JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau anaeleza hoja ya Watoto wa Shule kupumzika wakati wa likizo ilishatolewa maelekezo na Waziri wa Elimu kupitia kwa Kamishna wa Elimu kuwa mwongozo uliopo wakati wa likizo ni marufuku Watoto kwenda Shuleni kufundishwa

Anakumbushia tukio la hivi karibuni la Mwanafunzi kuchoma Moto majengo ya Shule ya Sekondari Jenista Mhagama (Songea), alipoulizwa alisema alitaka Shule ifungwe ili aende likizo, akisema ingawa njia hiyo si sahihi lakini ni ujumbe kuwa Wanafunzi wanatakiwa kupata Haki ya kupumzika

Mdau anadai alitegemea Waziri wa Elimu angetoa tamko haraka lakini anaona kimya, hivyo anahoji wanaosimamia Sekta ya Elimu ni wasomi, je, hawaoni umuhimu wa kupumzika? Hawajui kufanya hivyo ni mateso kwa Watoto? Hawajui Mtoto ana haki ya kupumzika, kujichanganya na Jamii na kucheza?

Soma https://jamii.app/LikizoKwaWanafunzi

#Elimu #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji #JamiiForums #Governance
1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uwepo wa #Demokrasia na Uhuru wa kutoa maoni sio ruhusa ya kuvunja Sheria, kutukana Watu na anayefanya hivyo anastahili kuchukuliwa hatua

Wasira ameeleza hayo Juni 12, 2025 alipokuwa akizungumza na Viongozi wa CCM katika Jimbo la Peramiho, Wilayani Songea

Soma https://jamii.app/WasiraRuvuma

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #Siasa #UchaguziMkuu2025
2
Kila mtu ana ndoto au mawazo ya mafanikio, lakini ni wachache sana wanaochukua hatua ya kweli kuyafanikisha

Tofauti kati ya waliofanikiwa na waliokwama ni hii: Wale wachache (1%) hawakai kungoja muda mzuri wanachukua hatua mara moja

Kuwa mmoja wa wanaochukua hatua

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
DAR: Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima) lililopo eneo la Ubungo limewekwa ulinzi mkali na Askari Polisi leo Juni 15, 2025 huku njia zote zinazowezesha Watu kufika kwenye kanisa hilo zikiwa zimezuiwa

Aidha, licha ya Askari hao kuwepo eneo hilo baadhi ya Waumini wamejitokeza maeneo ya karibu na kanisa hilo

Ikumbukwe Juni 13, 2025, Naibu Katibu wa Kanisa hilo, Askofu Maximilian Machumu (Mwanamapinduzi) alisema taarifa kuwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa amefungia Kanisa lao, si za kweli bali lililofungiwa ni Kanisa la Glory of Christ Church ambalo halina uhusiano na Kanisa lao, hivyo Jumapili hii wanatarajia kurejea Kanisani kuendelea na Ibada

Soma https://jamii.app/KanisaUfufuoUlinziPolisi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufufuo na Uzima) linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambalo Juni 2, 2025 lilifungiwa, wamejitokeza eneo la pembezoni mwa Kanisa hilo lililopo Ubungo wakipiga maombi huku Kanisa hilo likiwa limezungukwa na Askari Polisi

Juni 14, 2025, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Askofu Gwajima alitangaza uwepo wa ibada leo Juni 15, 2025 eneo la Ubungo

Soma https://jamii.app/WauminiGwajimaWasaliNje

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
Ajira kwa Vijana ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya Mtu Binafsi, Jamii na Taifa kwa ujumla. Ajira humfanya mtu awe na ari ya kutosha, kuwajibika na kushiriki kikamilifu katika nyanja zote za Kijamii na Kiuchumi

Kwa mujibu wa Utafiti wa Nguvu Kazi (ILFS 2021), Tanzania, ilikuwa na nguvu kazi ya Watu wapatao 25,861,023 ambapo kati ya Nguvu kazi hiyo, Vijana ni 14,219,191 sawa na 55.6%.

Soma https://jamii.app/UwajibikajiWaVijana

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFVijana #RestlessDevelopment #UshirikiWaVijana
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima) waliokuwa wamekusanyika leo Juni 15, 2025 kwaajili ya ibada wametawanywa na Askari Polisi waliokuwa wanalinda eneo hilo baada ya Waumini kujikusanya na kuanza kuelekea katika kanisa hilo

Awali, Waumini hao walikusanyika eneo la umbali wa takriban mita 300 tokea lilipo Kanisa hilo ambalo limezungukwa na Askari, ambapo walifanya maombi na kuimba nyimbo

Soma https://jamii.app/WauminiGwajimaWatawanywishwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema "Sijawahi hata siku moja kukaa na Mheshimiwa Rais, Spika au Waziri Mkuu na kuzungumzia kesi, kwanza sina hata majalada hapa. Tunazungumza mambo ya masilahi mapana ya Taifa" akifafanua kuhusu ufuatiliaji wa masuala ya Mahakama unaofanywa na viongozi wa Serikali haumaanishi kuingilia uhuru wa Mhimili huo

Amesema hayo leo, Juni 15, 2025 katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji George Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, iliyofanyika Ikulu Jijini Dodoma

Soma https://jamii.app/RaisHaingiliiMahakama

#JamiiForums #JamiiAfrica #ConstituonalRights
Mdau wa Jukwaa la JF Chit-Chats and Jokes ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala wa Siku gani unazipenda katika wiki

Ni kitu gani kinakufanya uwe na siku pendwa katika wiki?

Mjadala zaidi https://jamii.app/SikuIpi

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika ghafla ya kumuapisha Jaji Mkuu mpya George Masaju amesema "Lazima wananchi wafike mahali waelewe kazi ya mihimili hii na kumuweka Rais mahali anapostahili, kumtofautisha na Jaji Mkuu, Spika, lakini pia kuelewa Rais anavyofanya kazi kama Mkuu wa mhimili"

Ameyasema hayo Juni 15, 2025 Jijini Mbeya akisisitiza kuwa ni muhimu Wananchi na Viongozi waelewe majukumu ya mihimili ya dola na kuheshimu mipaka yake ili kulinda utawala wa Sheria na Demokrasia ya kweli

Soma https://jamii.app/RaisKuingiliaMahakama

#JamiiForums #JamiiAfrica #ConstituonalRights
1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antipas Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi leo Juni 16, 2025, ili kusikiliza kesi zinazomkabili

Ikumbukwe Juni 2, 2025 Mahakama iliagiza upande wa Jamhuri kuhakikisha unaharakisha na kutoa taarifa za mwenendo wa upelelezi wa kesi ya Uhaini ili shauri lianze kusikilizwa mapema

Soma https://jamii.app/KesiLissuKurindimaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
3
DAR: Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo ya karibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mashauri yanayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu, yanaendelea Mahakamani hapo

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa #CHADEMA wameshawasili Mahakamani kufuatilia kinachoendelea

Soma https://jamii.app/KesiLissuKurindimaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, #TunduLissu ambaye anakabiliwa na Kesi mbili kwenye Mahakama ya Kisutu amesema kwa siku 68 ambazo amekuwa Gerezani, amenyimwa haki ya kuzungumza kwa faragha na Mawakili wake ambao wamekuwa wakienda kuonana naye

Ameongeza kuwa licha ya hivyo yeye pamoja na Mawakili wake hawapati nafasi ya kubadilishana nyaraka kwaajili ya kushughulikia kesi zinazomkabili

Lissu akiwa kizimbani amesema amekuwa akizungumza na Mawakili kwenye simu akiwa eneo ambalo halimpi nafasi ya kufanya mazungumzo ya faragha, ambapo amesema kuwa, kupitia mawasiliano ya simu au eneo chumba anachotumia kuwasiliana na Mawakili wake kuna uwezekano wa kupokwa kwa Haki ya Faragha

Amesema mazingira ya aina hiyo ni kinyume na Sheria

Soma https://jamii.app/LissuNaMawakili

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025