JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kila unapokubali pesa au ahadi za kifedha ili kumpigia mtu kura, unatoa kibali kwa viongozi wasiostahili kuingia madarakani, matokeo yake Wananchi wanabaki wakilalamikia huduma duni za afya na Elimu, miundombinu mibovu na ukosefu wa ajira

Rushwa ya uchaguzi ni mzigo wa muda mrefu kwa jamii nzima. Thamani ya kura yako ni kubwa zaidi kuliko noti wanazotumia kukuhadaa.

Chagua Viongozi waadilifu, wenye maono na uwezo wa kusimamia rasilimali za taifa kwa manufaa ya wote

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
DAR: Shahidi wa kesi inayomkabili Saleh Ayoub (39), Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres amesema Mtoto (jina linahifadhiwa) alimueleza kuwa Mwalimu Saleh alikuwa anamtoa darasani na kumpeleka kwenye chumba kisicho na matumizi wakati mwingine kwenye choo kisha kumuingilia

Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa ameahirisha shauri hilo linalosikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni hadi Februari 26, 2025 huku akisisitiza anataka mashahidi wawili ndani ya mwezi huu ili kuepuka shauri hilo kucheleweshwa

Ikumbukwe, Shauri hilo lilifikishwa Mahakamani siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji sababu za kutofikishwa Mahakamani kwa Watuhumiwa aliodai wanahusika na vitendo vya ukatili katika Shule hiyo

Soma https://jamii.app/GreenAcresFeb18

#JamiiForums #CivilRights #Justice #Governance #ChildRights
👍2
DAR: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefafanua kuhusu ufungaji wa kamera za usalama (CCTV Camera) katika barabara na maeneo ya Kariakoo ambapo imesema mradi huo utagharimu Tsh. Milioni 514 kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa biashara eneo la Kariakoo na Barabara Kuu zinazoingia na kutoka katikati ya Jiji

Taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Elihuruma Mabelya imeeleza mchakato wa mradi huo utahusisha Usimikaji / Ujenzi wa Fiber Optic eneo lote la CBD, Servers (zenye uwezo mkubwa), ujenzi / usimikaji wa Mfumo kwenye Control Rooms (zipo control Rooms mbili)

Nyingine ni Networking, Modern Back up System, Earth works na kuwa Awamu ya Kwanza kamera zitakazofungwa ni 40 pamoja na supporting Systems

Soma https://jamii.app/KameraKariakoo

#JamiiForums #Accountability #Governance #ServiceDelivery
Mwanachama wa JamiiForums.com anashauri hata kama unampenda Mtu/Ndugu/Rafiki kwa kiwango kikubwa kiasi gani lakini ni vema kuweka mipaka ya mambo gani unaweza kuyavumilia kutoka kwake ili kujijengea Heshima

Anasema kuishi na Mtu yeyote sio jambo rahisi sababu ya Utofauti wa Tabia na Malezi lakini hilo lisikufanye ukahatarisha Furaha na Amani yako kwa lengo la kumfurahisha Mtu mwingine

Kujifunza mengi zaidi bofya https://jamii.app/MaudhiMipakaWatu

#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFStories #JFChitChats
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Mkuu wa Mkoa, Paulo Chacha amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Tabora, Mayala Mburi kutokana na tuhuma za kutukana Wateja (Akiwemo Mtumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu) waliokwenda kupata huduma za mafuta

Maagizo hayo yalitolewa wakati RC Chacha alipotembelea Ofisi za GPSA mkoani Tabora Februari 18, 2025, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa

Aidha, Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora, Mayala Mburi akijibu tuhuma hizo ameeleza kuwa alikuwa amelewa na ndio ilisababisha kutoa lugha za matusi kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na Wateja hao

Soma https://jamii.app/GPSAKutukanaWateja

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Kutolewa kwa Elimu Bora huwapa Watu nafasi sawa ya kufanikisha ndoto zao, kuvunja mzunguko wa Umasikini na kujenga jamii yenye haki na usawa

Iwapo Watoto wananyimwa Elimu kwa misingi ya Jinsia, hali ya Kiuchumi au Ulemavu, basi tunawanyima fursa ya Maisha bora na kuzuia Maendeleo ya Jamii nzima. 

Tujitahidi kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu bila ubaguzi, Serikali inawekeza katika Mifumo ya Elimu inayofikia wote na tunapigania Sera zinazowezesha upatikanaji wa Elimu kwa makundi yote ya Jamii 

#ElimuNiHaki #JamiiForums #CivilRights #HakiZaKiraia #ElimuKwaWote #HudumaZaKijamii #ElimuKwaUsawaNaHaki
Japokuwa #Uwajibikaji ni msingi wa Maendeleo, tabia ya kujipendekeza kwa wenye Mamlaka (Uchawa) inazidi kuathiri Uwajibikaji wa Viongozi na Taasisi

Badala ya kuhoji, kusimamia, na kudai Uwajibikaji, baadhi ya Watu hujitokeza kutetea makosa kwa maslahi binafsi, jambo linalosababisha uvunjifu wa Maadili ya Utawala bora

Swali muhimu ni Je, ni kwa kiasi gani uchawa unachangia kuzorota kwa Uwajibikaji Nchini? Usikose kujiunga nasi katika kujadili tatizo hili na kutafuta suluhisho la kudumu kwa maslahi ya Taifa

Ni Alhamisi ya Februari 27 kuanzia Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku kupitia Xspaces ya JamiiForums

Kujiunga Bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #Governance #TukemeeUchawa
Katika andiko hili la kwenye Shindano la Stories of Change 2021, Mshiriki ameeleza mambo mengi ambayo atawafundisha Watoto wake kabla ya Kifo chake

Wewe utawafundisha Watoto jambo gani?

Soma Andiko hili kwa urefu zaidi kwa kubofya https://jamii.app/NitafundishaWatotoSOC2021

#JamiiForums #Maisha #SOC2021 #LifeLessons
"Ushawahi kusafiri kwenye Basi umekaa na Mtu yeye kila anachokiona njiani anakula tu" ni Mjadala unaoendelea JamiiForums.com kwenye Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko

Unaweza kushiriki Mjadala huu zaidi kwa kubofya https://jamii.app/KulaOvyoSafarini

#JamiiForums #JFChitChats #JFStories
👍1