JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Usikimbilie kufanya mengi bila ubora, fanya kwa kiasi lakini kwa kiwango cha juu na ubora zaidi

Katika maisha au kazi mafanikio si idadi, bali ubora ndio huleta matokeo ya kweli

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
1
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia kero ya mazingira duni ya vyoo vya Stendi Kuu ya Mkanaledi ya Mtwara, akidai hali hiyo inahatarisha #Afya za Watumiaji na wanavyovizunguka

Soma https://jamii.app/VyooVichafuMkanaledi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
1
Kupitia Televisheni ya Taifa ya Iran, Wananchi wamehimizwa kuondoa programu ya #WhatsApp kwenye Simu zao, ikidaiwa (bila ushahidi wowote wa moja kwa moja) kuwa programu hiyo inakusanya taarifa za Watumiaji na kuzipeleka kwa #Israel

Katika taarifa yake, Kampuni ya #Meta ambayo inamiliki WhatsApp imesema “Tunasikitishwa na ripoti hizi za uongo ambazo huenda zikatumiwa kama kisingizio cha kuzuiwa kwa Huduma zetu wakati Watu wanazihitaji zaidi.”

Serikali ya #Iran imekuwa ikizuia upatikanaji wa Mitandao mbalimbali ya Kijamii kwa Miaka mingi, lakini Watu wengi nchini humo hutumia mbinu za kukwepa vizuizi hivyo kama #proxies na Mitandao Binafsi ya Intaneti (VPNs) ili kuendelea kupata Huduma

Mwaka 2022, Iran ilipiga marufuku WhatsApp na Google Play wakati wa Maandamano makubwa ya kupinga Serikali yaliyotokana na kifo cha Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa na Polisi wa Maadili wa Nchi hiyo. Marufuku hiyo iliondolewa mwishoni mwa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/IranVSWhatsApp

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiendelea, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa #TFF, Wakili Aloyce Komba, akizungumza na Clouds FM amesema Kamati ya Uchaguzi haipo huru kutokana na mazingira ya ufanyaji kazi kutokuwa katika msingi ulionyooka

Ikumbukwe Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza Uchaguzi huo utafanyika Agosti 16, 2025, Jijini Tanga huku nafasi zinazowaniwa zikiwa ni za Rais (Nafasi 1) na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji (Nafasi 6)

Soma https://jamii.app/UchaguziTFF25

#JamiiForums #JFSports #Accountability
1
DIPLOMASIA: Kufuatia tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kutaka nchi 36 (ikiwemo Tanzania) kufanyia kazi baadhi ya mambo ya kiuhamiaji ambayo yanaweza kusababisha raia kuzuiwa kuingia Marekani, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali ya Tanzania imeanza mashauriano

Amesema, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, imeanza kufanya mashauriano na wenzao upande wa Marekani kujua maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho, hususani yanayohusiana na masuala ya kikonselii ili kuharakisha Tanzania isiwe moja ya nchi zitakazozuiwa kuingia Marekani

Tamko la Serikali linakuja baada ya Donald Trump kutaka nchi 36 kufuatilia na kutoa taarifa kabla ya Julai 18, 2025, kuhusu utayari wa nchi zao kuboresha hati za usafiri kwa raia wao, pamoja na kuchukua hatua kuhusu raia wao walioko Marekani kinyume cha sheria

Soma https://jamii.app/TanzaniaMazungumzoMarekani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akiuliza swali Bungeni leo, Juni 18, 2025, Mbunge wa Moshi Vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi ametaka kujua lini Serikali itatunga Sheria itakayomshurutisha Mtoto kuwatunza Wazazi wake wakizeeka

Amejibiwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis ambaye amesema suala hilo lipo katika Sera, Maboresho ya Mwaka 2003

Soma https://jamii.app/MatunzoYaWazee

#Maisha #Accountability #Governance #JamiiForums #Malezi
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla, leo Juni 18, 2025 amezungumzia hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, akisema bado deni letu ni himilivu, hivyo kama Waziri wa Fedha anakopa ili kuleta maendeleo akope, Bunge litapitisha

Soma https://jamii.app/KigwangallaMikopoMwigulu

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Bungeni
Ulitumia mbinu gani ili kufanikisha kujenga Nyumba yako ya kwanza? Ulichukua Mkopo au uliweka Akiba kidogokidogo?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NyumbaMaraKwanza

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats #JFStories #Maisha
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Bara, Stephen Wasira amesema tangu kupata uhuru, Tanzania imepata maendeleo makubwa na kwamba anayesema hakuna kilichofanyika anamfanisha na 'Kasuku' kwa kuwa anazungumza mambo kwa kukariri bila kujua maana yake

Amesema hayo Juni 17, 2025 alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Wilayani Katoro

Soma https://jamii.app/WasiraKatoro

#Siasa #Governance #JamiiForums #Kuelekea2025
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza katika tukio la Serikali kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kisasa wa Arusha Council Sports Complex, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema “Nawaomba tumrudishe Mama, tutafanya makubwa zaidi.....mtakaposhtaki hamuwezi kufanikiwa.”

Uwanja huo ambao utajengwa eneo la Bondeni City, utakuwa na uwezo wa kubeba Watu kati ya 8000 - 10,000 walioketi, ukiwa umezungukwa na Viwanja vya Mpira wa Kikapu 2, Uwanja wa Mpira wa Wavu (1) na Viwanja vya Tenisi (2)

Soma https://jamii.app/KariaArusha

#JamiForums #JamiiAfrica #JFSports
1
Mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2024/25 zinaendelea kushika kasi, #Yanga imeendelea kubaki katika nafasi ya kwanza kwa kufikisha Pointi 76 baada ya kuiunga Tanzania Prisons Magoli 5-0, #Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 75 baada ya kuichapa KenGold Magoli 5-0 pia

Yanga imeshinda ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya wakati Simba nayo ilikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora

Timu hizo mbili zimesaliwa na michezo miwili kukamilisha Ligi, ukiwemo unaozikutanisha zenyewe mnamo Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, ambapo ni mchezo unaotarajiwa na wengi kuwa utaamua bingwa wa Ligi

Soma https://jamii.app/MbioZaUbingwa

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu kuelekea kwa Mbunge, Luhaga Mpina kwamba yalimfurahisha na kumpa furaha

Jana Juni 17, 2025, Rais Samia akiwa ziarani Mkoani Simiyu alisema Mbunge wa Kisesa (Mpina) 'amerukaruka' kwenye kutaja Mambo yaliyofanyika Jimboni kwake, huku akieleza amelidharau Jimbo lake kwa kusema "Kisesa iko kama Mwanamke aliyesuka Nywele"

Soma https://jamii.app/MbungeNgonyani

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025
2
Kijana, Kujua haki zako ni ngao ya kukulinda. Ukiwa na uelewa wa haki zako, unapata ujasiri wa kuzitetea si tu kwa ajili yako, bali pia kwa ajili ya wengine katika jamii.

Ni wajibu wetu sote kujielimisha kuhusu haki na majukumu yetu kama raia

Tuelewe sheria, sera na mifumo ya kisheria inayotuathiri na tushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi ili kuhakikisha jamii yenye haki, usawa na uwajibikaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa