Mara nyingi tunakimbizana na maisha, tukisahau kuwa msingi wa ndoto zetu zote ni mwili wenye afya bora. Hakuna mafanikio yatakayokuwa na maana bila afya njema
Kila chaguo unalofanya leo, kama kula Mlo sahihi, kufanya Mazoezi au kupumzika vya kutosha ni Uwekezaji katika Maisha yako ya baadaye
Usingoje hadi uanze kuugua ndipo utambue thamani ya fya. Anza leo na hatua ndogo, kunywa Maji ya kutosha, tembea zaidi, punguza Msongo wa Mawazo na kula Mlo kamili
#JamiiForums #JamiiAfrica #GoodMorning #AmkaNaJF

👍1
#KENYA: Watu takriban 16 wameripotiwa kufariki kufuatia maandamano ya “Siku ya Uwajibikaji wa Vijana” yaliyofanyika jana, Juni 25, 2025, katika kuadhimisha Mwaka mmoja tangu Maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu(KNCHR), Dkt. Raymond Nyeris, zaidi ya Watu 400 walijeruhiwa, wakiwemo Waandamanaji, Maafisa wa Polisi na Waandishi wa Habari. Kati ya hao wengi walitibiwa na kuruhusiwa kurudi Nyumbani, huku 83 wakihitaji Matibabu zaidi
#KNCHR pia imesema Watu 61 walikamatwa na kuzuiliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi, wengi wao wakiwa kutoka Kaunti ya #Nairobi
Soma https://jamii.app/MaandamanoCasualties
#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #Governance

❤1
DAR: Barabara ya Kivule kwenda Banana ambayo imekuwa ikilalamikiwa na Wadau wa JamiiForums.com imeanza kukarabatiwa ambapo kwa takribani wiki nzima kumekuwa na mchakato wa maboresho unaoendelea
Desemba 17, 2023 mmoja wa Wadau aliandika wakati wa Mvua hali huwa mbaya kiasi kwamba shughuli muhimu zilikuwa hazifanyiki kutokana na Barabara kuharibika kwa kiwango kikubwa huku kukiwa hakuna ushirikiano kutoka kwa Viongozi wao kuhusu maboresho
Soma https://jamii.app/BarabaraKivule
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #JamiiAfrica

Mdau wa JamiiForums.com anaeleza Serikali ilianzisha Mfumo wa Public Employee Performance Management Information System (PEPMIS) ili kurahisisha Utendaji wa Watumishi lakini bado baadhi ya Watumiaji wanapitia changamoto
Anadai kipengele cha kupima Utendaji wa Mtumishi, Wakuu wa Idara ya Halmashauri ya Kigoma Ujiji hawana uelewa mzuri wa kukitumia hali ambayo imesababisha Watumishi wa ngazi za chini kuwa na alama 0% wakati mhusika akiingia katika akaunti yake anaona alama nzuri na ametekeleza majukumu yake inavyotakiwa
Anahoji Afisa Utumishi, Afisa Elimu, Wakurugenzi n.k wanapokuwa hawatekelezi majukumu yao katika Mfumo wa PEPMIS mbona hawachukuliwi hatua? Uzembe wao unachangia wale wa chini wakose Haki zao za msingi.
Soma https://jamii.app/MfumoWaPEPMIS
#Accountability #JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JamiiAfrica

Katika Mazingira yenye ushindani wa Kisiasa, Kijamii na Kibiashara, Waandishi wa Habari wanakumbana na changamoto kama Shinikizo kutoka kwa wenye Mamlaka, Upendeleo wa Vyombo au Wahariri na ushawishi kutoka kwa Wafadhili au Wamiliki wa Vyombo vya Habari
Katika yote haya, ukweli na Haki ya Wananchi kupata Taarifa sahihi vinapimwa kila Siku. Je, ni taarifa zote zinahitaji Mizania? Tunawezaje kuhakikisha kuwa Habari haipindishwi kwa maslahi binafsi au ya Taasisi fulani?
Kufahamu haya na mengine, usikose kujiunga nasi kwenye Mjadala wa Mizania kwenye Uandishi wa Habari, tutachambua maeneo muhimu yanayohitaji Mizania, namna ya kukabiliana na shinikizo na Ulinzi wa Uhuru wa Habari
Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025

Mdau wa JamiiForums.com anaandika “Ningependa kufichua uovu wa #Rushwa unaoendelea katika Vituo vya Ukaguzi wa Mazao ya Kilimo na Maliasili vilivyopo njia ya Segera - Dar kupitia Bagamoyo, hata ukiwa na risiti zote za Ushuru wanakulazimisha utoe pesa kwa kitisho cha kukufanyia ukaguzi zaidi.”
Anaongeza “Wanajua umebeba Mali za kuoza ama unawahi kufikisha Mzigo Sokoni basi wanakuambia ukaguzi huo wa ziada utafanyika kukipambazuka."
Anaongeza "Kwakweli ni uonevu uliokithiri. Mamlaka za Serikali ikiwemo #TAKUKURU ifanye uchunguzi kwani tunaoumia ni wengi katika suala hili.”
Soma https://jamii.app/UkaguziWaMazao
#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica #Uwajibikaji

Karibu kwenye Mjadala wa Mizania katika Uandishi wa Habari. Je, waandishi wa habari wanawezaje kusimamia ukweli bila kupindishwa na shinikizo, upendeleo au ushawishi?
Tujadili pamoja, ni maeneo gani yanahitaji mizania zaidi? Uhuru wa habari unalindwaje katika mazingira ya sasa?
Jiunge nasi kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Tujadili pamoja, ni maeneo gani yanahitaji mizania zaidi? Uhuru wa habari unalindwaje katika mazingira ya sasa?
Jiunge nasi kuanzia saa 12 jioni hadi 2 usiku kupitia #Xspaces ya JamiiForums
Kujiunga bofya https://jamii.app/MizaniaSpaceJune26th
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
👍1
Akizungumza katika mjadala wa “Mizania katika Uandishi wa Habari Kuelekea Uchaguzi Mkuu; Ni Wapi Inahitajika?” Peter Elias Mhariri msaidizi wa siasa (Mwananchi) amesema “Mizania bado ni changamoto katika tasnia ya Habari Nchini hasa katika Vyombo vya Habari vya Mtandaoni, ni mara chache unaweza kukuta kuna Mizania sawa”
Ameongeza kwa kusema kuwa kuelekea katika Uchaguzi kunakuwa na mashinikizo mengi, hasa kutoka kwa Wanasiasa ambao wanakuwa na nguvu ya Ushawishi, ni vema Wadau wa Habari wakawa makini kwa hili
Amesema kwamba Vyombo vya Habari vinahitaji kusimamia au kuweka mkazo zaidi katika suala la Wanasiasa wenye Ushawishi kutumia nguvu waliyonayo ndani ya Vyumba vya Habari kwa lengo la kunufaika wao au kwa maana ya kupata maslahi binafsi
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kwa kusema kuwa kuelekea katika Uchaguzi kunakuwa na mashinikizo mengi, hasa kutoka kwa Wanasiasa ambao wanakuwa na nguvu ya Ushawishi, ni vema Wadau wa Habari wakawa makini kwa hili
Amesema kwamba Vyombo vya Habari vinahitaji kusimamia au kuweka mkazo zaidi katika suala la Wanasiasa wenye Ushawishi kutumia nguvu waliyonayo ndani ya Vyumba vya Habari kwa lengo la kunufaika wao au kwa maana ya kupata maslahi binafsi
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Akichangia mjadala kuhusu “Mizania katika Uandishi wa Habari Kuelekea Uchaguzi Mkuu; Ni Wapi Inahitajika?” Ergon (Mdau) amesema Vyombo vingi vya Habari vimekuwa vikiendesha shughuli zao zikiwa katika mazingira ya hofu kutokana na Uhalisia wa Hali ilivyo
Ameongeza kuwa “Media” nyingi zimekuwa visemeo vya Wanasiasa badala ya kuwa Wasemaji wa Jamii ya kawaida ndio maana hata taarifa nyingi zinazotawala zinahusu ambacho wanasiasa walikuwa wanakisema au wanatarajia kukisema
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kuwa “Media” nyingi zimekuwa visemeo vya Wanasiasa badala ya kuwa Wasemaji wa Jamii ya kawaida ndio maana hata taarifa nyingi zinazotawala zinahusu ambacho wanasiasa walikuwa wanakisema au wanatarajia kukisema
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Akiongea katika Mjadala, Mwanahabari Elias Msuya, amesema Vyombo vya Habari vilirekodi mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Josephat Gwajima, baadaye kukawa na shinikizo vikitakiwa kuondoa taarifa hiyo. Siku kadhaa baadaye kukawa na Watu mbalimbali wakiwemo Wanasiasa ambao walimjibu (Gwajima) lakini hakukuwa na shinikizo la kwamba hayo majibu nayo yasiwekwe hewani
Anasema Matukio kama yale ya kujibiwa kwa Askofu Gwajima yanaonesha kunakosekana kwa Mizania ya usawa, kwa kuwa kila upande unastahili kupata Haki sawa
Ameeleza kuwa, Kuelekea kwenye Uchaguzi ni vema Watu wote wanaohusika kwenye Vyama wakapewa Haki sawa, hii isiwe kwa Vyombo vya Habari Binafsi bali vyote
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Anasema Matukio kama yale ya kujibiwa kwa Askofu Gwajima yanaonesha kunakosekana kwa Mizania ya usawa, kwa kuwa kila upande unastahili kupata Haki sawa
Ameeleza kuwa, Kuelekea kwenye Uchaguzi ni vema Watu wote wanaohusika kwenye Vyama wakapewa Haki sawa, hii isiwe kwa Vyombo vya Habari Binafsi bali vyote
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
❤1
Akichangia mada katika mjadala wa Mizania katika Uandishi wa Habari Kuelekea Uchaguzi Mkuu Mkurugenzi Mtendaji (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema kuna Wanahabari hawajalipwa Miaka kadhaa, wanategemea “source” ndio awape, tayari inatengeneza ushawishi wa Mwanahabari kuandika tofauti na kile ambacho aliyetoa hela hatakipenda
Ameongeza kwa kusema “Unapopata stori ambayo inakuwa ya upande mmoja na ukaitumia, uwezo wako wewe Mwandishi unakuwa unafifishwa na unawanyima Haki wale wanaotaka kusikia upande wa pili unataka kusema nini”
Amesema Jamii ikielewa kuwa chombo chako cha Habari kina mwelekeo fulani inakuwa inashusha thamani ya Biashara yako
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kwa kusema “Unapopata stori ambayo inakuwa ya upande mmoja na ukaitumia, uwezo wako wewe Mwandishi unakuwa unafifishwa na unawanyima Haki wale wanaotaka kusikia upande wa pili unataka kusema nini”
Amesema Jamii ikielewa kuwa chombo chako cha Habari kina mwelekeo fulani inakuwa inashusha thamani ya Biashara yako
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Akichangia mada katika mjadala, Mdau Caejay, amesema ikionekana Chombo cha Habari fulani kinaripoti taarifa ambazo haziwafurahishi waliopo katika Utawala, kunatengenezwa Mazingira ya kuonekana hicho kilichoripotiwa sio sahihi
Ameongeza kuwa Kinachofanyika kwa sasa katika Vyombo vya Habari ni kuua Uzalendo wa Watanzania, kwani kusema mambo kwa maslahi ya Taifa sio kulichukia Taifa lako
Amesema “Kuna hii falsafa ya No Reforms No Election, inaonekana kuwa ni ya Kichama lakini kuna mambo ambayo ni ya Kitaifa, mambo kama hayo yalitakiwa kuwa katika Vyombo vya Habari ili kujadiliwa na kupatikana kwa Usawa”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kuwa Kinachofanyika kwa sasa katika Vyombo vya Habari ni kuua Uzalendo wa Watanzania, kwani kusema mambo kwa maslahi ya Taifa sio kulichukia Taifa lako
Amesema “Kuna hii falsafa ya No Reforms No Election, inaonekana kuwa ni ya Kichama lakini kuna mambo ambayo ni ya Kitaifa, mambo kama hayo yalitakiwa kuwa katika Vyombo vya Habari ili kujadiliwa na kupatikana kwa Usawa”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Akichangia mada katika mjadala Mjumbe Mtendaji Kamati Tendaji (TEF), Neville Meena, amesema “Wakati wa Uchaguzi kumekuwa hakuna Mizania ya usawa kwa Vyombo vya Umma ambavyo vinaendeshwa kwa Kodi za Wananchi, vingi vimekuwa vikiegemea upande mmoja”
Ameongeza kuwa “Suala la kusukumwa kuandika kwa upendeleo ni jambo ambalo lipo kwenye Vyombo vya Habari wala siyo siri, hilo jambo lipo na linatokea, Mimi mwenyewe nimekutana na hali hiyo mara tatu katika Vyombo vikubwa hapa Nchini”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kuwa “Suala la kusukumwa kuandika kwa upendeleo ni jambo ambalo lipo kwenye Vyombo vya Habari wala siyo siri, hilo jambo lipo na linatokea, Mimi mwenyewe nimekutana na hali hiyo mara tatu katika Vyombo vikubwa hapa Nchini”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Akichangia mada katika mjadala wa Mizania katika Uandishi wa Habari Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji (JamiiAfrica), Maxence Melo, amesema Suala la Mizania bado ni changamoto katika sekta ya Habari na hilo lipo wazi
Ameongeza kuwa “Mwanahabari anatakiwa kuelewa yeye anaishi katika Jamii, unachokiandika na kukiripoti kinatakiwa kuendana na Jamii husika, usipofanya hivyo ni rahisi Mwananchi kutafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake, ndio maana Watu wengi wanakimbilia kuwasilisha ujumbe wao kupitia njia mbalimbali za Mtandaoni
Amesema “Sisi JamiiAfrica tumekuwa tukiwapa nafasi Wananchi kueleza hisia zao ikiwemo kero zao, kufanya hivyo haimaanishi tunaichukia Serikali bali tunaonesha uhalisia wa kile kilichopo kwenye Jamii na ambacho kinahitajika”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
Ameongeza kuwa “Mwanahabari anatakiwa kuelewa yeye anaishi katika Jamii, unachokiandika na kukiripoti kinatakiwa kuendana na Jamii husika, usipofanya hivyo ni rahisi Mwananchi kutafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake, ndio maana Watu wengi wanakimbilia kuwasilisha ujumbe wao kupitia njia mbalimbali za Mtandaoni
Amesema “Sisi JamiiAfrica tumekuwa tukiwapa nafasi Wananchi kueleza hisia zao ikiwemo kero zao, kufanya hivyo haimaanishi tunaichukia Serikali bali tunaonesha uhalisia wa kile kilichopo kwenye Jamii na ambacho kinahitajika”
#JamiiForums #JamiiAfrica #PressFreedom #Democracy #Accountability #Uwajibikaji #MizaniaSpace #KuelekeaUchaguzi2025
❤1
Akichangia mada katika mjadala, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, amesema Usipokuwa na Uhuru wa Kiuchumi ni ngumu kuwa na Mizania, ni lazima utaegemea upande fulani
Ameongeza kuwa, Matarajio ya nafasi za Kisiasa pamoja na Mabadiliko ya Kiteknolojia yanachangia kukosekana kwa Mizania ya Habari
Amesema “Mizania ni kujibu maswali bila kuacha maswali, chochote ambacho kinaonekana kuacha maswali, kinamlazimu Mwanahabari kufuatilia majibu ambayo hayajakamilika”