This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa #ACTWazalendo, Isihaka Mchinjita anasema iwapo chama chake kikishinda Uchaguzi Mkuu katika Kiti cha Urais, watafanya mabadiliko katika eneo la Tanganyika Packers lililopo Kawe lisitumiwe na Boniface Mwamposa kwaajili ya kuombea Watu wapate ajira bali litarejeshwa kuwa sehemu ya Viwanda
Soma https://jamii.app/ACTKuhusuKawe
#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025

❤4
UTEUZI: Rais Samia leo Juni June 23 2025 amemteua Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi Tanzania Balozi Simon Nyankoro Sirro kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Zaidi bofya https://jamii.app/UteuziJuni23
#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi

❤1
Rais Samia leo Juni 23, 2025 amemuhamisha Kenan Laban Kihongosi kutoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Paul Makonda
Zaidi bofya https://jamii.app/UteuziJuni23
#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
Zaidi bofya https://jamii.app/UteuziJuni23
#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
🔥1
Rais Samia leo Juni 23, 2025 amemteua Mhandisi Machibya Masanja kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Zaidi bofya https://jamii.app/UteuziJuni23
#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
Zaidi bofya https://jamii.app/UteuziJuni23
#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
❤4
Mara nyingi, maamuzi tunayoogopa ndiyo hasa yanayobeba mabadiliko tunayoyahitaji maishani. Hofu hukuzuia kuona picha kubwa lakini ndani yake kuna nafasi ya kukua, kubadilika na kuvuka mipaka uliyoiweka mwenyewe
Usiogope kuchukua hatua kwa sababu ya hofu ya kushindwa, kumbuka, safari ya mafanikio huanza na ujasiri wa kufanya kile ambacho wengine wanaogopa
#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJF #GoodMorning

❤6
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Dodoma: Akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa Mifumo ya Kidijiti, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema “Wanaokuja kujieleza na kuwashawishi mjiridhishe kuwa lugha zao haziwapelekei na nyie kuingia kwenye machafuko yakapoteza usalama na amani ya nchi”
Soma https://jamii.app/MajaliwaKushawishiwa
#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
Soma https://jamii.app/MajaliwaKushawishiwa
#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama hicho, imeahirishwa hadi Julai 10, 2025 baada ya Jaji aliyetakiwa kuisikiliza kudaiwa yupo Mtwara hivyo kushindwa kufika Mahakamani
Juni 10, 2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, iliagiza CHADEMA kusitisha shughuli zote za Kiutendaji na oparesheni hadi Kesi hiyo itakaposikilizwa. Katika kesi hiyo Said na wenzake wanadai CHADEMA imekuwa ikiitenga #Zanzibar katika masuala mbalimbali, ikiwemo mgawanyo wa Rasilimali Fedha
Kupitia Ukurasa wake katika Mtandao wa X, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche ameandika “Kesi ya kina Said Issa ni Kesi ya Kisiasa kujaribu kuzuia Chama chetu kufanya shughuli zake halali. Jaji aliyepanga Kesi leo anakosaje kuwepo Mahakamani Siku ya Kesi tena Kesi muhimu kama hii kwa Nchi?”
Soma https://jamii.app/KesiYaCHADEMAJulai10
#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa

DAR: Siku moja kabla ya mchezo dhidi ya #Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Uongozi wa #Simba haujatuma wawakilishi katika Mkutano uliohusisha Wanahabari ambao ni maalum kwa ajili ya kuzungumzia mtanange huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano Juni 25, 2025
Taratibu za Ligi hiyo ni kuwa siku moja kabla ya mchezo, timu husika zinatakiwa kutuma Kocha na Mchezaji kuzungumza na Wanahabari kuhusu mchezo unaofuata ambapo ni ratiba pia inayofuatwa na Azam TV ambao wanahusika kurusha matangazo ya Ligi
Soma https://jamii.app/SimbaMkutanoni
#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25

🤣4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwassa ameipa siku mbili Kampuni ya IFS Consulting Limited ambayo ilipewa tenda na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ya kupakia na kushusha Mizigo, kuwalipa Wabeba Mizigo malipo yao wanayodai ya Wiki Tisa katika Bandari ya Bukoba
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mgomo uliofanywa na Wabeba Mizigo Juni 23, 2025, wakidai stahiki zao kiasi cha Tsh. Milioni 18 ambapo Meneja IFS Consulting Limited Kagera, Godfrey Ismail, amesema wameshakusanya Tsh. Milioni 6 ya Fedha wanayodaiwa na wanaendelea na mchakato
Baada ya maelekezo hayo ya Mkuu wa Mkoa, Wabeba mizigo wameendelea na Kazi wakiisubiri, Jumatano ya Juni 25, 2025 kujua hatima ya malipo yao
Soma https://jamii.app/BukobaBandarini
Video Credits: Azam TV
#Accountability #JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JamiiForums #JamiiAfrica

DODOMA: Akizungumza Bungeni, Juni 24, 2025, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema “Utafiti uliofanyika hivi karibuni ukionesha Watanzania wengi wanaunga mkono Serikali ya chama hicho unatakiwa kupingwa kwa Utafiti mwingine na sio wapingaji kujibu kwa hasira kwani hali iliyopo ni nzuri sana.”
Soma https://jamii.app/UtafitiCCM
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025

Kutambua haki zako bila kuelewa na kutimiza wajibu wako ni sawa na kuwa na gari bila mafuta, linaweza kuwa la kisasa na lenye uwezo lakini haliwezi kukupeleka popote.
Jamii bora hujengwa na raia wanaotambua kuwa haki huambatana na wajibu
Vijana tushiriki katika shughuli za kimaendelo, mikutano ya kijamii na majukwaa mbali mbali ili kuhakikisha Haki zetu zimezingatiwa na kushauri maboresho tunayoyataka kwenye jamii yetu
#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment

DODOMA: Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza #Bungeni leo, Juni 24, 2025 ametoa ufafanuzi wa utofauti kati ya Deni la Taifa na Deni la Serikali
Amesema Deni la Taifa linahusisha Deni la Serikali na Sekta Binafsi, mfano inapotokea Mfanyabiashara amekopa katika Taasisi za Kifedha, wakati Deni la Serikali linahusiana na Mapato ya Serikali
Soma https://jamii.app/DeniUfafanuzi
#Uchumi #Economy #JamiiForums #JamiiAfrica
Amesema Deni la Taifa linahusisha Deni la Serikali na Sekta Binafsi, mfano inapotokea Mfanyabiashara amekopa katika Taasisi za Kifedha, wakati Deni la Serikali linahusiana na Mapato ya Serikali
Soma https://jamii.app/DeniUfafanuzi
#Uchumi #Economy #JamiiForums #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza kuhusu hoja ya Deni la Taifa amesema ni vema Wananchi wakajadiliana kuhusu matumizi ya Mkopo na sio ukubwa wa deni lililopo
Mwigulu ameyasema hayo Bungeni leo Juni 24, 2025
Soma https://jamii.app/DeniTakwimu
#JFUchumi #JFEconomy #JamiiForums #JamiiAfrica

Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akisema tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, ni muhimu kutafakari kwa makini iwapo Viongozi tuliowachagua waliwakilisha maslahi yetu kikamilifu
Mdau, Mbunge wako ni nani, na juhudi zake Jimboni kwako zimetimiza matarajio yako? Unampa alama ngapi kati ya 10 kulingana na utendaji wake?
Mjadala https://jamii.app/RateYourMP
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
Mdau, Mbunge wako ni nani, na juhudi zake Jimboni kwako zimetimiza matarajio yako? Unampa alama ngapi kati ya 10 kulingana na utendaji wake?
Mjadala https://jamii.app/RateYourMP
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amekutana na Walimu Shule za Msingi na Sekondari Wilayani hapo kuwashukuru kwa ushirikiano na ametoa Tsh. Milioni 2 yakununua matofali ya kujenga Ofisi za Chama cha Waalimu Hai
Kikao hicho kilifanyika Juni 21, 2025, Mjini Bomang'ombe
Soma https://jamii.app/MbungeWaHai
Video: Bananafm Tz
#Siasa #Accountability #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Kikao hicho kilifanyika Juni 21, 2025, Mjini Bomang'ombe
Soma https://jamii.app/MbungeWaHai
Video: Bananafm Tz
#Siasa #Accountability #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika amesema kitendo cha Jaji Hamidu Mwanga, aliyepangwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake Wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama hicho, kutotokea Mahakamani ni mwendelezo wa kutotenda Haki
Mnyika ameeleza kuwa tayari wameshaandika barua ya kuonesha kutokuwa na Imani na Jaji huyo na kutaka ajiondoe na shauri hilo apangiwe Jaji mwingine
Katika kesi hiyo Said na wenzake wanadai CHADEMA imekuwa ikiitenga #Zanzibar katika masuala mbalimbali, ikiwemo mgawanyo wa Rasilimali Fedha
Soma https://jamii.app/JajiKesiYaCHADEMA
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #Siasa

DAR: Mwanachama wa #ACTWazalendo, Wakili Peter Madeleka, amesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025 kwa ya kudai “reforms” kipindi hiki ni kosa la Jinai
Amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi TV ambapo ameongeza kuwa ana uhakika wa kushinda Ubunge katika Uchaguzi wa 2025 kwa kuwa licha ya changamoto zilizopo bado nafasi ipo kwa Vyama vya Siasa
Madeleka ambaye aliwahi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi kabla ya kujipambanua kuwa Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, alijiunga na ACT, Mei 2025
Soma https://jamii.app/MadelekaKauli
#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025
Amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi TV ambapo ameongeza kuwa ana uhakika wa kushinda Ubunge katika Uchaguzi wa 2025 kwa kuwa licha ya changamoto zilizopo bado nafasi ipo kwa Vyama vya Siasa
Madeleka ambaye aliwahi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi kabla ya kujipambanua kuwa Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, alijiunga na ACT, Mei 2025
Soma https://jamii.app/MadelekaKauli
#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025
Kujiheshimu si tu kuhusu namna unavyowatendea wengine, bali zaidi ni namna unavyojitendea mwenyewe. Kujitunza ni tendo la upendo wa ndani, ishara ya kwamba unatambua thamani yako na unathamini maisha yako katika ukamilifu wake
Unapojitunza, unatangaza kuwa nafsi yako ina thamani. Unapojithamini, unawaonesha wengine jinsi ya kukuheshimu. Unapokuwa na amani ndani yako, una uwezo wa kuwapa wengine toleo bora la ‘wewe’ na si kilichobaki.
Jitunze, Jiheshimu, Jipende!
#GoodMorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #Selflove

❤2🙏2
Juni 16 - 17, 2025, JamiiAfrica iliendesha mafunzo maalum kuhusu Akili Unde katika Uandishi wa Habari (AI in Journalism) yaliyolenga kukuza Uelewa na Ujuzi wa Teknolojia katika Taaluma ya Habari
Mafunzo hayo yalilenga kuendana na Mabadiliko ya Dunia na Teknolojia ya Habari ambapo Wanafunzi walijifunza na kujadiliana masuala anuai kuhusu AI ikiwemo matumizi, faida na changamoto zinazotokana na Teknolojia hiyo hususan suala la Upotoshaji wa Taarifa
Mafunzo haya yaliyohusisha Wakufunzi na Wanafunzi wa Shahada ya Uandishi wa Habari pamoja na Uhusiano wa Umma yalitoa fursa ya kujua namna teknolojia inavyobadilika mara kwa mara na namna ya kukabiliana na taarifa zisizo sahihi zinazozalishwa na AI.
#JamiiAfrica #JamiiForums #AIJournalism #FactChecking