JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Maafisa Polisi wamemkamata Askari anayefahamika James Mukhwana kwa kuhusika na mauaji ya cha mwalimu na mwanablogu, Albert Omondi Ojwang' aliyefariki akiwa kizuizini baada ya kushikiliwa kwa kuchapisha taarifa za uongo

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi imesema kuwa Askari James wa Kituo cha Polisi cha Kati Nairobi alikamatwa Juni 12, 2025 na kuwekwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Capitol Hill na anatarajiwa kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya Ojwang'

Ikumbukwe Albert Ojwang' (Mwanaharakati na Mwanamtandao) alifariki Dunia Juni 8, 2025, Siku moja baada ya kukamatwa Nyumbani kwake Kakot, Homa Bay, akiwa chini ya uchunguzi kuhusu chapisho alilodaiwa kumdhalilisha Naibu Mkuu wa Polisi kwenye Mtandao wa Kijamii wa X

Soma https://jamii.app/AskariJamesKifoOjwang

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
DAR: Klabu ya #Simba imesema Serikali imeruhusu watumie Uwanja wa Mkapa kufanya mazoezi Juni 14, 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya #Yanga unaoratajiwa kuchezwa Juni 15, 2025

Barua hiyo imeeleza kuwa uwanja upo tayari kwa mchezo na wameruhusiwa kwa mujibu wa Kanuni kwa kuwa Simba itakuwa ugenini katika mchezo huo ambao Yanga imekuwa ikisisitiza haitaingiza timu uwanjani

Barua imeandikwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Boniface Tamba kwenda kwa Simba na nakala kwa Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu

Soma https://jamii.app/SimbaMazoezi

#JFSports #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Mdau anadai changamoto ya foleni ya magari ya mizigo mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma ni kero kubwa, inakwamisha Uchumi wa Watu wengi na kuwafaidisha wachache

Anadai kuna Kiongozi wa Usalama hapo anamiliki eneo la kuegesha (parking) anatoza Sh 10,000 kwa siku badala ya Tsh. 5,000 inayotozwa kwingine na kwamba Mwanausalama huyo anatoa kipaumbele kwa Wateja wake kuvusha magari huku wengine wakibaki kucheleweshewa mchakato

Pia, Mdau anadai hali ya Watumishi kukosa uadilifu inachangia foleni kwa kuwa michakato inafanyika kwa kasi ndogo kwa baadhi ya Maafisa kujali maslahi binafsi

Ikumbukwe, Aprili 2025, Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo aliunda Kamati Maalumu kuchunguza msongamano huo ambapo baadhi ya Wadau walimwambia inatengenezwa na Watu wachache kwa sababu wanazozijua wao

Soma https://jamii.app/TundumaFoleniJuni

Video Credits: CHAWAMATA TV

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
SIMIYU: Mdau anakumbushia kuwa Machi 2021, Waziri wa Nishati (wakati huo), Dkt. Medard Kalemani alishiriki kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo, ambapo shamrashamra zilikuwa kubwa na kuwapa matumaini makubwa Wananchi

Mdau anasema Kalemani alieleza Kituo kitajengwa ndani ya Mwaka mmoja kwa gharama ya Tsh. Bilioni 75, anamnukuu "Umeme utakaozalishwa hapa ni mkubwa utauwezesha mkoa huu na mikoa jirani kuendesha shughuli za viwanda na uwekezaji unaohitaji umeme mwingi."

Hivyo, Mdau anadai kilichotokea mradi haujakamilika na hakuna majibu ya kueleweka kutoka kwa Mamlaka na kwamba changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara bado ipo kwa kuwa kituo hicho kilitegemewa kutatua changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/UmemeSimiyu

#JamiiForums #Accountability #Governance
KENYA: Mtuhumiwa wa pili ambaye ni fundi wa vifaa vya umeme amekamatwa kutokana na kosa la kuchezea Mifumo ya CCTV katika Ofisi ya Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi alipokuwa akishikiliwa Mwanamtandao, Albert Ojwang' (31)

Fundi huyo anatuhumiwa kuzima Mfumo wa Ulinzi wa Video kwa madai ya kulipwa Tsh. 60,000 hatua iliyofanikisha kufichwa kwa ushahidi kuhusu Ojwang' kuteswa na kuuawa akiwa ndani ya Kituo hicho cha Polisi

Fundi huyo ambaye jina lake bado halijawekwa hadharani inaelezwa kuwa amekamatwa leo Juni 13, 2025 baada ya Askari Polisi James Mukhwana kukamatwa

Soma https://jamii.app/MtaalamuCCTVAkamatwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeusogeza mbele mchezo Namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Simba ambao ulipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Juni 15, 2025

Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 katika Uwanja wa Mkapa kuanzia Saa 11:00 Jioni

Soma https://jamii.app/SimbaYangaJuni25

#JFSports #JamiiForums
Kila Juni 13, ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino.

Mwaka huu 2025 Kaulimbiu inaangazia umuhimu wa kuzuia Saratani ya Ngozi kwa Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Ualbino) kupitia uelimishaji, uchunguzi wa afya na upatikanaji wa Mafuta ya kuzuia Mionzi ya Jua (Sunscreen)

Ukosefu wa upatikanaji wa mafuta maalum ya ngozi, mavazi ya kujikinga na jua, pamoja na huduma za uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Ngozi, unasababisha vifo vinavyoweza kuzuilika kabisa

Soma https://jamii.app/AlbinismAwareness

#JamiiForums #JamiiAfrica #AlbinismAwarenessDay
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akisoma majibu ya barua yao ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo akisema barua iliyotumika kulifungia Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima haitambuliki na Mamlaka iliyotajwa kulifungia

Ameyazungumza hayo leo Juni 13, 2025 baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo upande wa Kanisa ukiwakilishwa na Wakili Kibatala unaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini

Soma https://jamii.app/KanisaLaGwajima

#JamiiForums #JFMatukio
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Naibu Katibu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, Askofu Maximilian Machumu “Mwanamapinduzi” amesema taarifa kuwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa amefungia Kanisa lao si za kweli bali lililofungiwa ni Kanisa la Glory of Christ Church ambalo halina uhusiano na Kanisa lao

Ikumbukwe, Juni 2, 2025 ilisambaa barua iliyoonesha imetoka kwa Kihampa akifungia Kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima lakini Wanasheria wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala wamesema majina ya Kanisa hayaendani na jina sahihi la Wateja wake (Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church)

Soma https://jamii.app/AskofuMaximilianMachumu

#JFMatukio #JamiiForums
BAADA YA SAMIA KUKUTANA NA VIPNGOZI WA YANGA, SIMBA; VIONGOZI TPLB WAJIUZULU

Baada ya mgogoro wa muda mrefu kuhusu Yanga na Simba kucheza mchezo wa Ligi Kuu, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mnguto amewasilisha barua ya kujiuzulu huku Rais wa #TFF, Wallace Karia akimsimamisha Kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa #TPLB, Almasi Kasongo

Haya yametokea ikiwa ni saa chache baada ya Rais Samia kufanya mazungumzo na Viongozi wa Klabu za #Simba na #Yanga na kisha taarifa kutoka kuwa mchezo huo uliokuwa uchezwe Juni 15, 2025 umeahirishwa hadi Juni 25, 2025

Soma https://jamii.app/TPLB_Wajiuzulu

#JamiiAfrica #JFSports
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, akizungumza wakati wa Ibada, Juni 3, 2025 alisema “Tuwe Wazalendo wa kuishi kwa Amani, tulijenge Kanisa na Taifa letu kwani ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutengana.”

Soma https://jamii.app/AskofuWolfgangPisa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Quotes #JFNukuu
Mdau wa JamiiForums.com anaeleza kuwa licha ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (#RITA) kuweka tangazo Mtandaoni kuwa Kituo cha Miito (CALL CENTER) kipo wazi Saa 2 Asubuhi hadi Saa 10 Jioni lakini simu yao 0800 117 482 haipokelewi na kuna muda inakatwa

Anaeleza lengo la RITA kuwa na Huduma nyingi Mtandaoni ni kusogeza Huduma karibu na Wananchi, lakini ni kawaida kuona malalamiko ya maombi kufanyiwa kazi kwa muda mrefu, akitoa mfano Kusajili Cheti inaweza kuchukua hadi Miezi Miwili ‘Account Status’ haibadiliki

Soma https://jamii.app/HudumaRITA

#JamiiForums #HudumaZaKijamii #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #JFMdau2025
Ushiriki wako kama kijana katika mchakato wa maamuzi, kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi taifa ni njia ya kuhakikisha kuwa maamuzi yanayoathiri maisha yako yanazingatia mahitaji na sauti yako

Shiriki kwenye midahalo, mikutano ya kijamii na michakato ya Kidemokrasia, uweze kuchangia mawazo, kuchochea mjadala na kushinikiza mabadiliko ya Sera kwa maslahi ya wengi

Zaidi soma https://jamii.app/VijanaUshiriki

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFVijana #RestlessDevelopment #UshirikiWaVijana
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema “Ni kweli Kituo cha Kupoza Umeme cha llamilo (Simiyu) kimechelewa Utekelezaji wake kutokana na sababu za Kiutendaji na kwamba Mkandarasi wa Ujenzi ameshapatikana, na Utekelezaji utaendelea ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme.”

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mdau kueleza licha ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, kuweka jiwe la msingi la Mradi Machi 2021 na kuahidi Unenzi kukamilika baada ya Mwaka mmoja lakini sasa inaelekea Miaka mitano hakuna kilichofanyika, changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara ipo vilevile, akahoji, kama Wananchi walidanganywa?

Taarifa ya #TANESCO imeongeza kuwa “Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO tutahakikisha tunakamilisha kwa awamu ujenzi wa Miradi yote ya Gridi Imara iliyopangwa kama ilivyokusudiwa katika maeneo yote nchini.”

Soma https://jamii.app/UmemeSimiyuMradi

#Governance #Accountability #Transparency #JamiiAfrica #Uwajibikaji  #ServiceDelivery #JamiiForums #JFMdau2025
DIGITALI: Wadukuaji wamekuja na mtindo mpya wa kusambaza Kiunganishi (Link) zitakazofanya udukuliwe taarifa zako utakapobofya link hiyo

Wadukuzi hao hujifanya wana picha zako hivyo hukuambia ubofye link ili kupata picha na ukibofya utatakiwa kuingiza taarifa zako kama Namba ya Simu

Ukipata ujumbe huo usifungue ili kuepusha kudukuliwa

Soma https://jamii.app/UsifungueUjumbeHuu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFDigitali #Accountability #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima), Askofu Maximilian Machumu (Mwanamapinduzi) kutangaza kuwa Kanisa lao halijafungwa na Serikali, Tawi la Kanisa hilo la Kibaha limefungwa na Watu wanaodhaniwa kuwa ni Askari Polisi kwa kuweka utepe na kuwataka Waumini waliokuwemo kuondoka

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X (Twitter), Mwanamapinduzi ameonesha Video na kuandika kuwa Jeshi la Polisi limefunga Kanisa hilo

Ikumbukwe, Juni 2, 2025 ilisambaa barua iliyoonesha Msajili wa Jumuiya ya Kiraia amelifungia Kanisa linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima lakini Wanasheria wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala wamesema majina ya Kanisa hayaendani na jina sahihi la Mteja wake (Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church)

Soma https://jamii.app/KanisaKibaha

#JamiiForums #JFMatukio #JamiiAfrica