JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya #CHADEMA, Godbless Lema kupitia Akaunti yake kwenye Mtandao wa X ameandika kuwa wameshambuliwa kwa mabomu ya machozi walipokuwa katika ofisi za chama hicho, Songea, eneo ambalo walitarajiwa kufanya mkutano wao leo Aprili 10, 2025

Upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia kuhusu tukio hilo amezungumza na JamiiForums na kusema "Polisi wamevamia mkutano wetu na Wanahabari, wameondoka na Viongozi wetu kadhaa wakiwemo Makamu Mwenyekiti, John Heche na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema.”

Amesema Polisi imewachukua kwa ajili ya mahojiano, alipoulizwa sababu za wao kuzuiwa kufanya mkutano na Wanahabari ambao ulipangwa kufanyika asubuji ya leo, amesema Polisi hawajatoa sababu yoyote

Jitihada za JamiiForums kutafuta upande wa Jeshi la Polisi Mkoa zinaendelea

Soma https://jamii.app/CHADEMAKuvamiwaSongea

#JamiiForums #Demokrasia #KuelekeaUchaguzi2025 #HumanRights
👍1
DAR: Aprili 8, 2025, Mdau wa JamiiForums alieleza kuwa eneo la Posta Barabara ya Kanisa la KKKT kuelekea Karimjee kuna chemba zimepasuka na kutiririsha majitaka, Mamlaka zimechukua hatua kwa kushughulikia utengenezaji wa miundombinu hiyo ambapo kwa sasa majitaka hayo hayatiririki

Soma https://jamii.app/ChembaKurekebishwa

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
MAREKANI: Rais #DonaldTrump, siku ya Jumatano Aprili 9, 2025 alisitisha ghafla ushuru wa Forodha kwa Nchi nyingi kwa kipindi cha Siku 90, na kuongeza zaidi kiwango cha ushuru kwa Bidhaa kutoka China hadi kufikia 125%

Hatua hiyo imeonekana kuwa jaribio la kupunguza Mvutano wa Vita ya Kibiashara ambayo haijawahi kushuhudiwa kati ya Marekani na Mataifa mengi Duniani, na kulenga zaidi mzozo kati ya Marekani na China

Wakati Hisa na Dhamana za Serikali zikiuzwa kwa wingi, Wananchi wanashuhudia Akiba zao za kustaafu zikipungua, huku Biashara zikiashiria mauzo duni kuliko matarajio na kupanda kwa bei.

Soma https://jamii.app/TrumpTariffs90Days

#JamiiForums #Governance #TariffWar #TrumpTarrifs
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Safia Jongo ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa amesema hakuna raia yeyote akiwemo Askari Polisi anayeruhusiwa kumpiga Mtu bali anatakiwa amueleze kosa lake kisha amfikishe Kituo cha Polisi

Ametoa kauli hiyo wakati wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii yaliyotolewa kwa Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa wenye viti na Maafisa Tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa Wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Soma https://jamii.app/AskariKumpigaMtu

Video Credits: Star TV

#Accountability #Uwajibikaji #HumanRights #JamiiForums
1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UWAJIBIKAJI: Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Kenani amehoji hatua ya Serikali kumkamata Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na kuitaka itoe maelezo kuhusu sababu za kukamatwa kwake

Amesema hayo leo Aprili 10, 2025 akiwa Bungeni Dodoma

Soma https://jamii.app/KukamatwaTunduLissu

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Gaston Garubindi amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Tundu Lissu amefikishwa Kituo cha Polisi kati (Central) na tayari amehojiwa na Ofisi ya Upelelezi ya Kanda Maalumu

Amesema Lissu amehojiwa kwa tuhuma mbili ambazo ni Uhaini na kutoa taarifa za uongo huku ikielezwa atafikishwa Mahakamani ndani ya Saa 48

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2024 Wilayani Mbinga wakati alipomaliza mkutano wa hadhara pamoja na Wanachama wengine kadhaa

Soma https://jamii.app/LissuUhainiCentral

#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu mnamo Aprili 9, 2025 katika Mtaa wa Soko Kuu, Wilaya ya Mbinga kwa kosa la kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025

Taarifa imetoa onyo kwa Vyama vya Siasa kutoa maneno ya uchochezi na Kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu

Aidha, taarifa ya Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Gaston Garubindi imesema Tundu Lissu amefikishwa Kituo cha Polisi Kati (Central) na tayari amehojiwa na Ofisi ya Upelelezi ya Kanda Maalumu kwa tuhuma mbili ambazo ni Uhaini na Kutoa Taarifa zilizokuwa zinapelelezwa za kufanya Uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025

Soma https://jamii.app/LissuKukamatwaUchochezi

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #Demokrasia #Accountability #KuelekeaUchaguzi2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, #TunduLissu amefikishwa Mahakama ya Kisutu baada ya kuhojiwa na Ofisi ya Upelelezi Kanda Maalumu, ambapo Mkurugenzi wa Sheria #CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi alinukuliwa akisema anatuhumiwa kwa tuhuma za Uhaini na kutoa taarifa za uongo

Taarifa zaidi ya kinachoendelea Mahakama zitafuata

Soma https://jamii.app/LissuKisutuApr10

#JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #TunduLissu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la Uhaini

Lissu amefikishwa Mahakama hiyo leo Aprili 10, 2025 na kusomewa shitaka hilo huku kesi ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025

Ikumbukwe Lissu alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/KesiLissuKuhairishwa

#JamiiForums #HumanRights #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Usafiri wakiwemo wamiliki wa malori, Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania na Mawakala wa Forodha Wilayani Tunduma wamedai changamoto ya foleni iliyopo mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma inatengenezwa na Watu kwa maslahi yao binafsi

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo amesema ameunda Kamati Maalumu kuchunguza na kubaini sababu kwa kuwa suala hilo limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara

Ikumbukwe, Oktoba 1, 2023, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Serikali ina mkakati gani wa kuondoa foleni ya malori Tunduma”, pia Mei 31, 2025, Mdau mwingine aliandika “Mifumo ya Kikodi katika Mpaka wa Tunduma ni tatizo, inasababisha foleni kubwa. Kwanini Tanzania haitumii mfumo sawa na Zambia?”

Soma https://jamii.app/TundumaFoleni

#Accountability #Uwajibikaji #JamiiForums #ServiceDelivery
Kwa kutoa taarifa za ukweli na kuandika Habari bila Upendeleo, Vyombo vya Habari hufungua Macho ya Wananchi na husababisha shinikizo kwa Viongozi na Taasisi kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya kifisadi

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
UCHUMI: Mwaka 2024, bidhaa kubwa zilizouzwa kutoka Marekani kwenda China zilikuwa Maharage ya Soya – ambayo hutumika hasa kulisha Nguruwe Milioni 440 Nchini China. Marekani pia ilisafirisha Dawa na Mafuta ya Petroli kwenda China

Kutoka China kwenda Marekani, kulikuwa na wingi wa Vifaa vya Kielektroniki, Kompyuta na Vitu vya Kuchezea (Toys). Idadi kubwa ya Betri, ambazo ni muhimu kwa Magari ya Umeme, pia zilisafirishwa kutoka China.

Aidha, wakati Maumivu ya Ushuru yakitarajiwa, China imetoa msamaha wa Ushuru kwa Asilimia 100 kwa Nchi 33 za Afrika kwa Bidhaa zao zote zinazoingia kwenye Soko la Nchi hiyo.

Fahamu zaidi https://jamii.app/TrumpvsChinaTZ

#JamiiForums #Tariffwar #TrumpRecession #TrumpTariffs
1
DAR: Mshereheshaji, Anthony D. Luvanda akihojiwa na Clouds FM Machi 18, 2025, alisema Tasnia hiyo imekuwa ikivamiwa na Watu wengi ambapo wapo wanaofanya vitu kinyume cha Sheria na kukiuka faragha za Watu kwa kuchapisha picha na video ambazo zinadhalilisha Utu

Soma https://jamii.app/NukuuLuvanda

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka hususani TAMISEMI kufuatilia changamoto iliyopo katika Shule ya Misingi Kitonga, Ilala ya Wanafunzi kuwa wengi kuliko Miundombinu ili kuona namna bora ya kuitatua na kupunguza msongamano wa Wanafunzi

Aidha, Mdau anadai Wanafunzi wengi wamekuwa wakipata changamoto kufika Shuleni hasa kipindi cha Mvua kutokana na Miundombinu mibovu ya Barabara inayotumika kuelekea kwenye Shule hiyo

Soma https://jamii.app/KitongaShule

#JamiiForums #Accountability #Elimu #Governance
RUVUMA: Mdau anadai uchakavu wa madarasa katika Shule ya Msingi Lipepo, Kata ya Nalasi, Tunduru Kusini umesababisha Wanakijiji kujichanga na kuanza ujenzi wa Darasa 1 lakini nguvu zao ziliishia njiani, wakaahidiwa kuongezewa nguvu na Kiongozi wao lakini hilo halijatimia

Mdau ametoa wito kwa Wadau mbalimbali na Serikali kuwasaidia kuboresha Vyoo na kuwajengea miundombinu mipya ya Madarasa

Soma https://jamii.app/ShuleYaLipepo

#JamiiForums #ServiceDelivery #PublicHealth #Elimu