JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Klabu ya Simba inaongoza kwa 3-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho

- Goli la kwanza limefungwa na Gerson Fraga katika dakika ya 21

- Goli la pili limefungwa na Clatous Chama huku goli la tatu likifungwa na Josee Miquisson

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
SIMBA SC YAIADHIBU YANGA SC. YATINGA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Simba imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Yanga SC goli 4-1 katika mchezo wa nusu fainali

- Magoli ya Simba yamefungwa na Gerson Fraga, Clatous Chama, Luis Miquisson na Mzamiru Yassin huku goli la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Feitoto

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
FULL TIME: PLATEAU 0-1 SIMBA

> Klabu ya Simba imepata ushindi ugenini na sasa itahitaji sare ya aina yoyote kwenye mchezo wa nyumbani Desemba 5, mwaka huu ili kusonga mbele

#TotalCAFCL #CAFCL #SimbaSC #SSC #PlateauUnited #PlateauSimba #CAFChampionsLeague #CCL
#JFSports: CAF imeipiga faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 23 (USD 10,000) #SimbaSC kwa kufanya β€˜tambiko hatarishi’ katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates

- Maafisa wa mchezo wamesema Simba waliwasha moto katikati ya uwanja wakati wakijifanya kuomba kabla ya mechi

Soma https://jamii.app/SimbaSCFaini
SIMBA SC YAACHANA NA WAWA

- Pascal Wawa aliyeitumikia Simba kwa misimu minne, ataondoka klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa Juni 2022

- Wawa ni mchezaji wa 3 kuagwa na #SimbaSC baada ya Bernard Morrison na Rally Bwalya

Soma > https://jamii.app/WawaSimba

#JFSports
πŸ‘14
JUMA KASEJA ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWAKA HUU

Amewahi kuwa Mlinda Mlango wa Timu ya Taifa, #TaifaStars na #SimbaSC. Pia amezichezea Timu za #MoroUnited, #Yanga, #MbeyaCity, #KageraSugar na KMC

Hivi sasa ni Mkufunzi wa Taifa Stars na #NgorongoroHeroes

Soma https://jamii.app/KasejaKustaafu

#JFSports
πŸ‘18πŸ‘Ž1πŸ”₯1
CAF: SIMBA SC 7-0 HOROYA AC

Ushindi huo umeifanya #SimbaSC kufikisha pointi 9 na kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiungana na #RajaCasablanca katika Kundi C

Magoli yamefungwa na #ClatousChama (matatu), #JeanBaleke (mawili) na #SadioKanoute (mawili)

Soma https://jamii.app/SimbaHoroya

#JFSports #CAFCL
πŸ”₯10πŸ‘3
ULIMBOKA MWAKINGWE AFUNGIWA MAISHA KWA KOSA LA KUPANGA MATOKEO

TFF imewafungia kujihusisha na mpira Mwenyekiti wa #KitayosceFC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship), Yusuph Kitumbo na kocha wa soka, #UlimbokaMwakingwe baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la upangaji wa matokeo katika mchezo wa Aprili 29, 2023 kati ya #FountainGateFC dhidi ya Kitayosce

Ulimboka ambaye ni mchezaji wa zamani wa #SimbaSC aliwahi kutuhumiwa kupeleka rushwa kwa kipa Shabani Kado wa #MtibwaSugar Mwaka 2011 wakati Kitumbo alifungiwa kwa tuhuma za kupanga matokeo ya Championship Mwaka 2016 baadaye akasamehewa

Je, Unadhani TFF kutoa adhabu bila kuikata pointi Kitayosce ni sahihi?

Soma https://jamii.app/UlimbokaBan

#KemeaRushwa #JFSports
πŸ‘3❀1
NGAO YA JAMII: ULIYEMTAKA KAJA, FAINALI NI YANGA Vs SIMBA

#SimbaSC imefanikiwa kwenda Fainali ya Ngao Ya Jamii kucheza dhidi ya #YangaSC baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa penati 4-2 kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya goli 0-0 baada ya dakika 90.

#SingidaFountainGate itakipiga na #AzamFC kupata mshindi wa 3. Mechi zote zitachezwa Agosti 13, 2023 katika Uwanja wa Mkwakwani Mkoani #Tanga

Soma https://jamii.app/Ngao23

#JFSports #NgaoYaJamii2023 #JamiiForums
πŸ‘4
LIGI KUU BARA: SIMBA YAIRARUA DODOMA JIJI 2 - 0

#SimbaSC imeendeleza rekodi yake nzuri kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga #DodomaJijiFC goli 2 - 0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi

Simba imefikisha alama 6 na kuongoza Ligi hiyo huku Dodoma Jiji ikiwa na alama 3 katika nafasi ya 7.

Fuatilia Kilichojiri https://jamii.app/SSCvsDJFC

#JamiiForums #JFSports #NBCPL
❀1
CAF: SIMBA YAINGIA HATUA YA MAKUNDI KWA SARE

#SimbaSC imepata matokeo ya goli 1-1 dhidi ya #PowerDynamos ya #Zambia kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, hivyo kuingia Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kwa faida ya goli la ugenini baada ya matokeo ya awali kuwa 2-2

Kwa kuwa #Yanga nayo imeingia hatua hiyo, timu hizo zimeandika historia kwa mara ya kwanza #Tanzania kuwa na timu mbili kwa wakati mmoja katika Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa

Soma https://jamii.app/SimbaCAF23

#JFSports #CAF #CAFCL #JamiiForums
πŸ‘10
#MICHEZO: Kocha wa zamani wa #Arsenal, #ArseneWenger na Mwamuzi Mstaafu wa #FIFA, #PierluigiCollina, ni miongoni mwa Wajumbe walioambatana na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, kwa ajili ya kushuhudia Mechi ya ufunguzi wa African Football League 2023

Mechi hiyo kati ya wenyeji #SimbaSC dhidi ya #AlAhly ya Misri inatarajiwa kuchezwa leo, Saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, maarufu #Lupaso

Soma https://jamii.app/WengerAtuaTz

#JamiiForums #JFSports #SimbaVsAlAhly #Football #Soccer
πŸ‘3
WATABIRI MPO?

Leo Desemba 2, 2023 ni siku ngumu kwa Watani wa Jadi, #SimbaSC watakuwa Ugenini wakikipiga Nchini Botswana dhidi ya Galaxy majira ya Saa 10 Jioni

Vilevile, #YangaFC wapo nyumbani, watakipiga kwenye Uwanja wa Mkapa Saa moja Usiku dhidi ya Al Ahly ya Misri, michezo yote ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi

Kwako Mdau unadhani Simba watachomoka Botswana au Yanga watawakalisha Vigogo wa Soka la Afrika?

Kwa taarifa, habari, makala na tetesi za Michezo tembelea Jukwaa la 'Sports' https://jamii.app/JFSports

#JamiiForums #JFSports #Michezo #Soka
πŸ‘2
CAFCL-ROBO FAINALI: YANGA SC vs MAMELODI, SIMBA SC vs AL AHLY FC

Klabu ya #YangaSC itakutana na Klabu ya #MamelodiSundowns kutoka Afrika Kusini kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika

Katika Droo iliyochezeshwa leo, Mtani wa Jadi wa Yanga, Klabu ya #SimbaSC imepangiwa kuvaana na Klabu ya #AlAhlyFC kutoka Misri

Aidha, Klabu ya TP Mazembe itakutana na Klabu ya AtlΓ©tico PetrΓ³leos huku Klabu ya ES Tunis ikikutana na ASEC Mimosas katika michezo mingine ya Robo Fainali

Zaidi soma https://jamii.app/Draw_QrtrCAFCL

#JFSports #CAFCL
❀7πŸ‘5
MNYAMA SIMBA AMTAFUNA AZAM FC, ATWAA KOMBE LA MUUNGANO 2024

Goli pekee lililofungwa na Babacar Sarr dakika ya 77 limeiwezesha #SimbaSC kutwaa Kombe la Muungano 2024 dhidi ya #AzamFC katika Fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, #Zanzibar

Simba ambayo imekuwa na msimu wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara 2023/24 na Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24, kabla ya mchezo huo iliitoa KVZ kwa magoli 2-0 wakati Azam FC iliifunga KMKM magoli 5-2

Baada ya mchezo huo, Kiungo wa Simba, Saidi Ntibazonkiza 'Saido' aliyeibuka mchezaji Bora wa Fainali, amesema mashabiki wao hawatakiwi kukata tamaa hata kama timu hiyo inapata matokeo mabaya kwa kuwa ni sehemu ya mchezo

Soma https://jamii.app/Muungano24

#JFSports #JamiiForums #MuunganoCup #MuunganoCup2024
πŸ‘7
Patrick Aussems, Kocha wa Zamani wa #SimbaSC alitoa kauli hiyo muda siku chache baada ya kuachana na klabu hiyo aliyoitumikia kuanzia Julai 2018 hadi Novemba 2019

#JFSports #JFNukuu #JamiiForums #JFGoodMorning #JFQuotes #JFNukuu #AmkaNaJF
πŸ‘3
#JFSPORTS: Klabu ya #SingidaBlackStars imesema Beki Israel Patrick Mwenda aliyesajiliwa kwa ada ya Tsh. Milioni 200, alilipwa Tsh. Milioni 140 kabla ya kusaini kwa mujibu wa Mkataba na kiasi kingine kilichobaki (Tsh. Milioni 60) kinatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili

Taarifa imeeleza zaidi kuwa Klabu itaendelea kufanyia kazi maslahi yake kwa mujibu wa makubaliano, huku Uongozi ukimtaka kuripoti kambini haraka kwaajili ya maandalizi ya ligi inayoendelea

Israel Mwenda alisajiliwa katika Msimu wa 2024/25 na Singida Black Stars akitokea kwa Wekundu wa Msimbazi, #SimbaSC

Soma https://jamii.app/SingidaBlackStars

#JamiiForums #Michezo #Sports
❀1πŸ‘1
DAR: Azam FC imefanikiwa kumsajili kipa #AishiManula kutoka Simba SC kwa mkataba wa Miaka mitatu, akiondoka Msimbazi baada ya nafasi yake ya kucheza kuwa finyu kutokana kuandamwa na majeraha pamoja uwepo wa Mousa Pinpin Camara.

Manula alijiunga na #SimbaSC Mwaka 2017 akitokea Azam FC, alionesha uwezo mkubwa ngazi ya klabu ya na Timu ya Taifa ya Tanzania β€œTaifa Stars” kiasi cha kupewa jina la Tanzania One

Je, usajili wa Manula unaweza kuisaidia #AzamFC kutwaa mataji msimu ujao?

Soma Zaidi https://jamii.app/ManulaAzam

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais wa Heshima wa #SimbaSC na mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji (Mo Dewji), kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kuwa tangu mwaka 2018 amechangia kiasi cha Tsh. bilioni 45 kwa ajili ya uendeshaji wa klabu, ikiwa ni pamoja na usajili, mishahara na maandalizi ya timu.

Aidha, aliongeza Tsh. bilioni 20 kwa ununuzi wa asilimia 49 ya hisa ndani ya klabu hiyo.

Amefafanua β€œMara nyingi nimekuwa nikitoa msaada nje ya mfumo rasmi, kila palipojitokeza uhitaji wa dharura kuanzia 2017 hadi 2024 nimetumia takribani bilioni 22 katika misaada ya dharura na hivyo kufanya jumla ya mchango wangu Simba kufikia Tsh. Bilioni 87. Hivyo kusema Mo hatoi hela ni kauli ya kupotosha yenye mwelekeo wa chuki”.

Mo amewataka wadau wa Simba kuacha fitina, badala yake washirikiane kuijenga Simba.

Kwa fedha hizi, nini kinaikwamisha Simba kufanya vizuri?

Shiriki Mjadala https://jamii.app/MoBilioniSimba

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports
❀2πŸ‘1
MICHEZO: Klabu ya #SimbaSC imeingia makubaliano na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri #Betway kuwa mdhamini mkuu kwa mkataba wenye thamani ya Tsh. Bilioni 20 kwa Miaka mitatu.

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Zubeda Sakuru amesema β€œUdhamini huu unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa.”

Ikumbukwe, udhamini huo mpya unakuja baada ya Simba kuachana na mdhamini wake mkuu, Kampuni ya M-Bet bila kuwekwa wazi kilichotokea ambapo Mwaka 2023 pande hizo zilisaini mkataba wa Miaka mitano wenye thamani ya Tsh. Bilioni 26.1.

Soma Zaidi https://jamii.app/MdhaminiMkuuSimba

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSports