JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#MICHEZO: Bondia wa ngumi za kulipwa, Twaha Kiduku, ameshinda Ubingwa wa Afrika/Mabara (UBO Intercontinental Super middle weight) baada ya kumpiga Bondia Abdo Khaled, Raia wa Misri kwa pointi katika pambano la round 10 lililochezwa Mtwara

Twaha Kiduku ameshinda Mikanda miwili ya UBO, mmoja akiwa ameutetea aliokuwa nao

#JFSports #Boxing
πŸ‘11πŸ‘7
NDONDI: ALIYESIMAMIA PAMBANO LA MANDONGA ASIMAMISHWA

TPBRC imemsimamisha kwa muda Habib Mohammed (Mkarafuu) kutokana na kasoro za kimaamuzi katika pambano la Karim Mandonga na Salim Abeid, hadi atakapopata Mafunzo ya Uamuzi

Soma - https://jamii.app/NdondiTZ

#JFSports #Boxing
πŸ‘18😁11πŸ‘1
NDONDI: PAMBANO LA FURY NA USYK HATARINI KUTOFANYIKA

Pambano limepangwa kufanyika Aprili 29, 2023 lakini #OleksandrUsyk anamlaumu #TysonFury kuwa kikwazo

Timu ya Usyk imedai licha ya Fury kukubaliwa kunufaika katika mgawanyo wa malipo kwa asilimia 70-30, amekuwa akitoa masharti mengi ambayo yameonekana kumkwaza Usyk anayeshikilia mikanda ya #WBA, #WBO na #IBF ya uzito wa juu

Soma https://jamii.app/FuryUsyk

#JFSports #Boxing
πŸ‘4❀3
Bondia #AnthonyJoshua anayetarajia kuzichapa na Bondia Jermaine Franklin Aprili 1, 2023 ndani ya O2 Arena, jijini London amesema ataachana na Masumbwi endapo atakutana na kipigo kutoka kwa Bondia #JermaineFranklin

Bingwa huyo mara mbili wa Dunia atapanda Ulingoni kutetea Heshima yake baada ya kupigwa na #OleksandrUsyk, huku pambano lake la mwisho kushinda likiwa Desemba 2020

Soma https://jamii.app/AJLastDance

#JFSports #Boxing
πŸ‘5❀2
NDONDI: TWAHA KIDUKU AMCHAKAZA IAGO KIZIRIA KWA POINTI

Bondia #TwahaKiduku ameshinda na kutetea Mikanda ya PST na UBO Inter Continental, Uzito wa kati Super Middleweight (Kilogram 76) kwenye Ukumbi wa Tanzanite Mkoani #Morogoro

Majaji watatu wamempa ushindi Kiduku kwa Pointi 98-92, 98-92, 97-93 licha ya mpinzani wake ambaye ni raia wa #Georgia kuonesha upinzani mkali katika Raundi zote 10

Soma https://jamii.app/KidukuKiziria

#JFSports #Boxing
πŸ‘13
#MICHEZO: Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imetoa adhabu kwa Bondia Hassan Mwakinyo kutojihusisha na Mchezo wa Ngumi nje na ndani ya #Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na Faini ya Tsh. Milioni 1

Mwakinyo amekutwa na hatia ya kutoa kauli chafu dhidi ya Uongozi wa #TPBRC pamoja na kugomea pambano dhidi ya Bondia Julius Indongo kutoka #Namibia lililopangwa kufanyika Septemba 29, 2023, Dar es Salaam

Siku moja kabla ya uamuzi huo, Mwakinyo aliandika, "Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili, ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi, see you soon."

Soma https://jamii.app/MwakinyoBan

#JamiiForums #JFSports #Boxing
πŸ‘6
MICHEZO: Serikali kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, imesema kuna haja ya kufuatilia utaratibu uliotumika katika mashtaka ya Bondia Hassan #Mwakinyo ili kubaini Uhalali wa adhabu aliyopewa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)

Ndumbaro amesema β€œSisi kama Wizara tutakaa na BMT (Baraza la Michezo la Taifa) na TPBRC, ili kupata taarifa rasmi ya kilichotokea na tutashauriana na wahusika wote kuhusu adhabu ilivyotolewa na uhalali wake. Kama adhabu ni sahihi ataitumikia, au kama kuna mushkeli kidogo tutakaa na kushauriana tunafanyaje,”

Oktoba 10, 2023 TPBRC ilitangaza kumfungia Mwakinyo kujihusisha na Ndondi ndani na nje ya Nchi kwa Mwaka mmoja na Faini ya Tsh. Milioni 1 baada ya kumkuta na hatia ya Kugomea Pambano licha ya kusaini Mkataba na Promota

Soma https://jamii.app/BanMwakinyo

#JamiiForums #JFSports #Boxing
πŸ‘5❀1πŸ”₯1
NDONDI: Bingwa wa Mkanda wa WBC Afrika, Fadhili Majiha 'Kiepe Nyani' amekuwa bondia wa kwanza wa #Tanzania kupata hadhi ya nyota Nne na 4.5 akivunja rekodi ya #HassanMwanyiko na #TonyRashid katika Mtandao wa #Boxrec

Majiha amefikia kiwango hicho wiki moja baada ya kushinda kwa pointi dhidi ya Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini, pia anashika nafasi ya 7 kati ya 1,056 uzani wa Bantam

Mwakinyo ndiye bondia wa kwanza Nchini kufikia Hadhi ya Nyota 4, kwa sasa ana nyota 2 (Super Walter), Tony Rashid ana nyota 2.5 (Super Bantam)

Soma https://jamii.app/RekodiZaNdondi

#Sports #Boxing #JamiiForums
πŸ‘7