JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kupitia Jukwaa la Habari na Hoja mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, Mwanachama anaomba Ushauri baada ya kufunguliwa Kesi ya Madai kutokana na Mtu aliyemdhamini kupata Mkopo 'kuingia Mitini' wakati wa marejesho

Anaomba Ushauri afanyeje au Msaada wa Kisheria wa namna ya kuepuka janga lililompata

Tembelea https://jamii.app/DhamanaMkopoKesi

#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFStories #JFChitChats
👍1
Unakubaliana na Mdau au wewe huwa unafanyaje pale baadhi ya Watu wanapoondoka kwenye Maisha yako?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MwacheAende

#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFStories #JFChitChats
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Jeshi la Polisi limesema linafanya uchunguzi wa madai ya kutekwa kwa Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo (30) ambaye ameripotiwa kupotea tangu Februari 14, 2025 huko Misungwi

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Audax Majaliwa amesema hakuna yeyote aliyeweza kuthibitisha alipo Manengelo ikiwemo Ndugu na Jamaa zake huku akitoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa zozote zitakazosaidia katika upatikanaji wa Manengelo

Inadaiwa Manengelo alichukuliwa na Watu wanne akiwa Nyumbani kwa rafiki yake, Jovin Thomas (32) ambaye ni Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Misungwi

Soma https://jamii.app/PolisiKutekwaBavicha

#JamiiForums #HumanRights #Governance
👍1
#DIPLOMASIA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio na Waziri wa Urusi, Sergey Lavrov wamekutana leo, Februari 18, 2025 nchini Saudi Arabia ili kujadili namna watakavyoboresha mahusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na kumaliza Vita ya Ukraine na Russia

Mazungumzo hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza toka vita hiyo ilipoanza huku Ulaya na Ukraine zikiwa hazijashirikishwa katika mazungumzo haya na Rais Volodymyr Zelenskyy amesema hatakubali matokeo ya mazungumzo hayo kutokana na nchi yake kutokuwepo

Soma https://jamii.app/VitaUkraineMazungumzo

#JamiiForums #Diplomasia
👍2
Kwenye Shindano la Stories of Change 2023, Mshiriki huyu aliwasilisha Andiko linaloelezea Nchi ya Kusadikika ambayo Walimu wengi wanaitamani kuishi ndani yake wakifanya kazi hiyo ya Ualimu

Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/NchiMwlKusadikikaSOC23

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #SOC2023 #Accountability
👍1
Kila Mtoto ana Haki ya kupata Elimu bora bila ubaguzi wa aina yoyote. Elimu si kwa ajili ya wachache wenye uwezo wa kumudu gharama, bali ni Haki ya kila Mtoto, bila kujali hali yake ya Kiuchumi

Uwekezaji ufanyike kuhakikisha Shule zinakuwa na Rasilimali za kutosha, kuwasaidia Watoto walio katika Mazingira magumu wapate Elimu pamoja na Kupigania sera zinazowekeza katika Elimu kwa wote

#ElimuNiHaki #MtotoKwanza #Demokrasia #JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #Democracy #ElimuKwaWote
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022, Kifungu cha 7 (c) majukumu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni pamoja na kupokea, kuchunguza na kushughulikia malalamiko kuhusu madai ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu

Soma https://jamii.app/TaarifaBinafsiMatumiziMabaya

#JamiiForums #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesaini mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (#TEMESA) unaogharimu Tsh. Milioni 514 wa usimikaji wa mifumo ya kamera za ulinzi katika barabara na maeneo ya Kariakoo ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa Saa 24

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema lengo ni kuimarisha usalama wa Wananchi na Wafanyabiashara na kuongeza ufanisi wa shughuli za kibiashara katika kusaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu na kutoa ushahidi wa haraka inapohitajika

Soma https://jamii.app/KameraMasaa24Kariakoo

#JamiiForums #Accountability #Governance #ServiceDelivery
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MANYARA: Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amevitaka Vyama vya Upinzani kuacha visingizio na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 akisema kuwa mafanikio aliyoyafanya Rais Samia Suluhu yanatosha kuipa CCM ushindi

Ameyasema hayo leo, Februari 18, 2025 katika ziara yake ya siku 4 Mkoani Manyara, alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM Wilayani Kiteto

Soma https://jamii.app/VyamaPinzaniUchaguzi2025

#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu25
👎1