JamiiForums
56K subscribers
33K photos
1.91K videos
30.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
Je, uko tayari kwa hiki kipya tunachokuletea?

Pamoja na kutangazwa kwa Washindi wa Maandiko Bora ya Msimu wa Nne wa #StoriesOfChange (#SoC04) na Waandaaji Bora wa Maudhui kutoka JamiiForums.com, kuna jambo jipya na la kipekee linalokuja usiku huo wa Septemba 21, 2024

Uko tayari kwa hii 'surprise'? Hili halijawahi kutokea! Usisahau kufuatilia akaunti zetu za Mitandao ya Kijamii ili usipitwe na lolote.

#JamiiForums #JFSuprise #StoriesOfChange2024 #TanzaniaTuitakayo #SoC2024
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#DIGITALI: Jukwaa la Kidigitali katika Uhakiki wa Taarifa la #JamiiCheck linaloendeshwa na #JamiiForums limeshinda Tuzo ya U.S.-Tanzania Tech Challenge iliyokuwa ikiwaniwa na Taasisi 113 za Kiteknolojia kutoka Tanzania

Shindano hilo liliandaliwa na Marekani kupitia Ubalozi wake nchini ambapo JamiiForums kupitia Mradi wake wa "Mwananchi Makini" inalenga kuhakikisha Wananchi wanakuwa na Taarifa Sahihi ili kufanya Maamuzi Sahihi wakati wa Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025

Ikumbukwe, JamiiCheck inawapa Wananchi fursa ya kuwasilisha taarifa ambazo hazijathibitishwa, kushiriki katika mchakato wa kuzihakiki na kupokea tathmini ya ukweli wake ndani ya muda mfupi

Soma https://jamii.app/USTechChallenge

#JamiiForums #JamiiCheck #JFDigitali #FactChecking #Accountability #DigitalRights #USTZTech
DIGITALI: Ni muhimu kuwa makini unaponunua simu iliyotumika kutoka kwa Mtu mwingine kwani muda mwingine wauzaji sio waaminifu

Hatua hii ni muhimu ili kuepuka kununua 'simu za wizi' au zilizotumika katika kufanya matendo ya kihalifu au kununua simu mbovu bila kujua

Mdau unaponunua simu iliyotumika au ya Mtu mwingine huwa unazingatia nini kwanza?

Soma https://jamii.app/TipsBuyingUsedPhones

#JamiiForums #JFDigitali #DigitalSecurity #DigitalSafety #DataProtection #DigitalWorld
#FewHoursToGo! Hafla ya utoaji wa Tuzo za Shindano la Stories of Change (#SoC) Msimu wa 4 inatarajiwa kufanyika kesho, Septemba 21, 2024

Mwaka huu Washiriki wameonesha uwezo wa juu katika kuijenga 'Tanzania Tuitakayo' wakilenga kuboresha #Uchumi, #Elimu, #Afya, #Teknolojia, #Kilimo n.k

Mbali na zawadi kutolewa kwa Washindi wa Maandiko Bora Usiku wa Septemba 21, 2024, Wazalishaji Bora wa Maudhui kutoka JamiiForums.com watatambuliwa na kutuzwa kwa mchango wao mkubwa katika Majukwaa yetu ya Kidijitali

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
MARA: Jeshi la Polisi linawashikilia Watu 18, wakiwemo Dereva, Kondakta na Abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa Usalama Barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda

Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, Saa 12 Jioni, ambapo Askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha Abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari

Ameelezea, Askari huyo alipoingia ndani ya gari, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia

Amesema “Askari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke, ghafla wakamzonga kwa maneno ya kebehi na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?”

Soma https://jamii.app/TrafikiMara

#JamiiForums #SocialJustice #Accountability #ServiceDelivery
MAREKANI: Rapa Sean Combs maarufu #Diddy, ameripotiwa kuwekwa katika uangalizi maalum ili kumuepusha na uamuzi wa Kujiua kutokana na kunyimwa dhamana baada ya kukamatwa, akituhumiwa kwa Utapeli, Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Utumikishaji Kingono

Jarida la 'People' limesema hatua hiyo imechukuliwa kama tahadhari kwasababu, Diddy aliyewekwa katika Gereza la Metropolitan Detention Center (MDC) huko Brooklyn (New York), yuko katika mshtuko tangu alipokamatwa na hali yake Kiakili bado haifahamiki

Aidha, taarifa zinaeleza Gereza la MDC lina sifa mbaya ikiwemo mazingira machafu, ukatili kwa wafungwa wageni kutoka wafungwa waliokaa muda mrefu pamoja na kesi za kujiua
-
Soma https://jamii.app/DiddyDidIt

#JamiiForums #JFMatukio
DAR: Mdau anadai matumizi ya Barabara ya Bagamoyo (Mwenge - Tegeta) ya Mwaka 2010 ni tofauti na ilivyo 2024 au itakavyokuwa baadaye hasa ukizingatia sasa inajengwa barabara ya magari ya Mwendokasi, hiyo inamaanisha maboresho yanatakiwa kuendana na matumizi na mazingira

Akizungumzia eneo la Bondeni ambapo kuna daraja kubwa, amestaajabu kuona maboresho ya barabara hiyo bado yanatengeneza daraja la kupitisha Mwendokasi kama lililokuwepo wakati mto huo unakula kingo zake kila mvua zinaponyesha

Amehoji kwanini pasijengwe daraja la juu kuunganisha Kituo cha ‘Kwa Komba’ na eneo la Taa za Kawe? Amedai kinachoendelea ni upotevu wa fedha za umma na ujenzi wa miundombinu isiyodumu kwani siku si nyingi daraja linalojengwa sasa linaweza ‘kumezwa’ na upana wa Mto

Soma https://jamii.app/DarajaMbeziMwendokasi

#JFHuduma #JamiiForums #JFUwajibikaji
#TheWaitIsOver! Bado saa chache tu kabla ya kuwafahamu walioibuka kidedea katika Msimu wa Nne wa Stories of Change 2024

Kupitia Maandiko yao, Mwaka huu (2024) Washiriki wameonesha ujuzi, maarifa na ubunifu wa hali ya juu, wakilenga kuboresha Sekta mbalimbali Nchini kwa Miaka 5-25, kwa kuandika kuhusu #TanzaniaTuitakayo

Mbali na Washindi wa Maandiko Bora kupewa tuzo, Wazalishaji Bora wa Maudhui ndani ya JamiiForums.com watatambuliwa kwa mchango wao katika majukwaa usiku wa leo

Soma https://jamii.app/FewHoursToSoCAwards

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
Zikiwa zimebaki saa chache kuelekea Utoaji tuzo kwa Washindi wa Msimu wa Nne wa Shindano la Stories of Change (2024) tujikumbushe Washindi wa Msimu wa Kwanza (2021), Msimu wa Pili (2022) na Msimu wa Tatu (2023)

Mdau kaa tayari kuwajua Washindi watakaoibuka kidedea katika Shindano la Stories of Change Usiku wa leo, Septemba 21, 2024

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #SoCWinnersNight #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
#STORIESOFCHANGE: JamiiForums inafanya Hafla ya Utaoji wa Tuzo kwa Maandiko Bora ya Shindano la Stories of Change 2024, inayofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam, leo, Septemba 21, 2024

Kupitia Maandiko yao, Mwaka huu (2024) Washiriki wameonesha ujuzi, maarifa na ubunifu wa hali ya juu, wakilenga kuboresha Sekta mbalimbali Nchini kwa Miaka 5-25, kwa kuandika kuhusu #TanzaniaTuitakayo

Halfa hii imehudhuriwa na Mabalozi, Viongozi wa Kiserikali na Watu Mashuhuri. Mgeni Rasmi wa halfa hii ni Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya kwa Tanzania, Christine Grau

Kufuatilia https://jamii.app/SoC2024

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange2024 #SOCWinners #SOCWinnersNight