JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NAMNA YA KULINDA NYWILA (PASSWORD) YAKO

1) Usitumie Nywila (Password) moja kwenye kurasa zako zote za Mitandao ya Kijamii. Hakikisha kila mtandao unatumia #Password yake

2) Hakikisha Nywila yako ina jumla ya herufi/alama zisizopungua 16 au na zaidi (Mfano: M1m1$%678abc@£+#)

3) Usitumie maneno ya kwenye Kamusi kama nywila yako. Na usiruhusu kivinjari chako (Web browsers mfano Chrome, Opera, Firefox, Brave n.k) kuhifadhi nywila yako

#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #UlinziWaData
TAARIFA ZAKO ZITABAKI SALAMA IKIWA UTAPOTEZA SIMU?

Kupoteza simu ni hatari zaidi ikiwa Wahalifu watapata njia ya kufikia Taarifa zako Binafsi ikiwemo zile za Kifedha

Unashauriwa kuwa na #Password (Nywila) imara ili kuwa salama zaidi

Soma https://jamii.app/DigitaliSalama

#JFDigitali
👍3
ZINGATIA YAFUATAYO KUIMARISHA ULINZI WA TAARIFA ZAKO

1) Funga Akaunti zisizo na Matumizi: Akaunti zisizotumika na kusimamiwa ipasavyo Mitandaoni bado zinaweza kuwa na #TaarifaBinafsi ambazo zinaweza kutumiwa vibaya

2) Weka Nywila (#Password): Fanya hivi katika Vifaa vyako vya Kidigitali ili kuimarisha Usalama wako. Kumbuka kuwa na Nywila Imara

Soma https://jamii.app/DPD23

#DataPrivacy #HakiYaFaragha
👍9
Ni mara ngapi umesikia Mtu amefunguliwa Akaunti katika Mtandao wa Kijamii au Majukwaa ya Kidigitali na Ndugu au Rafiki wa karibu?

Nywila (#Password) ni utambulisho binafsi ambao hulinda Taarifa zote katika ulimwengu wako wa kidigitali

Soma https://jamii.app/NywilaMtandaoni

#DataPrivacy
Unapotoa Nenosiri (#Password) kwa Rafiki, Mwenza au Ndugu wa karibu unadhoofisha Usalama wa Akaunti zako za Mitandao ya Kijamii na Majukwaa mengine ya Kidigitali

#JFDigitali #InternetSafety
Vipi mdau, una Password imara au na wewe upo kama mwamba hapa?

#Password imara husaidia kuongeza Ulinzi wa kifaa chako na kuepusha hatari ya kuibiwa Picha, Video, Nyaraka au Taarifa za Kibenki

#DataPrivacy #JFDigitali #JFToons
👍6
Ni rahisi kushawishika kutumia Nenosiri moja kwenye kila kitu; iwe Akaunti za Mitandao ya Kijamii, Baruapepe, Simu au Kompyuta

Ili kuwa na Ulinzi imara, epuka kutumia #Password moja kila mahali. Hii itasaidia kuwa salama katika Majukwaa mengine ikiwa Nenosiri la sehemu moja limejulikana

#JFDigitali
👍3
'PASSWORD' YAKO INAKUHAKIKISHIA ULINZI WA TAARIFA ZAKO MTANDAONI?

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya National Cyber Security Centre (NCSC) ya #Uingereza, Watu wengi wamekuwa wakitumia 'Password' (Nywila) ambazo ni rahisi kudukuliwa kwenye vifaa vyao vya Kielektroniki

#NCSC inashauri watu kutotumia 'Password' zenye Herufi au Tarakimu zinazofuatana au kufanana na badala yake watumie Mchanganyo wa Tarakimu, Herufi pamoja na Alama ili kuongeza #UlinziWaTaarifaBinafsi katika Vifaa wanavyotumia

Vipi Mdau, na wewe unatumia #Password' hatarishi zinazofanana na zilizotajwa hapo?
-
#JamiiForums #DigitalRights #DataProtection #DigitalSecurity #DataSecurity #JFDigitali
👍3
Nywila (#Password) mara nyingi hufananishwa na Mswaki kwasababu kama ambavyo hutakiwi kutumia Mswaki wako na Watu wengine ndivyo hivyohivyo unatakiwa kutunza Nywila zako

Kumshirikisha Mtu mwingine nywila yako ya Benki, Simu au akaunti za Mitandao ya Kijamii kunaweza kuhatarisha Usalama wako, sawa na kushiriki Mswaki kunavyoweza kuhatarisha Afya yako ya Kinywa

Kama vile unavyopaswa kubadili Mswaki kila baada ya Miezi michache, unapaswa pia kubadili nywila zako. Kutumia nywila moja kwa muda mrefu huongeza hatari ya Usalama wako Mtandaoni

Soma https://jamii.app/NywilaMswaki

#CybersecurityAwarenessMonth #JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #DigitalRights #JFDigitali #CyberCrime #StaySafeOnline