JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#NAMIBIA: WANAFUNZI ZAIDI YA 300 WAKUTWA NA #CORONAVIRUS

> Wizara ya Afya nchini humo imesema wanafunzi walioambukizwa wengi wao wanasoma Shule za Bweni

> Mpaka sasa #Namibia imethibitisha kuwa na jumla ya maambukizi 11,373 vya #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/COVID19Namibia
ATHARI ZA #COVID19: #NAMIBIA KUFUTA RIBA YA USHURU KWA 95%

> Wizara ya Fedha imepanga kufuta riba na kubatilisha adhabu zote kwa walipa kodi kuanzia Februari 2021

> Lengo ni kuwasaidia Wafanyabiashara wanaokabiliwa na matatizo ya Kiuchumi

Soma - https://jamii.app/TaxpayPenalties
NAMIBIA YASAINI MPANGO WA KIMATAIFA WA CHANJO YA #COVID19

> Taifa hilo limeidhinisha malipo ya Dola Milioni 1.7 kwa ajili ya chanjo ya Ugonjwa wa COVID-19

> #Namibia haiwezi kupewa ruzuku ya COVAX kwa kuwa ni nchi ya Uchumi wa Kati wa Juu

Soma https://jamii.app/NamibiaCOVAX
#NAMIBIA: WINGI WA TEMBO WASABABISHA SERIKALI KUWAUZA KWA MNADA

> Uamuzi huo umetokana na kuongezeka kwa matukio ya Tembo kuwashambulia Binadamu

> Idadi ya Tembo Nchini humo imeongezeka kutoka 7,500 mwaka 1995 hadi 24,000 mwaka 2019

Soma https://jamii.app/NamibiaMnadaTembo
UJERUMANI YAIOMBA MSAMAHA NAMIBIA KWA MAUAJI YA KIMBARI

#Ujerumani imekiri rasmi kufanya mauaji ya kimbari enzi za Ukoloni ambapo maelfu kutoka Jamii za Herero na Nama waliuawa

Nchi hiyo itaiunga mkono #Namibia kupitia Programu ya Maendeleo

Soma https://jamii.app/NamibiaGermany
#NAMIBIA: UPINZANI WAKOSOA MAKUBALIANO YA SERIKALI NA UJERUMANI

Walikubaliana kuhusu mauaji ya kimbari yaliyotokea wakati wa Ukoloni

Wapinzani wameishutumu Serikali kwa kuwaweka kando wao pamoja na Jamii zilizoathiriwa moja kwa moja na mauaji hayo

Soma https://jamii.app/OppNamibia
MICHEZO: SIMBA YAITAFUNA POWER DYNAMOS MAGOLI 2-0

Tamasha la #SimbaDay limemalizika vizuri kwa wenyeji kushinda, magoli yakiwekwa wavuni na #WillyOnana dakika ya 5 na #FabriceNgoma dakika ya 75, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam

Mchezo huo ni maalum ili kujiandaa kwa Msimu ujao wa 2023/24 kwa timu zote ambapo pia zina uwezekano wa kukutana katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa Dynamos itaitoa African Stars ya #Namibia kwenye Raundi ya Kwanza ya michuano hiyo

Soma https://jamii.app/SimbaDay23

#JFSports #JamiiForums
👍5
Kwa Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ripoti ya Global Gender Gap Report 2023 inaonesha Ukanda huu unashika nafasi ya sita kati ya nane, ukiwa umefikia 68.2% ya Usawa wa Kijinsia. Hii inamaanisha Maendeleo ya Usawa wa Kijinsia ni bora kuliko Kanda za Asia Kusini, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini

Hata hivyo, Maendeleo hayalingani miongoni mwa Nchi zilizopo katika Ukanda huu. #Namibia, #Rwanda, na Afrika Kusini, pamoja na nyingine 13, zimefanikiwa kufunga zaidi ya 70% ya pengo la jinsia. Lakini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, #Mali, na #Chad, zimebaki nyuma sana na kuwa na alama chini ya 62%.

Soma https://jamii.app/GenderGap

#JamiiForums #JFWomen #GenderEquality
👍7
BALOZI MBELWA KAIRUKI AHAMISHIWA UINGEREZA, KHAMIS OMAR APELEKWA CHINA

Rais Samia amemhamisha Balozi Mbelwa Brighton Kairuki kwenda #London ambako anachukua nafasi ya Dkt. Asha Rose Migiro ambaye amemaliza Mkataba wake

Balozi Ceaser Chacha Waitara anakwenda Ubalozi wa #Tanzania Nchini #Namibia akichukua nafasi ya Balozi Modestus Kipilimba aliyestaafu. Kipilimba aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) (2016-2019)

Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse anakwenda Ubalozi wa Tanzania Nchini #Kenya, anachukua nafasi ya Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene aliyehamishiwa Kampala, #Uganda

Ikumbukwe, mabadiliko haya yanakuja muda mfupi baada ya kauli ya Rais Samia kuwa alipata malalamiko kutoka kwa Rais mmojawapo katika Nchi za #SADC kuwa kuna Balozi wa Tanzania hawajibiki katika majukumu yake

#JamiiForums #Governance #Diplomacy
👍10
MWAKINYO: SITAPANDA ULINGONI

Pambano la #HassanMwakinyo dhidi ya Julius Indongo wa #Namibia kuwania Mkanda wa IBA Intercontinetal (Septemba 29, 2023) lipo hatarini baada ya Mwakinyo kudai kuna uongo na udanganyifu wa 'Mapromota' wa pambano hilo

Amesema kama changamoto zilizopo (hajazitaja) hazitatatuliwa basi msimamo wake utakuwa ni kutopanda ulingoni

Mabondia wote walipima uzito Mwakinyo Kilo 71.5, Indongo Kilo 69.85, awali, Mwakinyo alitakiwa apigane na Rayton Okwiri wa #Kenya lakini mabadiliko yakatokea dakika za mwisho

Soma https://jamii.app/MwakinyoAgoma

#JFSports #JamiiForums
👍51😁1
#MICHEZO: Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imetoa adhabu kwa Bondia Hassan Mwakinyo kutojihusisha na Mchezo wa Ngumi nje na ndani ya #Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na Faini ya Tsh. Milioni 1

Mwakinyo amekutwa na hatia ya kutoa kauli chafu dhidi ya Uongozi wa #TPBRC pamoja na kugomea pambano dhidi ya Bondia Julius Indongo kutoka #Namibia lililopangwa kufanyika Septemba 29, 2023, Dar es Salaam

Siku moja kabla ya uamuzi huo, Mwakinyo aliandika, "Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili, ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi, see you soon."

Soma https://jamii.app/MwakinyoBan

#JamiiForums #JFSports #Boxing
👍6
NAMIBIA: Serikali imeweka wazi taarifa za vipimo vya Afya vya Rais Hage Geingob (82) na kuueleza Umma kuwa kiongozi huyo amekutwa na Ugonjwa wa Saratani na anatarajiwa kuanza matibabu kama ambavyo Madaktari wake walivyoelekeza

Taarifa ya Serikali imesema kiongozi huyo amekuwa akifanya vipimo vya Afya mara kwa mara tangu aingie Madarakani Mwaka 2014 ingawa Wananchi walianza kuhoji kuhusu uimara wa Afya yake kabla hata hajaingia Ikulu. Hata hivyo, Serikali imesema Rais ataendelea na majukumu yake ya kikazi

#Namibia imekuwa kati ya Nchi chache Barani Afrika ambazo hutoa taarifa kuhusu Afya za Viongozi wake ikiwa ni tofauti na Serikali za Nchi nyingi ambazo taarifa za Afya za Viongozi huwa Siri na kusababisha Umma kupatwa na taharuki za mara kwaa mara

Soma https://jamii.app/PrezHage

#JamiiForums #Governance #Accountability #SocialJustice #AccessToInformation #JFSC
👍51
Baada ya Timu ya Taifa ya #Tanzania kushika nafasi ya mwisho katika Kundi F na kuondolewa kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (#AFCON2023), ratiba ya Hatua ya 16 imejulikana

Timu ambazo zimeingia hatua hiyo kupitia nafasi ya Mshindi wa Tatu Bora kwa kuwa na matokeo mazuri ni #Guinea, #Namibia, #Mauritania na wenyeji #IvoryCoast

Soma https://jamii.app/16BoraAFCON

#JFSports #AFCON #JamiiForums
👍41
#NAMIBIA: Rais #HageGeingob anatarajia kuanza Matibabu ya Saratani Nchini Marekani ikiwa ni Siku chache tangu Serikali ithibitishe kuwa Uchunguzi wa Kiafya umebaini ana Ugonjwa wa Saratani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, imesema shughuli zote za Urais zitakuwa chini ya Makamu wa Rais #NangoloMumba hadi Februari 2, 2024

Serikali ya Namibia imekuwa ikiweka wazi hatua zote za hali ya Kiafya ya Rais Geingob ikiwemo ya kugundulika kuwa ana tatizo la Saratani ya Tezi Dume pamoja na kufanyiwa upasuaji wa Mishipa ya Damu kwenye Moyo

Soma https://jamii.app/NamPress

#JamiiForums #Governance #Transparency #AccessToInformation
👍4
TANZIA: #Namibia imempoteza Rais wake, #HageGeingob ambaye amefariki Dunia wakati akiendelea na matibabu ya Saratani hospitalini katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Windhoek

Taarifa ya Makamu wa Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba imeeleza kuwa msiba huo umetokea usiku wa kuamkia leo Februari 4, 2024

Januari 2024, Rais Geingob na Serikali ya Namibia waliweka wazi kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi huyo na kueleza kuwa anasumbuliwa na Saratani

Soma https://jamii.app/HageGeingob

#Governance #HageGeingobDeath #RIPGeingob #JamiiForums
👍91
Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa aliyasema hayo wakati #Tanzania inajiondoa katika Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (The Common Market for Eastern and Southern Africa - #COMESA)

Nchi nyingine ambazo zilijiondoa katika Ushirika huo ni #Lesotho (1997), Msumbiji (1997), #Namibia (2004) na #Angola (2007)

#Diplomacy #Governance #JFQuotes #Economy #NukuuZaJF #Accountability #JamiiForums
👍1
Aliyekuwa Rais wa #Namibia, Hayati Dkt. Hage G. Geingob, alitoa kauli hiyo Agosti 12, 2022 wakati akiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana

Geingob alifariki Dunia Februari 4, 2024 baada ya kuugua Saratani ya Utumbo

#JamiiForums #GoodMorning #Accountability #AmkaNaJF #Governance #TopofTheMorning
👍1
RIPOTI: Nchi za Lesotho, Malawi, #Namibia, Zambia, Zimbabwe, #Angola na Msumbiji zimeripotiwa kukumbwa na hali mbaya ya Upatikanaji wa Chakula, hali inayosababisha takriban Watu Milioni 27 kutokuwa na uhakika wa Chakula

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), takriban Watoto Milioni 21 katika Nchi hizo wameripotiwa kuwa na #Utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa Lishe Bora

WFP imeeleza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo inayosababisha Watoto kupata Mlo mmoja au kukosa kabisa, zinahitajika takriban Tsh. Trilioni 1 (Dola Milioni 369) ambapo hadi sasa imepokea Theluthi moja tu ya kiasi hicho kutoka kwa Wafadhili.

Soma https://jamii.app/WFPFoodCrisis

#JamiiForums #Governance #FoodSecurity #Accountability
👍2
#NAMIBIA: Mahakama imeamuru Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yahakikiwe ikiwa ni uamuzi unaotokana na Kesi ya kupinga Matokeo hayo iliyofunguliwa na Vyama vya Independent Patriots for Change (IPC) na Landless People's Movement (LPM)

Tume ya Uchaguzi imeagizwa kuvipatia Vyama hivyo vifaa vya Uchaguzi Wiki ijayo ikiwemo idadi ya Kura zilizopigwa na kuhesabiwa katika kila kituo cha kupigia Kura kwaajili ya ukaguzi wao

Vyama hivyo vilifungua Kesi baada ya Matokeo kutangazwa ambapo viliituhumu Tume ya Uchaguzi kutowajibika ipasavyo katika zoezi la Uchaguzi huku baadhi ya Vituo vikidaiwa kukosa Karatasi za Kura

Soma https://jamii.app/NamibiaCourt

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #SocialJustice
TANZIA: Rais wa Kwanza wa #Namibia, Sam Nujoma amefariki Dunia akiwa na umri wa Miaka 95

Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Afrika Kusini Mwaka 1990 ilipopata Uhuru. Moja ya matukio yake ya kukumbukwa ni Mwaka 1960 alipokimbilia Nchini #Tanzania kutokana na vuguvugu lililotokea Namibia, ambapo Hayati Mwalimu, Julius alimpatia hifadhi

Baada ya Uhuru alichaguliwa kuwa Rais na kudumu hadi Mwaka 2005 ambapo aliamua kustaafu ila alibaki kuongoza Chama cha South West Africa People's Organisation (SWAPO) hadi Mwaka 2007

Soma https://jamii.app/SamNujomaAfariki

#JamiiForums #Governance #JFMatukio #RIPSamNujoma