JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kupumzika ni njia ya kuonyesha kwamba tunajithamini. Ni wakati wa kujisikia, kusikiliza mwili wako na kuiruhusu akili yako kutulia

Kupumzika kunaimarisha afya ya mwili na akili, huongeza ubunifu na hutupa nafasi ya kuona mambo kwa mtazamo mpya, hivyo usione aibu au kuhisi hatia unapojipa muda wa kupumzika

Leo chagua kupumzika, jipe nafasi ya kupumua, tulia, zima simu kwa muda, lala mapema au kaa sehemu iliyotulia

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha #LifeStyle
4👍1
Usikubali kuwa raia mtazamaji wa mustakabali wa Nchi yako. Taifa linahitaji Vijana wenye maono, Maadili na Moyo wa kujitoa, Vijana wanaochukua hatua badala ya kungoja.

Simama kwenye Misingi ya Haki na Uwajibikaji, sema kwa ujasiri dhidi ya Ukatili, Rushwa na Ubaguzi na Shiriki kwa vitendo kwenye shughuli za Kijamii, mchakato wa Uchaguzi au hata kwa kutoa Elimu na msaada kwa wengine

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
DAR: Kesi ya Marejeo iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri itatajwa leo Juni 27, 2025 Mahakama Kuu

Awali, shauri hilo lilipangwa kusikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jaji Mkwizu, lakini Juni 17, 2025 Mahakama iliagiza kuwa litakapotajwa tena Juni 27, Lissu anatakiwa kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/KesiMarejeoLissu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Governance #Democracy
Chama cha Mapinduzi kimesema ni marufuku kwa Mwanachama yeyote kualika kundi la wapambe au kuandaa msafara wa Magari, Pikipiki, Baiskeli, Ngoma na Matarumbeta ya kumsindikiza kwenda kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea

Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa mchakato wa ndani wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za Kugombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, unaanza rasmi Juni 28, 2025, hivyo kuwakumbusha Viongozi, Watendaji na Wanachama kuendelea kufuata Maadili ya Uchaguzi kama ilivyoanishwa kwenye Katiba, Kanuni za Uchaguzi wa CCM na Miongozo yake

Soma https://jamii.app/KuchukuaFomuCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025 #Democracy #Accountability #Governance
1
DAR: Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA wapo Mahakamani wakifuatilia shauri la Jinai No. 14496/2025, la Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Tundu Antiphas Lissu dhidi ya Jamhuri, ambapo anaomba Mahakama irejee uamuzi wa awali wa Hakimu anayeendesha kesi ya Uchochezi inayomkabili, ambaye alikubali maombi ya upande wa Jamhuri, ya kusikiliza ushahidi wa “mashahidi wa siri”

CHADEMA imeeleza kuwa Lissu hakufahamu jambo hilo ambalo linaathiri Haki yake ya kujitetea ipasavyo na linaweza kusababisha maamuzi yenye athari kubwa kwake binafsi

Soma https://jamii.app/LissuJuni27

#JamiiForums #Governance #Accountability #Democracy
DAR: Jamhuri imeweka mapingamizi matatu kutaka Kesi ya Marejeo iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA - Taifa, Tundu Lissu kwenye Mahakama Kuu kutupiliwa mbali

Kwa sasa kesi hiyo inaendelea kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Mawakili wa Lissu wanawasilisha hoja baada ya upande wa Jamhuri nao kuwasilisha hoja za mapingamizi yaliyowekwa.

Katika kesi hii, Lissu anaomba Mahakama irejee uamuzi wa awali wa Hakimu anayeendesha kesi ya Uchochezi inayomkabili katika Mahakama Kisutu, ambaye alikubali maombi ya upande wa Jamhuri kusikiliza ushahidi wa “mashahidi wa siri”

Soma https://jamii.app/LissuJuni27

#JamiiForums #Accountability #Democracy #JamiiAfrica
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa kueleza kuwa linafanya kazi kubwa katika kuzuia uhalifu.

Amesema hayo wakati akihutubia Bunge, leo Juni 27, 2025

Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25

#JamiiForums #Siasa #Governance
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akihutubia Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 55, leo Juni 27, 2025, Rais Samia ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuongeza jitihada za kukomesha matukio ya Watu kupotea

Soma https://jamii.app/WatuKupotea

#JamiiForums #Siasa #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu amesema baada ya kuingia Madarakani alikuja na Falsafa ya 4R, ambayo iliifanya Serikali kuunda Tume ya Maridhiano ambayo ilitoa mapendekezo ya muda mrefu na mfupi katika kuboresha masuala mbalimbali

Ameeleza kati ya mapendekezo ni kuondoa zuio la Vyama vya Siasa kutokufanya mikutano ya hadhara na hivyo kuviwezesha Vyama hivyo kufanya shughuli zao kwa Uhuru

Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25

#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia amesema pendekezo la Tume ya Maridhiano kuhusu mchakato wa Katiba Mpya lipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mwaka 2025/2030, na mchakato utafanyika ndani ya kipindi hicho

Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25

#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1👍1
Unapokuwa na ratiba katika shughuli zako iwe ya Wiki, Mwezi, Miezi au Mwaka inaweza kusaidia kurahisisha baadhi ya mambo yako na pia kukuwezesha kufanya majukumu mengi kwa mpangilio mzuri

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko maarufu kwa jina la 'Wachokonozi' wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa makosa mawili, jana Juni 27, 2025

Wamesomewa mashtaka ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Kifungu Namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao na kutoa maudhui Mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na Kifungu Namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta

Wawili hao wanaosimamiwa na Wakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), walipatiwa dhamana, na kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Julai 21, 2025

Soma https://jamii.app/WachokonoziDhamana

#JamiiForums #JFMatukio #DigitalRights #CivilRights #JamiiAfrica
MOROGORO: Mdau aliyejitambulisha ni Mkazi wa Kijiji cha Lungongole kilichopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara, anadai Barabara ya Kilosa kuelekea Kijiji cha Kilama “Mwiche Road” ina hali mbaya kutokana na kuharibika

Anaeleza Barabara hiyo ambayo inatumiwa na Wakulima wanaokwenda na kurudi shambani ni njia kuu ya Wakazi wanaoishi upande huo wa Milimani wakati wanapotaka kuelekea Kilosa Road

Anadai maeneo mengine ya Barabara yamekuwa na makorongo makubwa kiasi kwamba Watumiaji imewabidi kuunda njia mbadala katika mashamba ya Watu, anatoa wito TARURA kumalizia kazi waliyoianza

Soma https://jamii.app/Lungongole

#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji
1🔥1