kujaribu vidole vya Mhusika akiwa kwenye hali ya kutojielewa

FACE ID LOCK: Teknolojia hii kwa kiasi kikubwa ilianza kutumiwa na Kampuni ya Apple. Hakuna ushahidi wa wazi kuhusu udukuzi unaoweza kufanywa dhidi ya 'Face ID'

PASSWORD LOCK: Hii ni njia rahisi na maarufu zaidi. Ni salama na inashauriwa zaidi ingawa mmiliki anapaswa kufuata vigezo vyote vya utengenezaji wa Nywila imara.

#JamiiForums #DigitalRights #UlinziWaData
HATUA ZA USALAMA WA BARUA PEPE

Password: Unashauriwa kutumia neno la siri imara na uliloliandaa kwa kufuata vigezo vyote muhimu

Wezesha Two Factor Authentication/Multifactor Authentication: Itakusaidia kujua jaribio la kuingilia barua pepe yako

#DataProtection #UlinziWaData
KENYA: Mahakama Kuu Nchini humo imesema uzinduzi wa Vitambulisho vya 'Huduma Namba' ulienda kinyume na Sheria ya #UlinziWaData ya Mwaka 2019

Vilevile, Serikali imelaumiwa kwa kutotathmini namna ambavyo Ulinzi wa Taarifa ungeathiriwa

Soma https://jamii.app/HudumaNambaKE

#DataProtection
ULINZI WA DATA: Wakati mwingine Taarifa hukusanywa kwa nia njema, lakini Changamoto ni kwamba wengi hawana namna ya kuzitunza

Kuwepo Sheria ya #UlinziWaData kutasaidia kufahamu uhifadhi na usalama wa taarifa hizo upoje

Soma - https://jamii.app/UtunzajiTaarifa

#DataProtection
MAMILIONI YA WATU HAWAJUI TAARIFA ZAO ZINAVYOTUMIKA

Uhitaji wa Ulinzi wa Faragha ya Taarifa Binafsi sio kitu kipya kwani Taarifa hizo zimekuwa hatarini

Kuwepo Sheria ya #UlinziWaData kutahakikisha Haki ya Faragha inasimamiwa

Soma - https://jamii.app/DPD2022

#DataPrivacyDay #DataPrivacy
👍1
Katika Ukusanyaji wa Taarifa/Data za Watu miongozo mbalimbali inapaswa kuzingatiwa ikiwemo kuwepo kwa Sheria ya #UlinziWaData

Mkusanyaji wa Data/Taarifa anapaswa kuzingatia Faragha/Usiri wa wenye Data na kutekeleza Ukusanyaji kwa njia iliyo halali

Ni vema Mkusanya Data awe na kusudi maalum na lengo la kuendeleza ukusanyaji huo

Soma - https://jamii.app/UkusanyajiData

#DataProtection #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI: Haki ya Faragha ipo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 16. Kuwepo kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha kutahakikisha Haki hii inasimamiwa

Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira amesisitiza kuharakishwa kwa Sheria ili kulinda Taarifa Binafsi za watanzania ambazo zinaendelea kukusanywa

#JamiiForums #DataProtection #UlinziwaData #DataPrivacy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
USALAMA WA TAARIFA BINAFSI: Mbunge wa Viti Maalum, Judith Kapinga amesisitiza umuhimu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi akisema, ni hatari kutokuwa nayo ikizingatiwa baadhi ya Kampuni huuza Taarifa Binafsi za Wateja

Amesema, "Simu zinabeba ulinzi wa Fedha zetu, na maisha yetu ya kila siku. Tusipokuwa na Ulinzi wa Taarifa zetu, ni jambo ambalo kidogo linahatarisha"

#DataProtection #UlinziWaData #DataPrivacy
JF YAENDESHA SEMINA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NA FARAGHA KWA WABUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson jana (Juni 27, 2022) alishiriki Semina ya Umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha za Watanzania iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Jijini Dodoma

Spika ameipongeza JamiiForums na wadau wake (TLS, LHRC, Twaweza, CIPESA, Paradigm Initiative) na Wadau wengine walioshiriki kuandaa Muswada wa Mfano (Model Bill) unaolenga Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha za Wananchi

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaData #DataPrivacy
👍17
Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo akiendesha Semina ya Umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha kwa Wabunge alisisitiza umuhimu wa kuwa na Sheria rafiki na shirikishi itakayolinda Utu wa Mtanzania na kuweka mazingira rafiki kwa Uwekezaji Nchini

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaData #DataPrivacy
👍27🔥3
Sehemu za kupata Huduma ya Intaneti kwa Jamii (Internet Café) huwa na kompyuta zinazotumiwa na Watu wengi, kila mmoja akiwa na hitaji lake, hivyo anayetumia kifaa hicho anaweka taarifa zake kulingana na hitaji binafsi

Ili kulinda taarifa zako (Kama jina na mitandao uliyotembelea) na kuzuia watu kukudukua kutokana na taarifa ulizotumia hapo, ni muhimu kutoka kwenye akaunti zako zote (logout) na kufuta historia ya kila ulichofanya

Zaidi soma https://jamii.app/MtandaoJumuiya

#JamiiForums #DataProtection #DataPrivacy #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaData #JFSC
👍2