JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024 amependekeza mambo kadhaa kwa Shirika la Posta ili kuboresha Huduma hasa kwa njia ya Mtandao

Anasema ingawa Shirika la Posta limejitahidi kukabiliana na Maendeleo ya Kiteknolojia kwa kiwango fulani, bado kuna changamoto kama vile kutokuwa na Miundombinu ya Kidijitali ya kutosha, ufinyu wa Upatikanaji wa Huduma za Posta katika maeneo ya Vijijini na Ushindani kutoka kwa watoa Huduma wa Kampuni binafsi.

Soma https://jamii.app/PostaHudumaMtandao

#JamiiForums #ServiceDelivery #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Familia ya Flavian Methew Nyandikuu (85) Mkazi wa Mwenge Mlalakuwa, Mtaa wa Nyendikuu imedai Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa ‘imewapora’ Viwanja viwili ambavyo wamevimiliki kihalali kwa Miaka 40 na kudai Viwanja hivyo vimekabidhiwa kwa Watu wengine kinyume cha utaratibu

Msemaji wa Familia, Fortunatus Buyobe amesema “Ni Viwanja Namba 2107 na 2120 vipo Kilongawima, Mbezi Beach, ilikuwa sehemu ya shamba baadaye vikapimwa, miaka kadhaa nyuma kuna Wavamizi walijitokeza, kesi ikaenda Mahakamani, Mzee Nyandikuu akashinda na nyaraka halali zipo.”

Akifafanua kuhusu mgogoro huo, Wakili Barnaba Luguwa amesema “Nimepitia nyaraka za hukumu zimeonesha viwanja vinamilikiwa kihalali na Mzee Nyandikuu.”

Akihojiwa na ITV kuhusu madai hayo, Kamishna wa Ardhi Mkoa, Shukran Kyando amesema “Sisi hatujawahi kummilikisha mlalamikaji hiyo ardhi wala hatujawahi kumpa ofa, ardhi ile ilipimwa Mwaka 2000.”

Soma https://jamii.app/FamiliaYaNyandikuu

#JFMatukio #JamiiForums #Accountability #CivilRights
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wameanzisha mijadala tofauti kuhusu tabia ya Wabunge kutelekeza Majimbo yao na kusubiri hadi Miezi michache kabla ya uchaguzi ndio wanarudi kumalizia miradi na ‘vi zawadi vya hapa na pale’ ili kuwahadaa wapiga kura

Mdau mmoja amesema kama maendeleo anayoyaona sasa yangekuwa yanafanyika kwa utaratibu tangu mwaka wa kwanza wa uongozi, jamii ingekuwa mbali sana

Mdau mwingine amesema Wananchi wanapaswa kujifunza na kutambua tofauti kati ya maendeleo ya kweli na propaganda za kisiasa. Kwa wale wanaotaka kuendelea kuongoza, wajue kuwa Wananchi wa sasa si kama wale wa zamani, macho na masikio yao yako wazi

Mdau, vipi ‘hekaheka’ za jimboni kwako?

Soma https://jamii.app/WabungeMlikuwaWapi

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesema Veterani waliopigana Vita ya Kagera ambao walikuwa hawapati Pensheni wataanza kulipwa Julai 2025 na si Julai 2026 kama alivyoeleza Bungeni, Juni 23, 2025 (Bunge la 12 Mkutano wa 19 na Kikao cha 51)

Ikumbukwe Juni 13, 2024, akiwa Bungeni, Waziri Tax aliliambia Bunge “Maveterani wote waliopigana Vita ya Kagera wameshalipwa na hakuna anayedai.”

Aidha, Septemba 2, 2024, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Natoa ushuhuda Mzee wangu ni mmoja kati ya ambao hawajapata kifuta chasho cha kupigana Vita ya Kagera”, pia Desemba 19, 2024, Mdau mwingine aliandika "CPL NGUSSA GULINJA 692 DET sijalipwa malipo yangu ya Vita ya Kagera, kila nikifuatilia naambiwa hakuna anayedai”.

Soma https://jamii.app/MalipoVitaKagera

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #CivilRights
Taarifa ya Naibu Waziri Kivuli Habari, Mawasiliano na TEHAMA, wa Chama cha ACT Wazalendo, Emmanuel Ntobi imetoa wito kwa Serikali kufungulia mitandao ya kijamii ya X (Twitter), Clubhouse na Telegram huku ikisema hatua ya kuifungia ni mwelekeo wa Serikali kutaka kuficha matukio, taarifa na habari mbalimbali zinazohusu uchaguzi mkuu 2025 na michakato yake yote

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Kufungiwa mitandao ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 (1) na (2) inayotoa uhuru wa kutoa mawazo, kutafuta na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi na uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati, pamoja na haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani, ambayo ni muhimu kwa shughuli za wananchi na muhimu kwa jamii

Soma https://jamii.app/SerikaliMitandaoACT

#JamiiForums #JamiiAfrica #DigitalRights #Accountability #Democracy #Governance
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel akiwa anajibu swali la Mbunge Hawa Bananga amesema bima ya afya haina lengo la kusaidia wasiojiweza

Amesema "Usisahau kwamba Bima ya afya sio mfuko wa kusaidia wasiojiweza, ni watu wanachangia fedha zao, halafu ziwatibu pale watakapokutana na matatizo”

Zaidi https://jamii.app/BimaYaAfyaWasiojiweza

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFAfya #Accountability #ServiceDelivery #Governance #BimaYaAfyaKwaWote
Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) imeamuru vituo vyote vya televisheni na redio kusitisha mara moja matangazo ya moja kwa moja ya maandamano, ikidai kuwa ni ukiukaji wa Katiba ya Kenya na Sheria ya Mawasiliano na kutoa onyo kuwa vyombo vitakavyokaidi agizo hilo vitakumbana na hatua za kinidhamu.

Katazo hili imekuja wakati maandamano ya kitaifa yakiendelea kuadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano ya Juni 25, 2024 ya Vijana ya kupinga muswada wa fedha, yaliyogharimu maisha ya takriban watu 60

Maandamano ya mwaka huu, yaliyopewa jina la “Siku ya Uwajibikaji wa Vijana,” yamelenga masuala ya uwazi wa kifedha, haki za binadamu, na mageuzi ya usalama. Serikali imeweka ulinzi mkali katika maeneo nyeti kama Ikulu na Bunge, huku barabara kuu zikifungwa mapema asubuhi

Soma https://jamii.app/June25Maandamano

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #PoliceBrutality #HumanRights
Vituo vya Televisheni vya KTN na NTV vimeondolewa hewani baada ya kuendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Maandamano, ikielezwa kuwa ni baada ya kukiuka amri ya kutoonesha matangazo hayo

Hata hivyo, matangazo yanaendelea kupitia kurasa za #KTNNews na #NTVLive kwenye YouTube na pia kwenye kurasa za KTN Facebook na X (Twitter)

Mapema leo, Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) iliamuru vituo vyote vya televisheni na redio kusitisha mara moja matangazo ya moja kwa moja ya maandamano ikidai kuwa ni ukiukaji wa Katiba ya Kenya na Sheria ya Mawasiliano

Soma https://jamii.app/KTNKe

#JamiiAfrica #JamiiForums #Democracy #FreePress
DAR: Timu ya #Yanga imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 kwa kuifunga #Simba Magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa ikiwa ni ushindi wa Tano mfululizo dhidi ya Wapinzani hao wa Jadi

Ushindi huo uliotokana na Magoli ya Pacome Zouzoua na Clement Mzize unaifanya Yanga kumaliza Ligi kwa kuwa na Pointi 82 huku Simba ikibaki na alama 78

Michezo mingine iliyopita ya timu hizo Simba 0-1 Yanga (Oktoba 19, 2024), Yanga 1-0 Simba (Agosti 8, 2024), Yanga 2-1 Simba (Aprili 20, 2025) na Simba 1-5 (Novemba 5, 2023)

Soma https://jamii.app/YangaBingwa25

#JFSports #KariakooDerby #JamiiForums #JFLigiKuu25
Kuwa Mwananchi bora ni kuishi kwa Misingi ya Haki, Usawa na kuheshimu majukumu yetu katika Jamii. Tunapojifunza kuwa na maoni ya kujenga, kuuliza maswali ya msingi na kushiriki kikamilifu katika mambo yanayoathiri Maisha yetu, tunajifunza pia kuwa Viongozi wa kesho

Kiongozi mzuri huanza kwa kusikiliza, kuelewa matatizo ya Wananchi wake na kuyatatua kwa pamoja, hivyo Kijana usiache kushiriki, kuhoji na kusimamia Uwajibikaji kwa kila mmoja wetu

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
KENYA: Mahakama Kuu imetangaza kusitisha agizo la Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) la kupiga marufuku vituo vyote vya runinga na redio kurusha matangazo ya moja kwa moja ya maandamano, na kwamba kituo chochote kilichozimwa kutokana na agizo hilo kirejeshwe hewani mara moja

Jaji Chacha Mwita, ameagiza vituo vya NTV, KTN na K24 kurejeshwa hewani kutokana na ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na Chama cha Wahariri wa Kenya (KEG) kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali

Matangazo ya vituo hivyo yalizimwa wakati kukiwa na maandamano makubwa ya kitaifa dhidi ya Serikali, kuadhimisha Mwaka mmoja tangu maandamano ya Juni 25, 2024 ya Vijana ya kupinga muswada wa fedha, yaliyogharimu maisha ya takriban Watu 60

Soma https://jamii.app/KenyaJune25Updates

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #PoliceBrutality #HumanRights #FreePress
😁32