JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akihojiwa na Azam TV kuhusu maamuzi yanayofanywa na Rais wa Marekani, #DonaldTrump, ikiwemo Sera za kusitisha baadhi ya misaada kwa Nchi za Afrika, Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amesema hiyo ni inaweza kuwa fursa kwa Afrika

Kafulila amesema moja ya njia ya kujiweka sawa ni kupunguza matumizi ya kodi na mikopo katika maeneo yanayoweza kufanywa na Sekta Binafsi, moja ya sehemu ambayo ilikuwa na sapoti ya Marekani ili kunufaisha sekta mbalimbali kama Elimu, Afya au Maji ambazo zilikuwa zinapata msaada wa Marekani au Benki ya Dunia

Soma https://jamii.app/KafulilaTrump

#Uchumi #JFEconomy #Accountability #Governance
👍2
TABORA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka katika Wilaya ya Uyui kushughulikia ujenzi wa paa la Jengo la Walimu katika Shule ya Msingi Nsololo, kwani Walimu wanalazimika kukaa chini ya Mti ili kusubiri kuingia madarasani

Soma https://jamii.app/WalimuKukaaChiniYaMiti

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki ameomba ushauri wa nini cha kufanya baada ya kujenga nyumba kwa siri bila kumshirikisha mumewe

Je, una ushauri gani kwa Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/HanishirikishiMamboYake

#JamiiForums #LifeStyle
Mwanachama wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala huu akitoa Shukrani na Pongezi (Maua) kwa Wanaume hasa wale wanaojituma na hawapati "ASANTE" wanazostahili

Nawe unatuma 'Maua' gani kwa Wanaume waliopo kwenye Maisha yako?

Unaweza kushiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/MauaWanaume

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories
MWANZA: Timu ya #Yanga inaendelea kuonesha haina utani linapokuja suala la kuutafuta Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hiyo ni baada ya kuifunga Pamba Jiji Magoli 3-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na hivyo kuendelea kujikita kileleni katika msimamo

Magoli ya Chadrack Boka (29) na Ki Aziz (75 na 77) yanaifanya Yanga kufikisha alama 58 katika mechi 22, ikiiacha #Simba kwa pointi 7 ambapo ina alama 51 katika michezo 20 ikishika nafasi ya pili

Matokeo hayo ni mabaya kwa Pamba Jiji ambayo imesaliwa na alama 22 katika michezo 22 ikiwa nafasi ya 13 kati ya timu 16, hivyo inapambana kutoshuka Daraja

Soma https://jamii.app/PambaYanga

#JFSport #JamiiForums #JFLigiKuu25
👍1
Kupiga kura si tendo dogo, ni hatua muhimu ya kujenga Jamii tunayoitaka.

Kila mtu anapofanya jukumu lake, tunapata nguvu ya pamoja inayoweza kuleta mabadiliko halisi.

#KuraYakoSautiYako #HakiYaKupigaKura #HakiZaKiraia #CivilRights #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #SautiYakoNguvuYako #Demoracy
KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com anasema baada ya Duka la Dawa (MSD) katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kufungwa, sasa Wagonjwa na Wananchi wengi wenye uhitaji wanalazimika kwenda kwenye Maduka ya Watu Binafsi yaliyopo nje ya Hospitali kupata Dawa

Ametoa wito kwa Mamlaka husika kurejeshw Duka la MSD kwani ni tegemeo na msaada mkubwa, hususani kwa Wananchi ambao hushindwa kumudu gharama za Dawa kwenye Maduka binafsi

Soma https://jamii.app/MSDMpandaDuka

#Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
2👍1
MAREKANI: Rais wa Marekani, Donald Trump amesitisha takriban progamu 5,800 zilizokuwa zinafadhiliwa na mradi wa USAID ikiwemo misaada kwa Wakimbizi, Matibabu ya Kifua Kikuu, Malaria, UKIMWI na Chanjo ya Polio

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani imeelezwa kuwa Miradi hiyo imesitishwa kwa Maslahi ya Serikali ya Marekani

Soma https://jamii.app/TrumpUNAIDSProgramme

#JamiiForums #Diplomacy #Governance
👍3