JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kwa ushiriki zaidi, tembelea JamiiForums.com ili uweze kushiriki Mijadala mbalimbali Jukwaani au bofya https://jamii.app/MagerezaWanandoa

#JamiiForums #ConjugalRights
SIASA: Mchungaji Godfrey Malisa amefukuzwa uanachama na Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa

Aidha, hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa imetokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitishwa kwa Rais Samia Suluhu na Dkt. Hussein Mwinyi (Zanzibar) kuwania Urais wakiwa Wagombea pekee wa chama kumekiuka Katiba ya CCM

Soma https://jamii.app/MalisaAfukuzwaCCM

#JamiiForums #JFMatukio #Governance
#MALEZI: Mwanachama wa JamiiForums.com anasema Wazazi wana wajibu wa kutoa adhabu ya Haki kulingana na Umri, Jinsia, Uelewa na Akili ya Mtoto

Ametoa wito kwa Wazazi kuwafundisha Watoto kuomba Msamaha, ikiwa ni pamoja na kukubali (kukiri) Kosa na kuazimia kuwa hawatorudia, kwani wakirudia adhabu itakuwa kubwa zaidi

Aidha, ameshauri Wazazi kutowalinganisha Watoto wengine na kuwaonyesha kuwa ni mifano bora, wanaaminika na hawastahili kufanya Makosa kama waliyofanya

Unakubaliana na hoja za Mdau?

Shiriki Mjadala huu na mingine zaidi iliyopo JamiiForums.com au bofya https://jamii.app/AdhabuWatoto

#JamiiForums #ParentingsTips #SafariMaleziBora
1
Akilalamikia changamoto za Mfumo wa ESS, Mdau wa JamiiForums.com pia, amedai Wakuu wa Idara wamekuwa wavivu kuingia kwenye Mfumo kwa kisingizio cha kuwa wako 'busy' na majukumu na kuwaachia Maafisa Elimu Kata ambao kimsingi wengi wao nao ni wavivu wa kushughulikia suala hilo na hawajui chochote kuhusiana na Mfumo kwani nao wamekuwa wakiwaachia Wakuu wa Shule

Ametoa wito kwa Mamlaka husika kuliona hilo na kuwashughulikia Viongozi wanaoleta Uvivu kutimiza Majukumu yao

Soma https://jamii.app/ChangamotoMfumoESS

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #TEHAMA #ICT
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JamiiForums imeboresha mwonekano kwenye Kurasa za Mitandao ya Kijamii ili kukupa Mwonekano wa Kisasa na rahisi kwenye kuthibitisha Maudhui yake

Mwonekano huu mpya utakupa nafasi ya kushiriki Mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye Jukwaa letu pendwa la JamiiForums.com na zaidi ya yote utaweza kuhakiki uhalali wa maudhui hayo kwa kufuata Maelekezo yanayotolewa kwenye Video hii

Asante na endelea kufuatilia akaunti zetu kwa maudhui bora zaidi

#JamiiForums #GraphicsUpdate
1👍1
SINGIDA: Mdau wa JamiiForums.com anasema kuna kero moja kwa Manispaa ya Singida ambapo kumekuwa na tabia ya uchelewaji wa kuchukua taka katika baadhi ya maeneo hasa Ginery

Anaeleza Wananchi wanatoa taka nje siku ya kubeba Gari halipiti, hii ni wiki ya tatu taka zimezagaa kwenye mitaa tu, hili tatizo limeanza tangu Desemba 2024.

Soma https://jamii.app/TakaKuzagaaSingida

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii
👍21
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kushughulikia kero ya daladala zinazotoka nje ya Dar es Salaam, ruti Mbezi- Mlandizi zinazoishia Njuweni Maili Moja

Soma https://jamii.app/DaladalaKukatishaRutiMbezi

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
Kura siyo bidhaa ya kununuliwa au kuuzwa, ni haki yako ya msingi kama raia. Unapokubali kuuza kura yako kwa pesa au ahadi za muda mfupi, unakabidhi hatima ya nchi kwa watu wasio na nia njema kwa maendeleo ya jamii

Simama imara, linda kura yako na hakikisha unachagua kiongozi kwa misingi ya uadilifu, uwezo na dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Februari 13, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi Saa 2:00 usiku, tutakuwa na Mwanasheria atakayeelezea Sheria inasemaje kuhusu utoaji wa zawadi wakati wa Uchaguzi na mipaka yake Kisheria

Hii ni fursa ya kujadili, kutoa maoni, kupendekeza maboresho na kuuliza maswali kuhusu uwazi na uwajibikaji katika uchaguzi, hivyo usikose kujiunga nasi kupitia #Xspaces ya JamiiForums

Kushiriki kubofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
1
DAR: Wananchi wa Saranga Ubungo wameto wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange kushughulikia kero ya Maji iliyopo eneo hilo kwa maelezo kuwa ni changamoto kubwa kwa Wakazi wa eneo hilo

Akitoa ufafanuzi, Mkuu wa Wilaya amemuagiza Meneja wa DAWASA Kanda ya Kinyerezi kuzungukia nyumba ambazo zimejiunganishia huduma ya maji bila kufuata utaratibu, jambo linalosababisha Wananchi wengine kukosa huduma ya maji, ili marekebisho yafanyike

Naye, Meneja wa DAWASA, Crossman Makere amekiri kufahamu kuhusu kero hiyo na kusema imeanza kufanyiwa kazi kwani zoezi la ulazaji wa mabomba linaendelea

Soma https://jamii.app/UhabaMajiSaranga

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery