JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kuna wakati unakuwa na uhitaji wa Ushauri kuhusu Magari, Ndege, Meli, Pikipiki au masuala yoyote ya Ufundi Makenika?

Sehemu pekee yenye kila aina ya Ujuzi na Maarifa ni Jukwaa la #JFGereji ndani ya JamiiForums.com

Tembelea JF Gereji ili kujifunza na kushiriki Mijadala mbalimbali kuhusu eneo hilo.

Kufahamu zaidi, ingia hapa >> https://jamii.app/JFgereji

#JamiiForums #JFMaarifa #JFGereji #TechWorld
👍1
KENYA: Rais #WilliamRuto ameiagiza Wizara ya #TEHAMA na Uchumi wa Dijitali kuandaa Sheria itakayovutia Uwekezaji wenye Ushindani katika Masuala ya Kidijitali huku akieleza kuwa Serikali yake imeweka nia ya kutengeneza mazingira yatakayovutia Kampuni za Teknolojia kuwekeza zaidi Nchini humo

Kauli ya Ruto inakuja siku chache tangu aanze ziara ya siku 10 katika Mataifa ya #Marekani na #Uingereza ambako amefanya mazungumzo na baadhi ya Kampuni za Kiteknolojia zikiwemo #Starlink, #Apple, #Intel, #Google, na #Microsoft

Kupitia ziara hiyo, Bosi wa Apple, #TimCook aliahidi kuwa kampuni hiyo itaanza maandalizi ya kuwekeza katika Chuo cha Wanasidi Programu (Developers) huku Bosi wa Microsoft, #BradSmith akiielezea #Kenya kuwa kivutio cha Uwekezaji mkubwa wa Kampuni za Kimarekani

Soma https://jamii.app/RutoOnICT

#JamiiForums #DigitalRights #Innovations #Technology #TechWorld #Accountability #Governance
👍8🔥1👏1
#UGANDA: Rais #YoweriMuseveni ameridhia kutengwa Bajeti ya Tsh. Bilioni 332.5 kila mwaka kwa lengo la kusaidia na kukuza ubunifu wa Teknolojia pamoja na kufuta Kodi ya Bidhaa kwa Wabunifu Wapya ili kuwapa motisha wanaoingia kwenye Soko hilo

Kwa upande wake Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Dkt. Monica Musenero akizungumza katika Wiki ya Taifa ya Sayansi, amesema Serikali haiwezi kushindwa kuwekeza kwa Wabunifu japo kwa bajeti ndogo. Pia, ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuweka nguvu zaidi katika eneo la Ubunifu

Ikumbukwe hadi sasa, Uganda imefanikisha kuundwa kwa Magari yanayotumia Umeme (EV) yakiwemo Mabasi ya Abiria kutoka kiwanda cha #KiiraMotors kinachomilikiwa kwa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi

Soma https://jamii.app/Ubunifu

#JamiiForums #Governance #Innovation #JFDigitali #TechWorld
👍91
Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano huadhimishwa kila Alhamisi ya Nne ya Mwezi Aprili kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa Wasichana katika #ICT

Pia, siku hii hutumika katika kuhamasisha Wasichana na Wanawake wadogo kuchagua masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM)

Mtag Msichana au Mwanamke yeyote ambaye anasoma au yupo katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Soma https://jamii.app/GirlsInICT2024

#JamiiForums #TechWorld #WomenInTech #GirlsInICT #STEM #SikuYaWasichanaKatikaICT #JFWomen #JFDigitali
👍3
Mdau huyu kutoka Jukwaa la 'Tech, Gadgets & Science' ndani ya JamiiForums.com ameandika kuhusu namna alivyopata changamoto ya Mawasiliano na Kupata Taarifa alipotembelea Nchi ambayo imezuia baadhi ya Mitandao

Pia, ameshauri juu ya Teknolojia zinazoweza kukusaidia kufanya mawasiliano yako na kufikia taarifa mbalimbali unapokuwa katika maeneo ambayo Mitandao inazuiwa

Jifunze zaidi https://jamii.app/VPNized

#JamiiForums #DigitalRights #TechWorld #DigitalWorld #FreeSpeech #FreedomOfExpression #CivilRights
👍2
Siku ya Kimataifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu huadhimishwa Septemba 16 kila mwaka ili kuangazia umuhimu wa Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi (STI) katika nchi zinazoendelea ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo Umaskini, Ukosefu wa Usawa na Uendelevu wa Mazingira

Siku hii inasisitiza umuhimu wa 'STI' katika kukuza Maendeleo Endelevu na kuongeza Ubora wa Maisha kwa watu waliopo nchi za Kanda ya Kusini ambapo bado kuna ufikiaji mdogo wa Teknolojia ya hali ya juu na utafiti wa Kisayansi

Soma https://jamii.app/STIDay2024

#JamiiForums #Science #Innovation #Technology #SaveOurPlanet #STIAction #TechWorld
TEKNOLOJIA: Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Ubora wa Huduma (NICE) ya Uingereza imesema teknolojia ya Akili Mnemba (AI), itasaidia kuongeza Uhakika wa Majibu ya Vipimo vya X-Ray kwakuwa ina uwezo wa kuona Uvunjikaji wa Mifupa zaidi ya inavyoonekana kwenye X-Ray

Kwa mujibu wa NICE, kwa sasa, uwezekano wa X-Ray kutoona Mivunjiko mingine zaidi kwa Mgonjwa huwa ni kati ya asilimia 3 hadi 10 kwenye vipimo vya sasa na hivyo kuongeza muda wa uchunguzi au kutopatikana kwa tiba stahili kwenye majeraha

Imeelezwa kuwa, teknolojia ya AI kwenye Vipimo vya X-Ray itapunguza muda wa kusubiri majibu kutoka kwa wataalamu wa Maabara, pamoja na kuondoa makosa ya kibinadamu yanayojitokeza wakati wa kusoma vipimo

Soma https://jamii.app/AIonXRays

#JamiiForums #TechWorld #DigitalWorld #Innovations #EmbracingTechnology
👍31
UINGEREZA: Kampuni ya Apple inayozalisha Vifaa vya Kidigitali zikiwemo Simu za #iPhone, iPads na Laptop, imefunguliwa Kesi ya Madai ya takriban Tsh. Trilioni 10.19 ikidaiwa kulazimisha Wateja kutumia huduma za iCloud

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Kundi la Watumiaji Huduma liitwalo 'Which?' inaituhumu Apple kukiuka Sheria ya Ushindani kwa kuwataka Wateja kuhifadhi Data zao kama Picha au Video kwenye #iCloud na kulipia gharama wanapohitaji kuongeza nafasi ya uhifadhi au kupata data zao

Apple imekuwa ikitoa Hifadhi ya Mtandaoni (Cloud Storage Space) yenye ukubwa wa Gigabytes 5 (5GB) kwa wateja wa Vifaa vyake, lakini imeweka sharti la malipo ya takriban Tsh. 40,416 kwa nyongeza ya Gigabaiti 50 na Tsh. 2,245,308 kwa Terabaiti 12 kwa mwaka

Soma https://jamii.app/iCloudSued

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #TechWorld #SocialJustice
👍1
Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mtumishi wa Serikali, ameshauri yafanyike maboresho ya Mfumo wa Uhamisho wa Watumishi ili wanaotaka kubadilishana Vituo vya Kazi waruhusiwe kutuma maombi kwa kuzingatia Kada zinazofanana

Amesea utaratibu huo utasaidia kuongeza ari ya Watumishi kufanya kazi kwa ufanisi kwasababu watakuwa katika Vituo walivyochagua tena kwa kubadilishana na Watumishi wengine wanaofanya kazi zinazolingana.

Soma https://jamii.app/UhamishoKidigitali

#JamiiForums #Governance #Accountability #JFDigitali #Techworld