JamiiForums
โœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ikiwa tunataka maendeleo ya kweli, Vyama vya Siasa vinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Wanawake kwa vitendo, kwa kuhakikisha kuna sera madhubuti za kuendeleza Uongozi wa Wanawake, kuwapa nafasi za kugombea bila vikwazo, na kupinga mifumo kandamizi inayowazuia

Katika kuelekea uchaguzi, tunapaswa kuhoji, Je, wanawake ndani ya Vyama vya Siasa wanapewa nafasi za kugombea au wanatumiwa tu kama wapiga kura?

#JamiiForums #UsibakiNyuma #ThubutuGombeaOngoza #JFWomen #WomenInPolitics #Democracy #GenderBalance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali imejipanga kuendelea kuwa na hifadhi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya UKIMWI ambapo pia amewataka Vijana kutambua ugojwa huo bado upo na waendelee kuchukua tahadhari

Ameyasema hayo wakati anazungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Machi 1, 2025

Soma https://jamii.app/MsigwaKuhusuARV

#JamiiForums #PublicHealth #JFMatukio
๐Ÿ‘2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe, Askofu Dkt. Benson Bagonza akizungumza na MwanaHabari amesema suala la utekaji na Watu kupotea siyo dalili nzuri kwa Taifa na kueleza kuwa kuna mambo ya kuligawa Taifa yanaendelea kufanyika Nchini

Soma https://jamii.app/BagonzaMahojiano

Video Credits: MwanaHabari

#JFMatukio #Siasa #JamiiForums
Uhuru wa Kujieleza ni msingi wa Haki nyingine nyingi na unapodhoofishwa, Uhuru wa Watu Kukusanyika, Kuandamana au Kuabudu unakuwa hatarini pia

Mfano: Ikiwa Watu hawawezi Kujieleza kwa Uhuru, hawataweza kuunda au kujiunga na vikundi vya kutetea maslahi yao (Uhuru wa Kukusanyika)

#SautiYetuUhuruWetu #JamiiForums #DemocracyMatters #FreedomOfSpeech #HumanRights
๐Ÿ‘1๐Ÿ”ฅ1
DAR: Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema uwepo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari hauna lengo la kufanya Watu wazuiwe kuingia katika tasnia hiyo bali inalenga kupatikana kwa Huduma bora

Akizungumza katika Uzinduzi wa Bodi hiyo, leo Machi 3, 2025, Msigwa amesema โ€œUtafiti tulioufanya hivi karibuni tulibaini Vyuo vyetu vinazalisha zaidi ya Waandishi wa Habari 500 kila Mwaka. Kusoma ni jambo moja lakini Watu hao wanahitaji kujengewa uwezo ili kuwa na ubora wa kufanya kazi iliyo bora.โ€

Ameongeza โ€œHiyo inaonesha kuna ongeko la Vijana katika tasnia na wengi wao wana Shahada ya Habari, unadhani watakwenda wapi? Hivyo, uwepo wa Bodi ya Ithibati utasaidia wawe bora na kinachozalishwa kiwe bora pia. Kama Vyuo vinazalisha, unadhani wakitoka hapo watakwenda wapi? Lazima tushirikiane kuwasaidia.โ€

Soma https://jamii.app/BodiYaIthibati

#PressFreedom #JFMatukio #Accountability #JamiiForums
๐Ÿ‘1
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Malaysia juu ya juhudi za Serikali kudhibiti nafasi ya Kidigitali na kuzuia Uhuru wa Kujieleza hasa kwa Waandishi wa Habari ilidhihirishwa na Muswada wa Usalama Mtandaoni wa Mwaka 2024

Kupitia mradi wa 'Sinar' ambalo ni shirika lisilo la Kiserikali waligundua madhara yatakayojitokeza na kuchapisha ripoti za kimataifa ambazo zilichochea uhamasishaji nchini humo ambapo Wataalamu wa IT na wajasiriamali waliwasilisha pingamizi juu ya mabadiliko ya Muswada huo kwa Serikali

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Boniface Simbachawene, akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Umma kushughulikia vibali vya uhamisho ili kuokoa Familia nyingi za Watumishi

Ameyasema hayo leo Machi 3, 2025 katika Kikao Kazi cha Waziri wa Utumishi na Wakuu wa Taasisi

Ikumbukwe, Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto ya Mfumo wa Uhamisho wakidai umekuwa kero kwao kwa maelezo kwamba licha ya kuwa ni wa Mfumo wa Mtandaoni (Online) lakini wahusika wanaotakiwa kupitisha wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa Waombaji wa Uhamisho

Soma https://jamii.app/FamiliaZinakufaUhamisho

#JamiiForums #Governance
Mdau wa Jukwaa la Siasa ndani ya JamiiForums.com ameanzisha Mjadala kuhusu Wizi wa Kura kuua 'morali' ya Wapigakura katika chaguzi Nchini

Amesema ili kuongeza ushiriki wa Raia katika masuala ya Uchaguzi, sanduku la kura liheshimiwe. Wapigakura waheshimiwe na atangazwe waliyemchagua, sio vinginevyo

Unakubaliana na hoja zake?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WiziWaKuraVsWapigaKura

#JamiiForums #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #Accountability #FreeAndFairElection
๐Ÿ‘1
DAR: Muda mfupi baada ya Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari kuzinduliwa leo Machi 3, 2025 imeelezwa huo ni mwanzo wa kuwaondoa Waandishi Makanjanja kwenye tasnia ya Habari na kuwa kuna dalili za kuporomoka kwa Uandishi wa Habari Nchini

Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati, Tido Mhando, amesema โ€œTunachokisikia na kukiona kwenye Vyombo vya Habari ni mambo yaleyale kila Siku yanayozungumzwa na wakati mwingine yanakinaisha. Kuna dalili za kuporomoka kwa kiwango cha Uandishi wa Habari tofauti na ilivyokuwa Miaka ya nyuma.โ€

Ameongeza, kuporomoka kwa Maadili ya Waandishi wa Habari kunatokana na kukosekana kwa usimamizi wa Taaluma hiyo na kueleza Bodi itasimamia miongozo iliyopo ili kutekeleza majukumu yake kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Waandishi wengi wa Habari hapa Nchini

Soma https://jamii.app/BodiYaIthibati

#PressFreedom #JFMatukio #Accountability #JamiiForums
โค1๐Ÿ‘1
Mdau umewahi kutapeliwa Mtandaoni, ilikuwaje na ulichukua hatua gani baada ya tukio hilo?

Mjadala Zaidi https://jamii.app/UtapeliMtandaoBasi

#JamiiForums #UtapeliMtandaoni #BewareOfScams #CyberSecurity #DigitalSafety #KataaUtapeliMtandaoni #KuwaMachoNaUtapeli
Unakubaliana na hoja za Mdau? Umewahi kupandishiwa kodi au kuongezewa gharama ya kitu baada ya mwenye mali kushawishiwa na dalali?

Mjadala https://jamii.app/BeiMadalali

#JamiiForums #Biashara #Udalali #Maisha
๐Ÿ‘1
DEMOKRASIA: Vyama vya Siasa vina jukumu kubwa katika kuhakikisha Usawa wa Kijinsia kwenye Uongozi wa Kisiasa, ikiwemo kuweka Mazingira rafiki kwa Wanawake kushiriki katika shughuli za Siasa bila hofu wala ubaguzi

Vyama vinapaswa kuhakikisha Wanawake wanapata nafasi sawa za kugombea, kushiriki maamuzi na kupewa nafasi za Uongozi

#JamiiForums #UsibakiNyuma #ThubutuGombeaOngoza #JFWomen #WomenInPolitics #Democracy #GenderBalance
Vyombo vya Habari vina jukumu muhimu katika kuimarisha ushiriki wa Wanawake katika #Siasa kwa kusambaza maudhui sahihi na jukwaa la usawa, kuangazia changamoto wanazokumbana nazo, na kusimulia mafanikio yao badala ya kueneza maudhui kandamizi.

Hata hivyo, mara nyingi maudhui yanayoenezwa huendeleza mfumo dume, kudhalilisha au kudhoofisha jitihada za #Wanawake katika Uongozi.

Kuelekea Uchaguzi wa 2025, ni wakati wa Vyombo vya Habari kuhakikisha kuwa vinatumika kujenga, kuwezesha, na kuleta mabadiliko chanya kwa usawa wa kijinsia katika uongozi wa Kisiasa Nchini

#JamiiForums #UsibakiNyuma #ThubutuGombeaOngoza #JFWomen #WomenInPolitics #Democracy #GenderBalance
LINDI: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi - Nachingwea (MANAWASA) imejibu hoja ya Mdau wa JamiiForums.com kuhusu uhaba wa Maji Nachingwea kwa kusema mahitaji ya maji ni Lita 6,000,000 kwa siku wakati uzalishaji unaofanyika kwa siku ni Lita 3,000,000

Changamoto nyingine inayosababisha uhaba ni kupasuka mara kwa mara kwa bomba kubwa linaloleta maji Nachingwea kutokea kwenye tanki la usambazaji maji Chiliogoli ambapo kumesababisha kupunguza uzalishaji maji

Mkurugenzi Mtendaji wa #MANAWASA, Kiula Makalla Kingu amesema mpango uliopo ni kutekeleza Mradi wa Tsh. Bilioni 2.9 kubadilisha bomba kubwa ambalo limekuwa likipasuka mara kwa mara, hatua za awali za manunuzi zimeshakamilika na kwa sasa wanaendelea na kutoa maji kwa wateja wake kwa njia ya mgao

Soma https://jamii.app/NachingweaMaji

#JFHuduma #JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery