JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kiongozi anayeanza safari ya uongozi kwa kujihusisha na Vitendo vya #Rushwa hujenga msingi wa Utawala usiozingatia #Haki na Maadili

Tabia hii husababisha matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo na ufisadi, hali inayodhoofisha imani ya Wananchi kwa Viongozi wao

Ni wajibu wetu kama Wananchi kuhakikisha hatuwapi nafasi Viongozi wanaotumia rushwa kujipatia madaraka

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
TANZIA: Rais wa Kwanza wa #Namibia, Sam Nujoma amefariki Dunia akiwa na umri wa Miaka 95

Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Afrika Kusini Mwaka 1990 ilipopata Uhuru. Moja ya matukio yake ya kukumbukwa ni Mwaka 1960 alipokimbilia Nchini #Tanzania kutokana na vuguvugu lililotokea Namibia, ambapo Hayati Mwalimu, Julius alimpatia hifadhi

Baada ya Uhuru alichaguliwa kuwa Rais na kudumu hadi Mwaka 2005 ambapo aliamua kustaafu ila alibaki kuongoza Chama cha South West Africa People's Organisation (SWAPO) hadi Mwaka 2007

Soma https://jamii.app/SamNujomaAfariki

#JamiiForums #Governance #JFMatukio #RIPSamNujoma
DODOMA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kufuatilia hali ya usafi wa Vyakula katika Soko la Sabasaba hasa msimu wa Mvua kwani inahatarisha Afya za Wananchi

Soma https://jamii.app/UsafiSokoSabasaba

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Shiriki katika Mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?" kupitia X Spaces ya JamiiForums

Usikose kujiunga nasi Februari 13, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 2 Usiku

Kushiriki, bofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
πŸ‘2
Elimu siyo tu Haki ya Msingi ya Binadamu, bali ni Msingi wa Maendeleo ya Mtu Binafsi, Jamii na Taifa. Miundombinu yake inapaswa kuboreshwa kila wakati kadiri uhitaji unavyoongezeka

Kuwepo kwa Madarasa ya kutosha, Madawati, Maabara za kujifunzia, Walimu wenye weledi pamoja na Mitaala ya Elimu inayobadilika kukidhi mahitaji ya Kijamii ni vitu vinavyofanya Elimu iwe Uwekezaji usiomalizika

Elimu huwapa Watu uwezo wa kujitambua, kudai Haki zao na kushiriki katika maamuzi ya Kijamii na Kisiasa. Jamii zilizo na kiwango cha juu cha Elimu zina uwezekano mkubwa wa kuwa na usawa wa Kijinsia, Kidemokrasia na Maendeleo ya Kiuchumi.

#Demokrasia #JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #Democracy #ElimuKwaWote
Mdau, unafanya nini kuhakikisha taarifa zako binafsi ziko salama mtandaoni?

Mjadala zaidi https://jamii.app/TaarifaBinafsiKutumikaVibaya

#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
πŸ‘1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka inayosimamia maboresho ya majitaka mitaa ya Mbezi Beach kwa Zena kurekebisha barabara badala ya kuziacha zikiwa zimefukuliwa ovyo kwani ni kero na kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na kusababisha changamoto ya usafiri na usalama kwa wanaotembea kwa miguu

Soma https://jamii.app/MifumoMajiTakaMbezi

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
πŸ‘1
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
πŸ‘1
Wanapokupa pesa leo ili uwapigie kura, jiulize, Kesho watachukua nini kutoka kwako? Je, ni haki zako za msingi, Maendeleo ya jamii yako, Huduma bora za afya, elimu au miundombinu?

Rushwa katika uchaguzi si msaada bali ni uwekezaji wa Viongozi wasiokuwa waadilifu ili wapate nafasi ya kujinufaisha kwa rasilimali za Umma

Uchaguzi ni nafasi yako ya kuleta mabadiliko, tumia haki yako kwa uangalifu. Usikubali thamani ya maisha yako na mustakabali wa Taifa kuwekwa rehani kwa pesa za muda mfupi

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
πŸ‘1
SONGWE: Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Boniface Kasululu ametolea ufafanuzi taarifa ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyedai baadhi ya maeneo ya Mkoa huo yana changamoto ya Wananchi kuumwa Magonjwa ya Tumbo na anahisi wengi wao wao wanasumbuliwa na Kipindupindu

Dkt. Kasululu amesema β€œSina taarifa hizo za Magonjwa ya Tumbo na Kipindupindu lakini unaposema suala limefika kwenye Kata maana yake Jamii inafahamu kinachoendelea. Sitaki kupuuza kuhusu suala hilo, lakini kwa sasa kila Mtaa kuna Zahanati na zote zinashughulika na Afya za Wananchi, kama taarifa hizo zipo na Mimi sina taarifa ngoja nifuatilie.”

Soma https://jamii.app/MagonjwaTumboTunduma

#JamiiForums #PublicHealth #Afya #Uwajibikaji #Accountability