JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mmoja wa Wadau wa JamiiForums.com anasema alishawahi kupanda Daladala za Madereva wanaokimbizana mpaka ikabidi aombe kushuka na kilometer kama moja mbele, alikuta Gari limepata Ajali huku Dereva na Kondakta wakiwa wamekimbia eneo la tukio

Vipi Mdau, nawe umeshawahi kupanda Daladala za Madereva wanaokimbizana, Ulifanyaje/Ulichukua hatua gani?

Mjadala zaidi https://jamii.app/DaladalaKukimbizana

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mtangazaji wa Clouds FM, Samuel Nathaniel Sasali ameeleza hawezi kuweka Picha/Video Mtandao za matukio ya harusi bila ruhusa ya Wahusika, akidai aliwahi kuitwa kuwa shahidi katika kesi iliyotokana na yeye kuposti tukio la Harusi ambapo baadaye ilibainika Bwana Harusi alikuwa na mke mwingine

Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekosoa matukio ya Watu kuchapisha picha na Video za Watu wengine Mitandaoni bila ridhaa yao, Washehereshaji (MC) nao walionekana kuwa moja ya kundi linaloongoza kwa kufanya vitendo hivyo

Februari 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia alisema “Ni muhimu kupata ridhaa ya mtu kabla ya kutumia taarifa zake binafsi, Washereheshaji wanaosambaza picha au video bila ridhaa wanakiuka Faragha ya Mtu.”

Soma https://jamii.app/SamSasali

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MTWARA: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ametoa kauli hiyo akijibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho kitatumia ili kuendana na ajenda ya 'No Reforms, No Election'

Lissu ameyasema hayo Aprili 7, 2025 wakati akihutubia Mkutano wa Hadhara Wilaya ya Masasi katika ziara ya kutoa elimu kuhusu 'No Reforms, No Election.'

Soma https://jamii.app/WananchiMkubalianeKuandamana

Video Credits: Mwanzo TV

#JamiiForums #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
2👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesema kitakwenda Mahakamani kuzishtaki Halmashauri mbalimbali Nchini kwa madai ya kushindwa kulipa stahiki za Walimu zaidi ya Tsh. Bilioni 12

Akizungumza na Waandishi wa habari, leo Aprili 08, 2025, Katibu Mkuu wa #CHAKAMWATA, Mwalimu Meshack Kapange amesema Halmashauri zinadaiwa na Walimu lakini hadi sasa hakuna malipo yoyote yaliyotolewa

Amesisitiza "CHAKAMWATA tumefuatilia kwa kina ili TAMISEMI itoe maelekezo kwa Mamlaka zake za chini lakini hakuna chochote kilichofanyika. Walimu wananyanyaswa kwa kuingiziwa makato ya Chama cha Walimu bila ridhaa yao, Walimu hatuko huru."

Soma https://jamii.app/CHAKAMWATAMadaiWalimu

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Eneo la Posta Barabara inayotokea kwenye Kanisa la KKKT kuelekea Karimjee kuna chemba zimepasuka zinatiririsha Majitaka, hali ni mbaya hasa kwa watembea kwa Miguu

Ameomba Mamlaka zitafute suluhu ya changamoto hiyo, kwasababu njia nzima imejaa Maji machafu hali ambayo inaleta kero na hofu ya Watu kupata Magonjwa, anatoa wito hatua zichukuliwe na Mamlaka husika

Soma https://jamii.app/MajitakaPosta

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability
👍2
Waandishi wa Habari wanapoishi kwa hofu ya mateso, kukamatwa au kudhulumiwa, ukweli unapozuiliwa na Demokrasia kudhoofika. Haki ya kusema ukweli inapaswa kulindwa na kuheshimiwa.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
UGANDA: Sehemu ya Wabunge kutoka Chama Tawala cha National Resistance Movement (NRM), Wabunge huru, na wa Upinzani wanaripotiwa kupokea kiasi cha Shilingi ya Uganda Milioni 100 (takriban Tsh. Milioni 70) kila mmoja kutoka kwa Rais Yoweri Museveni kama 'zawadi'

Gazeti la Monitor limeeleza kuwa Wabunge wa NRM walipokea pesa hizo kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Serikali Bungeni kati ya Saa mbili na Saa tatu Usiku Aprili 7, 2025 huku wengine wakiripotiwa kupokea kutoka katika makazi ya Spika, Anita Among, yaliyoko Nakasero

Inadaiwa Pesa hizo zilitolewa kama ishara ya shukrani kutoka kwa Rais kwa ajili ya "tabia njema" ya Wabunge hao, na pia kama mwitikio wa maombi yaliyotolewa na baadhi ya Wabunge waliokuwa wakikabiliwa na matatizo ya kifedha.

Soma https://jamii.app/MuseveniGifts100milion

#JamiiForums #AfricanPolitics
KILIMANJARO: Aliyekuwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Godfrey Malisa amewasilisha maombi Mahakamani akiomba uanachama wake ulindwe, ili afungue maombi ya kupinga mchakato wa kumteua Rais Samia kuwa mgombea Urais

Dkt. Malisa amewasilisha ombi hilo akiomba Mahakama itoe zuio la muda kwa lengo la kulinda hadhi ya Uanachama wake, wakati maombi yake ya kupinga uteuzi huo wa Rais yakiwa bado hayajafunguliwa

Katika maombi hayo, Dkt. Malisa ameishtaki Bodi ya Wadhamini ya #CCM na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro, ambayo ilitangaza kumfuta Uanachama, huku akidai anaweza kuthibitisha kuwa Katiba ya CCM na Utaratibu wa kumpata mgombea, Rais Samia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ulikiukwa na chama hicho.

Soma https://jamii.app/KupingaMgombeaUrais25

#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu2025
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akijibu hoja ya Mbunge Zahor Mohamed Haji aliyedai kuna dalili za Uvunjifu wa Amani kwa lugha za kejeli kuelekea kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Boniface Simbachawene amesema Serikali imejipanga na haipumziki

Amesema “Tumefanya Uchaguzi takriban mara Saba, kwa uzoefu huo Nchi yetu ni Mwalimu wa Demokrasia katika Kanda yetu, waliojiandaa kuleta fujo watambue Serikali haipumziki na imejipanga kusimamia Uchaguzi wa 2025.”

Soma https://jamii.app/BungeAprili9

#JamiiForums #Governance #Demokrasia #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema kuwepo kwa mazingira magumu yaliyogubikwa na nguvu kubwa za Vyombo vya Dola katika zoezi la Uandikishaji Wapigakura wapya Zanzibar ni kielelezo tosha kuwa Watawala hawapo tayari kutenda Haki licha ya kuwa ni mahodari wa kuhubiri Amani

Amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Chama Mkoa wa Kichama wa Micheweni katika Ukumbi wa Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba, Aprili 8, 2025

Soma https://jamii.app/NukuuOthman

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
DAR: Timu ya #Simba inaongoza kwa Magoli 2-0 dhidi ya Al Masry ya Misri katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Pili wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika unaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, magoli yakiwekwa wavuni na Elie Mpanzu na Steven Mukwala

Matokeo ya jumla mpaka sasa ni 2-2 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza Simba ilipoteza kwa Magoli 2-0 Nchini Misri

Soma https://jamii.app/SimbaAlMasry

#JFSports #JamiiForums #CAFCC
3
DAR: Timu ya #Simba imeendeleza rekodi yake ya kufanya kweli katika michuano ya kimataifa, hiyo ni baada ya kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa penati 4-1 dhidi ya Al Masry ya Misri kwenye Uwanja wa Mkapa

Dakika 90 zilikamilika kwa Simba kushinda Magoli 2-0 wafungaji wakiwa ni Elie Mpanzu na Steven Mukwala, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-2 kwa kuwa Robo Fainali ya kwanza Al Masry ilishinda 2-0

Hatua ya Nusu Fainali, Simba inatarajiwa kukutana na mshindi kati ya Zamalek (Misri) dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini

Soma https://jamii.app/SimbaAlMasry

#JFSports #JamiiForums #CAFCC
3👏2
RUVUMA: Kwa mujibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kupitia Ukurasa wao wa Mtandao wa X, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, #TunduLissu amekamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Mbinga

Taarifa hiyo imeeleza Lissu amekamatwa wakati alipomaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo Aprili 9, 2025 pamoja na Wanachama wengine kadhaa na kwamba bado hawajafahamu wamepelekwa Kituo gani cha Polisi

Soma https://jamii.app/LissuAkamatwaRuvuma

#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa
1
Mifumo ya udhibiti inayotumika kudhibiti taarifa Mtandaoni inaweza kutumiwa kuzuia taarifa muhimu, kupunguza upatikanaji wa taarifa huru, na kuzuia sauti za Wananchi kutoka kwenye majukwaa ya Kidijitali.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
TABORA: Mdau wa JamiiForums.com anasema akiwa katika safari zake alipita Urambo katika Stendi ya Wilaya ambapo alishangazwa na mwonekano wa Kituo hicho, Mazingira yake sio mazuri na kudai kimekaa 'local'

Anaeleza "Tuliposhuka kupata Huduma ya Vyoo kwa Wanaume, tulilipa ila nako tukakuta hali siyo nzuri, usafi hauzingatiwi na inavyoonekana hapafanyiwi usafi vizuri jambo ambalo ni hatari kwa Afya. Natoa wito Mamlaka husika kuchukua hatua kuweka Mazingira vizuri."

Soma https://jamii.app/UduniStendiUrambo

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery
👍1