JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com anasema katika zama hizi hakuna haja ya kuwekeza pesa nyingi kwenye elimu rasmi, badala yake Wazazi wawekeze kwenye kuwapatia Watoto ujuzi mbalimbali, ili waweze kujiajiri badala ya kusota wakisubiri ajira

Unakubaliana na hoja za Mdau?

Mjadala https://jamii.app/AjiraAfterChuo

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #LifeTips
👍1
KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Kata ya Buhembe - Manispaa ya Bukoba, amelalamikia kero ya ukosefu wa huduma ya Maji Safi katika Kata yao na maeneo ya jirani licha ya Serikali kujenga na kuzindua tanki kubwa la Maji

Mdau ametoa wito kwa Mamlaka husika kutatua changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/BuhembeKukosaMaji

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFMdau2025 #AccessToInformation #Uwajibikaji #PublicHealth #Afya
👍1
Kila Mtu anayeshtakiwa kwa kosa lolote ana Haki ya kusikilizwa kwa Haki mbele ya Mahakama huru na isiyo na upendeleo

Usawa mbele ya Sheria unahakikisha kuwa hakuna Mtu anayepaswa kubaguliwa kwa misingi ya Rangi, Jinsia, Dini, Hali ya Kiuchumi au Kijamii. Haki hizi si fadhila za Serikali, bali ni Haki za msingi ambazo zinapaswa kulindwa kwa kila Mtu.

#HakiKwaWote #UsawaMbeleYaSheria #Demokrasia #HakiZaKiraia #JamiiForums #Accountability #CivilRights #Democracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SINGIDA: Mbunge wa Viti Maalum, Jesca Kishoa, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika huko Nkalakala, Wilayani Mkalama, Februari 16, 2025 amesema kuna Kiongozi wa Kisiasa alimwambia "Jesca, tunza fedha zako, cheza na wajumbe. Unatumia njia ndefu mno. Kipenga kikipulizwa, zitumie kuwahonga Wajumbe ikiwa utagombea kupitia CCM au Chama chochote.’”

Zaidi https://jamii.app/HongoWajumbe

Video Credits: Jambo TV

#JamiiForums #Uwajibikaji #Demokrasia #Democracy #KemeaRushwa25 #ChaguaKiongoziSioPesa
DODOMA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia kero ya foleni na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Ardhi

Soma https://jamii.app/FoleniOfisiArdhiDodoma

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
1👍1
DAR: Timu ya #Yanga imeendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Singida Big Stars kwenye Uwanja wa KMC kwa Magoli 2-1

Wafungaji wa Yanga ni Clement Mzize dakika ya 14 na Prince Dube dakika ya 43 wakati wageni wamepata goli lao dakika ya 90+2 kupitia kwa Jonathan Sowah

Yanga imefikisha alama 52 katika michezo 20, Singida imesaliwa na pointi 37 ikiwa nafasi ya nne katika michezo 20. Nafasi ya pili ipo Simba ikiwa na alama 47 michezo 18, Azam FC michezo 19 pointi 42

Zaidi https://jamii.app/Yanga2Singida1

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo amesema matukio ya Mauaji, imani za kishirikina, Ubakaji na Ulawiti yameendelea kuwa yakiripotiwa mara kwa mara Mkoani hapo jambo ambalo anaeleza linatakiwa kupigwa vita

Amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Wananchi Wilaya ya Mbozi

Soma https://jamii.app/RCSongwe

#JamiiForums #HakiZaBinadamu #HumanRights #HakiZaKiraia #CivilRights #UtawalaWaSheria
👍2
Viongozi wanaopatikana kwa kununua kura hawawezi kutanguliza maslahi ya Wananchi. Wanakuwa na deni kwa waliowafadhili badala ya kuwajibika kwa wapigakura. Matokeo yake? #Rushwa, matumizi mabaya ya Rasilimali, na maamuzi yanayoathiri maendeleo ya jamii.

Tujifunze kwenye historia, Kiongozi anayenunua Uongozi hawezi kuwa na dhamira safi ya kutumikia Wananchi. Uchaguzi ni fursa ya kuamua hatma yetu. Tuchague kwa Akili, si kwa pesa

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo amewataka Wakazi wa Wilaya ya Mbozi kuacha kuwatumikisha Watoto katika kazi za shambani badala yake wawapeleke Shule ili wapate elimu itakakayowasaidia kujiandaa na ushindani wa Soko la Ajira

Januari 4, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alidai kuna tabia ya kutumikisha Watoto katika kazi za shamba Wilayani hapo na kueleza hata baadhi ya Walimu wamekuwa wakiwatumia Wanafunzi wao kulima katika mashamba yao binafsi

Akaeleza kuna Watoto wengi ikifika Januari wanatega kwenda shule kwa kuwa ni msimu wa kilimo wakikwepa kutumikishwa, akatoa wito kuwa kama ni mafunzo ya vitendo yafanyike kwenye mashamba ya Shule, pia akasema wengine wanakosa masomo kwa kuwa wanatumikishwa na Familia zao muda waliotakiwa kuwa Shule

Soma https://jamii.app/ChongoloMbozi

#JFMatukio #ChildRights #JamiiForums #SocialJustice #Accountability #Governance
Katika ulimwengu wa kidijitali ili kulinda taarifa zako binafsi na faragha kumbuka kujilinda mtandaoni kwa kusasisha vifaa vyako kama simu na kompyuta mara kwa mara ili kupunguza hatari ya uvunjaji wa usalama na kuhakikisha taarifa zako zinakuwa salama.

Soma https://jamii.app/MlinziTaarifaZako

#JamiiForums #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako