JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GEITA: Mdau ametoa wito kwa mamlaka kushughulikia utupaji ovyo wa taka kwenye Makazi ya Watu, Mtaa wa Ntengere, Kata ya Igulwa, Ushirombo ambao umegeuza eneo hilo kuwa 'dampo' akidai ni hatari kwa #Afya

Anashauri kuwepo na utaratibu maalum wa kudumu wa usimamizi wa taka, pia eneo hilo kurejeshwa kwenye matumizi yake ya awali kama Makazi au Ofisi za Umma

Zaidi soma https://jamii.app/DampoUshirombo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #JFMdau2025 #PublicHealth
Kuwa Mtu anayefikiri kwa uhuru, si kufuata tu kila kitu bila tafakari, fikra zako huru zinaweza kubadili Jamii au hali uliyonayo

Usikubali kila unachoambiwa bila kuchambua, usiamini kila taarifa au kauli bila kupima uhalisia wake

Uliza, chunguza, hakikisha unapata ukweli kabla ya kukubaliana

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Vyombo vya Habari ni sehemu muhimu kwenye Jamii yoyote iliyoelimika na kinachotakiwa ni kuziimarisha

Akizungumza na Wahariri, leo Julai 08, 2025, amesema “Tunatafakari namna tunavyoweza kuviimarisha kwa kuvilipa fedha zinazotokana na Kodi za Watanzania kwa sababu haiwezekani kuwa na Media ambayo hatujui hata vyanzo vyake vya fedha vinatoka wapi.”

Soma https://jamii.app/ProfesaMkumboMedia

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #DiraYaTaifa2025
MBEYA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Wakala wa Barabara Tanzania (#TANROADS) kushughulikia Matengenezo ya barabara ya Ibanda hadi Kyela Mjini, akidai kuwa baadhi ya sehemu zimeharibika na si salama kwa Watumiaji kutokana na mashimo mengi yaliyodumu kwa muda mrefu.

Anadai barabara hiyo imekuwa chanzo cha ajali na kuhoji kama Serikali itasubiri mpaka madhara makubwa yatokee ndipo iingilie kati.
  
Soma https://jamii.app/BarabaraIbandaKyela

#JamiiAfrica #JamiiForums #ServiceDelivery #Accontability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mchakato wa kupata Katiba mpya hauwezi kufanyika kwa urahisi ndani ya miezi mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025, akisisitiza kuwa "Si jambo jepesi asubuhi ukaamka Katiba ikawa imebadilika."

Ameyasema hayo leo Julai 8, 2025 katika kikao na Viongozi wa Dini, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)

Soma https://jamii.app/ChalamilaKatibaMpya

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Ruvuma: Kiongozi Mstaafu wa Chama cha #ACTWazalendo, Zitto Kabwe amesema "Wanaotaka tusishiriki Uchaguzi nawaona wamechanganyikiwa, ni heri tupeleke Wabunge wachache ili tukapambane ndani ya Bunge"

Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia Mjini Songea, Mkoani Ruvuma Julai 7, 2025 katika mwendelezo wa Operesheni ya Majimaji wakiwahamasisha Wananchi kulinda kura

Zaidi, soma https://jamii.app/ZittoUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema Maaskofu wanataka Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 uzingatie Haki za Wananchi kwa mujibu wa Katiba, akisisitiza kuwa “Uchaguzi usio na ushindani wa Vyama ambavyo vinashindana kwa Haki hauna maana, lazima Vyama vishindane"

Padri Kitima ameyasema hayo leo Julai 8, 2025, Dar es Salaam akiwa katika mahojiano na Jambo TV

Soma https://jamii.app/KitimaUchaguziWaHaki

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Akizungumza na Wajumbe wa #CCM Kata ya Kandawe, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax ametoa angalizo kwa Wana-CCM kuwa waangalifu dhidi ya Watu au makundi yenye nia ovu yanayoweza kuwa kichocheo cha vurugu

Dkt. Tax amesema "Tuhakikishe hakuna Mtu anayekuja kuvuruga amani ya kwetu, kuanzia chini na kupanda, unaweza kudharau ukasema hapa ni Kata lakini ina mchango Kiwilaya, Mkoa na Kitaifa."

Soma https://jamii.app/DktStergomenaKulindaAmani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Kuelekea2025 #Siasa
2
Mtu mwenye busara hategemei kuthaminiwa au kukubaliwa na wengine ili ajitambue au aendelee

Badala yake, ana uwezo wa kujikagua, kuona makosa yake mwenyewe na kujifunza kutoka kwayo

Anajua thamani yake haitegemei macho ya wengine bali ni kutoka kwake

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
1👍1
RUKWA: Jeshi la Polisi linamshikilia Samwel Kayoka (16), Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Mtenga kwa tuhuma za mauaji ya mdogo wake, Jackson Kayoka (14), baada ya kumpiga fimbo kichwani walipokuwa wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo.

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Shadrack Masija amesema tukio lilitokea Julai 7, 2025, Kijiji cha Mtenga 'A', Wilayani Nkasi ambapo kwa sasa uchunguzi unaendelea, na Samwel atafikishwa Mahakamani baada ya taratibu kukamilika.

Afisa Mtendaji wa Kijiji, Romwald Kapele amesema Watoto hao ni wa familia moja na kuwa walichokuwa wanafanya ni jambo la kawaida katika mazingira ya mila zao Watoto kucheza kwa kupigana kwa fimbo

Soma https://jamii.app/AmuuaMdogoWakeRukwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema uadilifu wa Uchaguzi umeshuka kwa kiwango kikubwa nchini, jambo linalotishia kuwepo kwa Uchaguzi ulio huru na wa haki.

Ameongeza kuwa Maaskofu hawajasema Watu wasiende kupiga kura, bali wanasisitiza Uchaguzi uwe wa haki, huru na unaoaminika.

Padri Kitima ameyasema hayo Julai 8, 2025 wakati akihojiwa na Jambo TV.

Soma https://jamii.app/UadlifuUmeshuka

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
DAR: Azam FC imefanikiwa kumsajili kipa #AishiManula kutoka Simba SC kwa mkataba wa Miaka mitatu, akiondoka Msimbazi baada ya nafasi yake ya kucheza kuwa finyu kutokana kuandamwa na majeraha pamoja uwepo wa Mousa Pinpin Camara.

Manula alijiunga na #SimbaSC Mwaka 2017 akitokea Azam FC, alionesha uwezo mkubwa ngazi ya klabu ya na Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kiasi cha kupewa jina la Tanzania One

Je, usajili wa Manula unaweza kuisaidia #AzamFC kutwaa mataji msimu ujao?

Soma Zaidi https://jamii.app/ManulaAzam

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica
Baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (#NECTA) kutangaza Matokeo ya Kidato cha 6, Wadau kutoka Jamiiforums.com wametoa shuhuda ya jinsi walivyopokea matokeo yao

Ulikuwa katika hali gani wakati unapokea matokeo yako ya Mtihani wa Taifa?

Soma https://jamii.app/MdauMatokeoForm6

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFElimu #JFChitChat #SwaliLaSiku
1
Wadau wa JamiiForums.com kwenye Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali wamemshauri mdau kuhusu biashara ya kufanya kwa mtaji wa Tsh. Milioni 30

Vipi mdau, ukiwa na kiasi hicho, ni Biashara gani ya kwanza utaifikiria?

Soma https://jamii.app/MtajiBiasharaMilioni30

#JamiiForums #JamiiAfrica #Biashara #Ujasiriamali #Uchumi
1